Jamaa kamuoa dada yake!

Jamaa kamuoa dada yake!

Mkeshaji

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2011
Posts
4,258
Reaction score
1,416
Habari zenu bandugu.
Hiki ni kisa cha kweli kabisa ambacho nimekishuhudia na ninaendelea kukishuhudia:
Ninaye jamaa yangu mmoja hivi, yeye amemuoa binamu yake yaani mtoto wa shangazi yake kabisa na hadi sasa wana watoto watatu.
Baba yake huyo jamaa yangu na mama wa huyo binti (aliyemuoa) wanazaliwa na baba mmoja na mama mmoja.

Kwangu mimi ilinistua sana nilipogundua hii kitu kwani naona kuwa hao ni mtu na dada yake wa damu kabisa.
Niliwahi kusikia kuwa kuna baadhi ya makabila na hata dini zinaruhusu ndoa katika mahusiano ya undugu wa karibu namna hiyo, lakini nilidhani kuwa haya mambo yalifanyika zamani sana (kwa sababu zao wakati huo) na sikutegemea kama yanaweza kufanywa na kizazi cha sasa.

Niliwahi kupata mafundisho kuhusu ndoa. Katika dini yetu pale inapobidi, ndoa za kindugu zinaruhusiwa lakini kuanzia kizazi cha tano yaani kama kwa upande wa shangazi na mjomba wanaoweza kuoana ni kuanzia vitukuu vyao kwani hawa hata ule undugu unakuwa umeachwa mbali sana lakini siyo kama huyu jamaa yangu na dada yake kwani hiki ni kizazi cha pili tu.

Mtiririko upo hivi:
Babu/Bibi
Baba/Mama
Mwana
Mjukuu
Kijukuu
Kitukuu
Kilembwe
Kining'ina

Je kwa mila na desturi za kitanzania (makabila na dini), zamani na sasa hii kitu ni sahihi?
Je ina athari yoyote katika jamii husika?
Karibuni.
 
Hakuna problem kabisa, as long hamkutoka tumbo moja au hamjachangia baba mmoja.
 
KUna nyingine toka Zimbabwe nimesoma jana... Mama kajazwa mimba na mwanaye wa kumzaa. walianza mapenzi baada ya mume kufariki na kwa kuwa mama hakutaka kuolewa na ndugu wa marehemu mumewe kama tamaduni zao zinavyotaka, akaamua kumgawia mwanawe na sasa ni mjamzito na wana mpango wa kufunga ndoa
 
Extraordinary!
 
Mbona hii hata kwa wakerewe ni kawaida tu? Binamu ni mke halali kabisa - undugu usipotee.
 
Hapo anagekuwa mwarabu, watu wangeshika Wireless Microphone Speaker :biggrin:

Hata ukiwambia mimi nikiziwi...Watasema lazima usikie tu mzee, watakununlia Ear hearing speakers ili usikie utake usitake.
 
Mbona hii hata kwa wakerewe ni kawaida tu? Binamu ni mke halali kabisa - undugu usipotee.

Kuna kisa kingine cha kweli kabisa kutoka koo za maeneo hayo uliyoyataja, jamaa alioa mke wake wa kwanza baada ya kuona kuwa hawajajaaliwa mtoto na huyo mkewe basi jamaa ikabidi atafute mke wa pili kwa minajili ya kupata mtoto. Kwa kushirikiana na mkewe pamoja na ukoo wake jamaa akamuoa mdogo wa mkewe, baba mmoja mama mmoja na ndiye aliyezaa naye. Lakini hawa wamama/mtu na dada/wake wenza walikuwa wakiishi pamoja na huyo mume wao/shemeji yao.

Wengine ni majirani zangu pale home. Mume alifariki, ndugu wakamlazimisha yule mjane aolewe na kaka yake jamaa kwani jamaa alikuwa na mawe ile mbaya kwa hiyo hawakupenda mali yao ipotee, hadi sasa mjane yupo na shemeji yake. Na huyu dada ni kijana tu wa miaka ya 30 hivi na siyo mbumbumbu.
 
Aarg!Mi nilifikiri dada kumbe binam!Binam nyama ya ham,au we hujui?
 
Kuna kisa kingine cha kweli kabisa kutoka koo za maeneo hayo uliyoyataja, jamaa alioa mke wake wa kwanza baada ya kuona kuwa hawajajaaliwa mtoto na huyo mkewe basi jamaa ikabidi atafute mke wa pili kwa minajili ya kupata mtoto. Kwa kushirikiana na mkewe pamoja na ukoo wake jamaa akamuoa mdogo wa mkewe, baba mmoja mama mmoja na ndiye aliyezaa naye. Lakini hawa wamama/mtu na dada/wake wenza walikuwa wakiishi pamoja na huyo mume wao/shemeji yao.
Hao wamekuwa wanyama tena sio bina-adamu.

Angekuwa huyo mwanamke kafa inawezekana lakni yuko hai, na mme wake anao mdogo wake....Aisay hii kali.
 
kwa hiyo na wewe unaweza kuoana na mtoto wa uncle wako.
Aisay naoa kabisa....Sioni kosa hapo.

Na anaye sema kuna kosa siatakuwa mjinga aniletee vitabu vya Mungu wapi mungu kasema kosa...Hivi nyie bin-adamu mnajiona mna akili kuliko Mungu!!

Kama kungekuwa na kosa si Mungu angeisha sema zamani....
since theres no where in the Qur'am or Bible that forbids...Wacha vijana wachangamkie watoto wa uncle zao.

Msilete sababu ya genetic and heriditary problems for your children....Wengine wakaogopa lakini sioni reason ya aina yoyote ukioa mtoto wa uncle yako mtoto atazaliwa ana problems...Mana kila kukicha naona watu wanaona vile, mtoto wa mjomba anaoa wa shangazi...na mtoto wa mamkubwa anao wa mamdogo...Sijasikia wamepata heriditary problems.

Mtoto kuzaliwa na health problems ni Amri ya Mungu c sababu zingine, Mungu tu, ndo kataka azaliwe vile.
 
Back
Top Bottom