Jamaa anamuoa mchumba wa rafiki yake kama mke wa pili

Jamaa anamuoa mchumba wa rafiki yake kama mke wa pili

Nilikuwa napenda hadi napenda tena....ila kuna kitu kizito nilipigwa aseee ndo akili ikafunguka kwamba kumbe dunia ninayoishi sio kabisa kama ya wengine. Siku hizi najiona kama vile nimegraduate....ili ujifunze kazima uumie hadi moyo ufe ganzi ndo utaelewa
Nshaumia sana tuuu!ila ndo nilivyo am the believer of one man hapo ndo nachekwaga sana na mashosti they think am a dumb stupid creature to exist...!!!
Ila haya maisha kwa sasa nkikuta mtu anadanga simhukumu na nikikuta mtu katendwa pia simhukumu huwezi jua pia...!!!

Ila huyo Dada kachemka sana yaani kama @deepond alivosema anafanyiwa vyote then kaenda kuuingia ukewenza...hyo Kali yaani itakula kwake
 
Very sad,of all people akachagua rafiki ya boyfriend wake????!!! Mtu wa hivi yuko soo heartless ....huyo muowaji ajiandae, kuwa na mtu wa hivi ni ngumu sana,hana moyo she can do anything.
.
KWAKWELI Bora hata nyie wanawake wenzake mmeliona.

Najaribu kuimagine
Uyu mwanamke anaroho Kias gani,

Ni ukatili ulopitiliza[emoji26]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kujifanyaga marafiki mpaka mnaunganisha family affairs zenu na wake/waume zenu matokeo yake huwa ndio kama haya...Jifanyen wazungu tu..HAPA STORI TU, KULA KILA MTU KWAKE.
[emoji2][emoji1][emoji1][emoji1][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Na kisingizio chao kikubwa "NIMELAZIMISHWA"
yaani 2021 Kuna mtu analazimishwa kuolewa tena mtu aliyeenda shule?

Huyo ameamua
Ameipenda polygamy

Au pengjne anafanya research ya polygamy ili atunukiwe masters degree yake[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Uyu mwanamke Ni mhuni tu,
Kwenye sim anaonekana kujutia, kujilaumu na kuwalaumu wazazi na ndugu zake mpk anatokwa na machozi.
Ila huwez amini alitupaki usiku mzima kumsubir yeyee na hakutokea.

Nakwa maelezo ya shoga Ake jana alivokwenda kwao, haonekani mwenye hofu Wala wasiwasi wowote.

Yuko sawa TU anaendelea na shughuli zake like nothing happened.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka 4 unakaa na mwanamke ambae anataka kuolewa wewe huendi kumuoa unategemea nini? Msela katokea mda mfupi kamuahidi ndoa na akafanya kweli.

Mwambie apige moyo konde mshkaji wako, next time akitaka mwanamke wa kumuoa asicheleweshe.
Ndoa ilkua ni mwakani mkuu Wala hakukua na tatizo Wala kinyongo chochote kwa mwanamke husika.

Wote walikua happy kufunga ndoa mwakani,

Hili lililotokea hapa katikati imekua Ni surprise Sana mkuu, ukizingatia Ni jins gan Hii couple ilipendana na malengo walokua wamejiwekea[emoji26]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkitoka out ya mbali na wenzi wenu au wachumba kimakundi basi jua lolote linaweza tokea . Mmoja wenu lazima aharibu kwa rafiki yake. Na kutongoza huwa ni rahisi sana. Mashemeji wanakulana sana, mkirudi tayari kuna mahusiano yameingia mdudu.
Huwa tunatoka Mara kwa mara na Tumezoea kuachiana familia wengine wanapokua mbali safari za mbali kikazi.

Nnachohisi huu mchakato umeanza MDA,

Kiukweli
Hili Jambo limeumiza Sana Moyo[emoji17]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo wanatanguliza hisia mzee, hapo jamaa atakuwa kamuimbisha Kwa maeneno matamu , kama kawaida ya michepuko mwishowe kabeba mazima
Vipi kuhusu kusimamia shoo? Labda brother big kamfunika dogo kwenye shoo??
 
