Jamaa kaliwa Tshs. 3,000,000 kwenye kamari, yupo hoi kitandani

Jamaa kaliwa Tshs. 3,000,000 kwenye kamari, yupo hoi kitandani

Mimi nabet sana huwa naona raha kubet kila weekend natenga 20,000 za bia na 10,000 ya kubeti ikipigwa hiyo 10,000 sibet tena mpaka wiki ijayo lakini nashukuru mungu mtaji wangu wa kubeti ni kama 90,000 na muda wa kama miezi miwili sijaweka hela yoyote jana liverpool iliniongezea mtaji wangu.

Nashauri tusibet kwa malengo ya kupata kipato, bali iwe kama mchezo game.
[emoji120][emoji120]
 
Kamari haimwachi mtu salama....kwanza kubeti ni haram lakini watu wabishi na hawataki kusikia...mimi simpi pole kwenye upuuzi kama huu ambao Mwenyezi Mungu anaupiga vita....
Haramu!? kwani kakwambia alienda kubetia kanisani/msikitini?
 
Teh,yaan stake mil 6 halaf inaliwa unakuwa normal
Katika betting Kuliwa ni jambo LA kawaida sana.

Na unalazimika ulizoee.

Kiuhalisia,
Betting ni vita ya kiuchumi baina yako na Muhindi au Mrusi.

Ni kama ulivo mchezo wa kupokezana vijiti,

Leo kuliwa zamu yako, Kesho itakua ZAmU ya Muhindi/mrusi

Pia
Ukijiona unabet unakula tu, halafu hata hauliwi.
Jua kua sio bure, wewe ni lazima Utakua unamatatizo.
 
Kwenye kamari cheza kile ambacho hutajuta kukipoteza! we chezea ada za shule za watoto, kodi ya nyumba, mtaji wako ahayo matokeo yake
 
Binafsi;
Niliwahi kuliwa Million 6 kwenye mkeka mmoja na sikupata presha.

Nlicheza mechi 2 tu, nkawapa ushindi Bayern na PSG wote walikua wanacheza nyumbani.

Bayern alishinda ila PSG alitoa sare, mikeka ukachanika.

{Wazee wenzangu kule kwenye Uzi wa mikeka ni mashahidi kwenye hili}

Nilitulia, Nikarelax na Nikaendeleza Mapambano.

Baada ya wiki 1,
Namaanisha wiki ilofuata nilimpiga muhindi million 18.

Na mapambano Bado yanaendelea.
Duuh! we jamaa mtaji wako sh. Ngap? Kampuni gan unabetia?
 
alikosa hata wa kumsukia mkeka??! iwe fundisho na kwa wengine
 
Ndo uanaume huo maana hakuna biashara ya chapu ya kukuingizia kipato cha juu kwa wakati mfupi zaidi ya betting isipokuwa ukienda kichwa kichwa ndo inakuwa majonzi mazito
 
Back
Top Bottom