Last week Kuna harusi moja, niliitafuta clip yake nikaipata.
Bwana harusi amewatambulisha ex wake ukumbini, lakini aliwaomba wasisimame, hi inaonesha aliwaharika kwenye sherehe.
Bwana harusi huyo alimuuliza mke wake(Bibi harusi) Kama atakuwa amemkwanza lakini alisema hapana,
Kitu hiki kiliwafanya watu waanze kuwa na wasiwasi kama Bwana harusi ndani ya ndoa atakuwa mwaminifu, watu wanaona Kama Bibi harusi atashuhudia mengi ndani ya ndoa. Ila jamaa alikuwa hana wasiwasi kabisa.
Hivi Ni sahihi kweli kuwatambulisha ex wako ukumbini?
Naona wengi wanatoa povu.
Lakini swali la kujiuliza huyo mwanaume alikuwa hajawahi kuwa na mahusiano? Kama jibu ni hapana, je angekuwa na watoto akawatambulisha wao na wazazi wao, ingekuwaje?
Mi nadhani cha muhimu ni hisia za mtu na upendo wa dhati. Mambo mengine ni drama tu!