Uyu mwanamke Ni mhuni tu,
Kwenye sim anaonekana kujutia, kujilaumu na kuwalaumu wazazi na ndugu zake mpk anatokwa na machozi.
Ila huwez amini alitupaki usiku mzima kumsubir yeyee na hakutokea.

Nakwa maelezo ya shoga Ake jana alivokwenda kwao, haonekani mwenye hofu Wala wasiwasi wowote.

Yuko sawa TU anaendelea na shughuli zake like nothing happened.


Sent using Jamii Forums mobile app
Anacheza kwene umri gani huyo bidada? Ukute ni kadogo bado hata hajui nini anataka
 
Nawaza kumshauri rafiki yangu, ashirikiane na uyu mwanamke.
Kisha binti atoroshwe akawekwe mafichoni kwa sikU kadhaa Hadi ile harusi ilopangwa itakapopita.

Uyu B atakapomtafuta akakosa Basi Iyo Ndoa ya kulazimisha itakua imeota manyoya.

Afu Sasa uyo B aje kwetu kulalamika kwetu katoroshewa MKE, na sisi tuje tumuoneshe kua upumbavu hatutaki.

SIJUI KAMA NIKO SAHII AU LAH[emoji848]

ushauri wenu tafadhali

Acha mawazo ya kijinga (excuse my language)...

Kama ulivyoeleza yote ni kweli(sio chai) basi huyo binti ni pimbi wa mwisho kwa sababu haeleweki...

1. Anadai anampenda sana dogo
2. Anadai anapendwa sana na B tokea muda mrefu amekuwa akimuhitaji, hii ina maana huyo mwanamke katongozwa na kakubali...
3. Anadai wazazi na ndugu zake wanampenda sana B, je hao wazazi walijuaje uwepo wa B wakati miaka yote minne wanatambia kuna dogo, jibu ni kuwa mwanamke mwenyewe ndio alimtambulisha B kwa wazazi wake na kumtambulisha huko lazima alisema ameshaachana na dogo...

Conclusion:
Huyo mwanamke ana mahesabu yake, achaneni naye, mnavyombebeleza mnazidi kumpa kichwa...

Mwambie dogo wachuchu wapo wengi sana hadi wengine wanajiuza...
 
Ni jamaa zangu wawili wameingia katika SINTOFAHAMU kubwa sana kwasababu ya mwanamke,

Nmewaza hapa mpaka kichwa kinaniuma sahivi.

KWA KUANZIA,
Ni kwamba mimi pamoja na hao jamaa zangu wawili sote Ni wafanyabiasha wa bidhaa Aina Moja.
Ofisi zetu ziko jirani pia (mji ule ule), Mara kwa mara husafiri pamoja kufata Mzigo, husaidiana hapa na pale mmoja wapo anapokua amekwama n.k

Kiukweli, Kwa sasa wote Tumekua marafiki Tena zaidi ya ndugu maana ukaribu wetu una mwaka wa 10 na zaidi Sasa.

Mimi na brother (Namuitaga brother coz katupita wote kiumri) wote tumeoa .

Ila Dogo wetu uyu
(tunamwitaga dogo coz wote tunamzidi kiumri) hajaoa bado ila ana mchumba wake wakike wamedumu miaka 4 Sasa na alkua alkua anategemea mwakani afunge nae ndoa baada ya kumalizia ujenzi wa nyumba yake ya kuishi na familia.

Kama unavojua marafiki watatu tuloshibana miaka na miaka huamua kuziunganisha familia zetu pamoja na mwaka Jana mwezi Kama huu Tuliunganisha familia zote 3 (mimi na familia yangu, brother na familia yake, Dogo na mchumba wake) tukaendelea wote tukapanda gari Moja kwenda kutalii pamoja MIKUMI na kurudi pamoja.

Boxing day ya mwaka huu nayo tulipanga itukute wote SERENGETI tukaenjoy na familia zetu.

KILICHOTOKEA JANA,
Nikiwa njian asbh naelekea bank, nkapita ofsin Kwake nkaona pamefungwa.

