Jamaa kaniwahi kuingiza vocha yangu, hadi tumepigana

Jamaa kaniwahi kuingiza vocha yangu, hadi tumepigana

The dumb Professor

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2023
Posts
852
Reaction score
1,978
Leo nipo zangu kwenye daladala na kavocha kangu ka 500 nimeshakwangua tayari kwa kuingiza.

Wakati naingiza nilikuwa nahangaika maana kioo changu hakitachi vizuri. Jamaa wa jirani akawa anainakili fasta na kaiingiza. ilipokataa nikamdaka fasta meseji imeingia.

Kwakifupi tumepigana, nimemng'oa jino mpaka daladala ikasimamishwa na tukashushwa kwa nguvu.

Sasa nimemkariri nina mpango wa kumfikisha mahakamani kwa kosa la wizi.

Mawakili wasomi hii kesi imekaaje?
 
Screenshot_2025-01-13-09-13-24-275_com.android.chrome.jpg
 
Hichi kituko kimewahi kufanywa na jamaa yetu mmoja. Tulikuwa tunasafiri ndani ya basi abiria mmoja alilinunua vocha. Ile amekwangua na kuanza kuingiza namba jamaa yetu aliziingiza chapchapu kwenye simu yake. Abiria anashangaa kujibiwa vocha imetumika. Karudiarudia jibu likawa ni lilelile ikabidi amshutukie jamaa yetu aliyekaa siti ya nyuma yake kuwa kaingiza namba hizo. Simu iliyoingiza namba hizo ikapigwa jamaa akaumbuka kesi ikaenda kumalizwa polisi
 
Back
Top Bottom