Habari zenu bandugu.
Hiki ni kisa cha kweli kabisa ambacho nimekishuhudia na ninaendelea kukishuhudia:
Ninaye jamaa yangu mmoja hivi, yeye amemuoa binamu yake yaani mtoto wa shangazi yake kabisa na hadi sasa wana watoto watatu.
Baba yake huyo jamaa yangu na mama wa huyo binti (aliyemuoa) wanazaliwa na baba mmoja na mama mmoja.
Kwangu mimi ilinistua sana nilipogundua hii kitu kwani naona kuwa hao ni mtu na dada yake wa damu kabisa.
Niliwahi kusikia kuwa kuna baadhi ya makabila na hata dini zinaruhusu ndoa katika mahusiano ya undugu wa karibu namna hiyo, lakini nilidhani kuwa haya mambo yalifanyika zamani sana (kwa sababu zao wakati huo) na sikutegemea kama yanaweza kufanywa na kizazi cha sasa.
Niliwahi kupata mafundisho kuhusu ndoa. Katika dini yetu pale inapobidi, ndoa za kindugu zinaruhusiwa lakini kuanzia kizazi cha tano yaani kama kwa upande wa shangazi na mjomba wanaoweza kuoana ni kuanzia vitukuu vyao kwani hawa hata ule undugu unakuwa umeachwa mbali sana lakini siyo kama huyu jamaa yangu na dada yake kwani hiki ni kizazi cha pili tu.
Mtiririko upo hivi:
Babu/Bibi
Baba/Mama
Mwana
Mjukuu
Kijukuu
Kitukuu
Kilembwe
Kining'ina
Je kwa mila na desturi za kitanzania (makabila na dini), zamani na sasa hii kitu ni sahihi?
Je ina athari yoyote katika jamii husika?
Karibuni.