Jamaa anamuoa mchumba wa rafiki yake kama mke wa pili

Jamaa anamuoa mchumba wa rafiki yake kama mke wa pili

Siwezi kuroga kwa sababu ya mwanamke. Roga km mtu kaiba gari yako au hela ila siyo mwanamke. Huyo dogo inabidi afanye sherehe ndogo ya kujipongeza maana angemuoa J angejikuta amepata watoto 3 na wote wa huyo brother wake. Nina ushahidi
Usemalo Lina ukweli kabisa, Hawa hawakuanza hivi karibun..

Huenda kulkua namahusiano ya Siri yanaendlea hapa katkat
 
Mpuuzi mpuuzi TU,
sijajua uko kwenye uke wenza kafuata nini.

Na sijui Ni Nani alimshaur kua uke wenza atafurahia maisha
Hana muda huyo atapigwa tukio atarudi...muda utaongea. Kuna muda wanawake tunazingua sana.
 
Mimi nakuaminia mzee wangu

We sio mtu wa mchezo mchezo pia uko deep kwenye ile tasnia pendwa [emoji2]

Kwa leo tuishia hapo

Kama vipi mchukueni dogo nendeni Zanzibar au bagamoyo akaubwage moyo

Badilisheni mazingira
Ntalifanyia kazi mkuu,[emoji120]
 
Kwa hapa huyo Dada hakumpenda huyo kaka sema kwa kua walikua mbali mbali ndo maana hakua anajaua tabia za msichana wake! Aachane nae itamkosti
Kabisa mkuu, kUna la kujifunza hapa
 
Bro kukutoa hofu ni kwamba huyo jamaa yenu amesha wadinyia wake zenu kubalini kataeeni huo ndio ukweli na Kama haja mdinya mkeo Basi mkeo ni mbaya Sana Hana mvuto....poleni na rafiki yenu jamaaa
Asante mkuu,
Hilo kwa MKE wangu SIDHANI ila sio vibaya umenipa tahadhari,

Shukran Sana ila ntalifanyia uchunguzi ilo suala.
 
Update....
Ni kwamba mwanamke alinyang'anywa simu ya awali alokua anatumia na kapewa simu mpya yenye line mpya ya Airtel.

Nmefanikiwa kuipata hio namba na nmempigia na kuongea mwanamke mwenyewe.

Anasema,
"Shem mi sio kwamba simpendi rafiki ako, nampenda sana na nilitamani awe mme wangu. Sema rafiki ako hakua serious na Mimi. Miaka 4 yote tangu ameleta barua hamna kinachoendelea. Familia inanisumbua Sana afu nikimwambia hataki kunielewa anadai mpaka amalizie nyumba yake. Nyumba imeisha anadai finishing bado. Hivi kweli shemej nyumbA inaweza mzuia mtu wasifunge Ndoa? Hivi kweli anachonifanyia mwenzako unaona Ni sahii."

Nikamjibu,
"Kwaiyo meji ukaona Njia rahisi Ni kuolewa TU na rafki yake, hujui itamuumiza Kias gani?"

Akasema,
"Shemej nikwambie TU ukweli, uyu B tangu mwanzoni ashaonesha ananipenda Sana. Afu tangu zaman keshaonesha Nia ya kunioa MDA mrefu. Sema Mimi TU ndo nilikua kikwazo, afu kingine uyu B anakubalika Sana uku nyumban.

Shemej presha kwa familia yangu kuhusu B Ni kubwa Sana, Baba na mama na dada zangu wote wanataka niolewe na B. Imefkia mpaka mama ananambia uyu alonichumbia Ni mhuni TU miaka 4 Ni uchumba sugu huo. Imefkia mpaka baba haniongeleshi kisa sitak kuolewa na B. Na wote washanambia nisipoolewa B Mimi sitokua mwanao Tena na watanifuta kwenye ukoo.

Shemej yang mi mwenywe Niko Njia panda apa, moyoni mwangu B hayupo kabisa ila nalazimishwa TU na familia yangu. Uto rafiki yako hawamtaki kabisa ata kumskia uku nyumbani."

Nikamwambia,
"Kwaiyo shemej uko serious kabisa umelazimishwa Hii ndoa?"

Akasema
"Ndio Shem, yaan naomba TU uniombee msamaha TU kwa rafk yako. Mi bado nampenda Sana."

Nikamwambia,
"Bas Shem naomba ufanye jion tuonane ata kwa jamaa tujue tunaliwekaje hili"

Akasema,
"Sawa, ila Mimi kwa jamaa siwez kuja tena.italeta balaa. Labda yeye ata aje kwako niwakute apo kwako"

Nikasema,
"Sawa"

Ninachowaza Sasa,
Kama ni kweli uyu mwanamke kalazimishwa. Na kweli ANAMPENDA jamaa.

Nawaza kumshauri rafiki yangu, ashirikiane na uyu mwanamke.
Kisha binti atoroshwe akawekwe mafichoni kwa sikU kadhaa Hadi ile harusi ilopangwa itakapopita.

Uyu B atakapomtafuta akakosa Basi Iyo Ndoa ya kulazimisha itakua imeota manyoya.

Afu Sasa uyo B aje kwetu kulalamika kwetu katoroshewa MKE, na sisi tuje tumuoneshe kua upumbavu hatutaki.

SIJUI KAMA NIKO SAHII AU LAH[emoji848]

ushauri wenu tafadhali
Hata msihangaike na yote hayo binti wala hana upendo anaosema angekuwa real asingefika hatua ya kuolewa na huyo jamaa hapo anawazuga tu,kubwa endeleeni kumshauri huyo dogo na kumpa maneno ya faraja is the matter of time atakuwa sawa tu.
 
Asante mkuu,
Hilo kwa MKE wangu SIDHANI ila sio vibaya umenipa tahadhari,

Shukran Sana ila ntalifanyia uchunguzi ilo suala.
uchunguze ili iweje.

cha kufanya just cut off the guy muendelee na maisha yenu.

Usitake kuja kuharibu ndoa yako kisa kuchunguza yasiyokuwepo.

Trust your woman, not all women are hoes.
 
Ninavyohis mimi hao walianza mahusiano walipokutanishwa tu inaonesha wana muda ktk mahusiano mpk kufikia kutaka kuoana ,na mshaur rafik yako asimng’ang’anie huyo binti akubali tu matokeo amuache kbs alie avumilie maumivu anayopitia ila ipo siku yatakwisha kwanza bint anaenda kwenye ndoa yenye changamoto ya wawili atammkumbuka jamaa na atamkuta jamaa tayar ana mke wake tena wanapendana avumilie tu hiki kipind cha mpito
 
Back
Top Bottom