Wakat wa mchana Tena narudi nkaona bado pamefungwa,

Ikabid nimpigie
"vipi dogo mbona ofsin ufungui leo ndugu yangu?"

Dogo akanambia anamatatizo makubwa , Kama naweza niende nyumban kwake,
Anamaongezi na Mimi na kuna kitu kinamchanganya Sana kichwani anajihisi anatamani TU aage dunia.

Nilipofika akaanza kinisimulia,
" kaka Mchumba wangu wa miaka yote J kanisaliti, wiki ijayo ni ndoa yake anaolewa na mtu mwingine, Na keshalipiwa mahali tayar".

Dah! Moyo ulienda mbio Sana sikuamini maneno Yale. [emoji848]

Nkamwambia
"Acha masihara wewe, iyo haiwezekan[emoji848]"

Akasema
"wee kama huamini mpigie rafiki yake wa karibu Mama P akwambie kila kitu maana mimi kila nikipiga simu yangu hapokei, nilipomtafuta shoga Ake mama p ndo kanieleza kila kitu"

Basi nikaendelea hewan kumcheki uyo mama p,
Kwa maelezo ya mama p

"Shemeji Mimi mwenyewe mwanzoni sikuamini nilichokiona, J.pili ilopita shoga angu J alinialika kua analipiwa mahali nihudhurie shughuli yake, nikajua rafiki ako ndo atakua anahusika.
Nilifika tukapika na kumpamba mwali kwa ajili ya ugeni wa washenga kuleta mahali nikastuka kuona mhusika Ni rafiki yenu B"

"Kwaiyo Mimi sijui Nini kinaendelea nikajua masihara, Ila baadae mashehe wakachoma ubani na Dua mbalimbali na Dua ikawa ni kuombea baraka uchumba wa B na J"

Dah! Wakuu ,
Kiukweli moyo ulistuka sana, nikawaza mambo mengi Sana tuloshea na Kaka etu uyu.
Inawezekanaje kaka B amuoe J wkt Ni shemeji yake kabisa Yule na wanaheshimiana Sana.

Inakuaje kuaje amfanyie mwenzetu ishu Kama hiyo.

Basi inabidi nimkatie uyu mdada simu nikampigia uyu brother etu Kama ni kweli hizi habar.

Jamaa bila hata hofu akanambia,
"Hizo habari Ni kweli, J namuoa mimi na amekubali kabisa kusilimu na atakua MKE wangu wa pili."

Nkamwambia,
"Brother Unakosea sana, uyo Ni mchumba wa Dogo uyo na wewe unalifahamu Hilo na Wana mwaka wa 4 huu Sasa"

Akasema,
"Kaka Mimi mambo yao hayanihusu, nnachojua washaachana nakwasasa nnachojua Mimi na J ndo tunapendana na mahali nishalipa tayar. Na ndoa Ni mwezi huu mwishoni. Kama mnaweza nisapoti sawa kama hamtapata nafasi haina shida ntalimaliza TU mwenyewe"

Nkamwambia,
"Brother Unakosea Sana, wee sio wa kumfanyia hivyo Dogo, ukzingatia Dogo ndo alkua anamtegemea uyo awe MKE wake wa Kwanza maishani mwake, na wewe Umeshaoa tayari na unajua kila kitu khs Hawa madogo tangu mwanzoni"

Akasema,
"Kaka , sahivi Mimi Sina MDA wa kulijadili hili, Kama Kuna malalamiko Basi amlaumu mwanamke wake maana yeye ndo anataka kuolewa na Mimi. Na Mimi Sina tatizo na Hilo. Mchana mwema Kaka, kuna mahali nawai."

Kisha akakata simu.

Dah!
Kiukweli Maneno Yale yaliniumiza Sana.

Dogo nahisi yalimuumiza zaidi mpaka akawa anabubujikwa na machozi pamoja na kamasi utadhani mtoto mdogo maana simu ilikua loudspeaker MDA ule.

Sahivi
Nmewaita jamaa zetu wengine wawili waje hapa kwa Dogo wamuweke sawa, maana Hali nnayomuona nayo asijekaa peke Ake akajidhuru.

Nmeaga naenda kufunga Ofisi narudi tukae nae kufikirie tunamshaur vipi kuhusiana na ili.....

USHAUR WENU kwenye hili Ni muhimu Sana wakuu,

Natanguliza shukran[emoji120]
Dogo akomae atafute mwanamke mwingine manake uchumba wa miaka minne tayari amefanya research ya kutosha na ana P.H.D ya uchumba sasa ni wakati wa kutafuta mtu wa kufunga nae ndoa rasmi..
 
Update....
Ni kwamba mwanamke alinyang'anywa simu ya awali alokua anatumia na kapewa simu mpya yenye line mpya ya Airtel.

Nmefanikiwa kuipata hio namba na nmempigia na kuongea mwanamke mwenyewe.

Anasema,
"Shem mi sio kwamba simpendi rafiki ako, nampenda sana na nilitamani awe mme wangu. Sema rafiki ako hakua serious na Mimi. Miaka 4 yote tangu ameleta barua hamna kinachoendelea. Familia inanisumbua Sana afu nikimwambia hataki kunielewa anadai mpaka amalizie nyumba yake. Nyumba imeisha anadai finishing bado. Hivi kweli shemej nyumbA inaweza mzuia mtu wasifunge Ndoa? Hivi kweli anachonifanyia mwenzako unaona Ni sahii."

Nikamjibu,
"Kwaiyo meji ukaona Njia rahisi Ni kuolewa TU na rafki yake, hujui itamuumiza Kias gani?"

Akasema,
"Shemej nikwambie TU ukweli, uyu B tangu mwanzoni ashaonesha ananipenda Sana. Afu tangu zaman keshaonesha Nia ya kunioa MDA mrefu. Sema Mimi TU ndo nilikua kikwazo, afu kingine uyu B anakubalika Sana uku nyumban.

Shemej presha kwa familia yangu kuhusu B Ni kubwa Sana, Baba na mama na dada zangu wote wanataka niolewe na B. Imefkia mpaka mama ananambia uyu alonichumbia Ni mhuni TU miaka 4 Ni uchumba sugu huo. Imefkia mpaka baba haniongeleshi kisa sitak kuolewa na B. Na wote washanambia nisipoolewa B Mimi sitokua mwanao Tena na watanifuta kwenye ukoo.

Shemej yang mi mwenywe Niko Njia panda apa, moyoni mwangu B hayupo kabisa ila nalazimishwa TU na familia yangu. Uto rafiki yako hawamtaki kabisa ata kumskia uku nyumbani."

Nikamwambia,
"Kwaiyo shemej uko serious kabisa umelazimishwa Hii ndoa?"

Akasema
"Ndio Shem, yaan naomba TU uniombee msamaha TU kwa rafk yako. Mi bado nampenda Sana."

Nikamwambia,
"Bas Shem naomba ufanye jion tuonane ata kwa jamaa tujue tunaliwekaje hili"

Akasema,
"Sawa, ila Mimi kwa jamaa siwez kuja tena.italeta balaa. Labda yeye ata aje kwako niwakute apo kwako"

Nikasema,
"Sawa"

Ninachowaza Sasa,
Kama ni kweli uyu mwanamke kalazimishwa. Na kweli ANAMPENDA jamaa.

Nawaza kumshauri rafiki yangu, ashirikiane na uyu mwanamke.
Kisha binti atoroshwe akawekwe mafichoni kwa sikU kadhaa Hadi ile harusi ilopangwa itakapopita.

Uyu B atakapomtafuta akakosa Basi Iyo Ndoa ya kulazimisha itakua imeota manyoya.

Afu Sasa uyo B aje kwetu kulalamika kwetu katoroshewa MKE, na sisi tuje tumuoneshe kua upumbavu hatutaki.

SIJUI KAMA NIKO SAHII AU LAH[emoji848]

ushauri wenu tafadhali

Dah! Jamaa huwez Amin alkua anamgharamia Yule mwanamke utadhan mke wake wa Ndoa.

Jamaa yangu Ni form four, ila alipambana kumlipia Ada mpaka binti uyu kamaliza chuo kikuu.

Kibaya Zaid ata hapo sheli anakofanya kazi uyu binti, jamaa ndo kamuunganisha na ndo mdhamini wake.

Binti kapangiwa nyumba nzima, anaishi kwa Raha Sana.

Jamaa alkua analipa kila kitu khs mahitaj yake yote ya nyumbani mpaka dharula za familia yake.

Gari anayotembelea kamnunulia uyu jamaa,
(Tena nilishiriki ipasavyo kwenye mchakato mzima wa kuiagiza mpak kuitia mkononi)

mafuta juzi juzi TU tunatoka gym alipitia she'll kumuwekea ya 350,000 kwa ajili ya mizunguko yake.nikishuhudia mwenyewe.

Mshahara anaolipwa sidhan hata Kama uwa anaugusa kabisa.

Kwakweli,
alichomfanyia jamaa Ni zaidi ya unyama[emoji26]

Binti analalamika eti jamaa alikuwa Anaona hayuko serious
Msimtaftie mwenzenu matatizo huyo binti ni mjinga na hafai. Yan huduma zote hizo alizopewa bado haliona jamaa hayupp serious nae? Hapo hakuna ndoa ya kulazimishwa wala nini sijawainona ndoa ya kulazimishwa na ndugu kwa mtu wa dink tofauti na ya kwenu. Huko kujiloza ni maigizo tu yakuficha aibu
Bas tambua ata mkimtorosha bado ipo siku atamkimbia kwa kisingizio kingne.

Ashukuru Mungu kwa kumfunulia hili mapema
 
Mshauri dogo aaachane nao. Japo ni kama ngumu kwa wanaochipukia mapenzi. Mwanamke tu?. Biashara yake iko strong..! mwambie asonge mbele na mambo yake. Asitetereke.

Huwezi jua MUNGU kamuepushia na kitu gani mbele. Tena ajitahidi sana asimfikirie tena huyo mwanamke. Amfute kabisa kichwani.

Pia mwambie awe mtulivu sana kwa sasa. Asikimbilie kuvuta ngoma ingine. Avute pumzi kama mwaka akisikilizia.

Ajabu huyo mwanamke hautapita muda ataanza kumsumbua dogo. Ksbb dogo atakuwa tayari amemfuta kichwani haitampa shida. Wala asijaribu kushughurika nao kwa lolote. Awasamehe ksbb pia atakuwa amejisamehe na yeye pia. Hao MUNGU ndie atashughurika nao. Malipo yapo hapa hapa duniani.
 
Huwa tunatoka Mara kwa mara na Tumezoea kuachiana familia wengine wanapokua mbali safari za mbali kikazi.

Nnachohisi huu mchakato umeanza MDA,

Kiukweli
Hili Jambo limeumiza Sana Moyo[emoji17]

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo kitu ni hatarii. Hata wewe itakuja kukuta usipokuwa makini.

Kama haupo usiruhusu rafiki yako atembelee familia yako utakuja kumlaumu mke wako bure mambo huanza polepole kwa kuzoeana. Hata wewe kama jamaa yako hayupo hakuna kutembelea familia yake ni mpaka ipigwe simu kukiwa na shida muhimu. Piga simu mara mojamoja tu kujua wanaendeleaje basi.
 
Hiyo kitu ni hatarii. Hata wewe itakuja kukuta usipokuwa makini.

Kama haupo usiruhusu rafiki yako atembelee familia yako utakuja kumlaumu mke wako bure mambo huanza polepole kwa kuzoeana. Hata wewe kama jamaa yako hayupo hakuna kutembelea familia yake ni mpaka ipigwe simwe kukiwa na shida muhimu. Piga simu mara mojamoja tu kujua wanaendeleaje basi.
Ntauzingatia ushaur wako mkuu[emoji120]
 
Bro kukutoa hofu ni kwamba huyo jamaa yenu amesha wadinyia wake zenu kubalini kataeeni huo ndio ukweli na Kama haja mdinya mkeo Basi mkeo ni mbaya Sana Hana mvuto....poleni na rafiki yenu jamaaa
 
Back
Top Bottom