Wewe pia uelewa wako kuhusu vipimo vya ukimwi na ukimwi ni zero.
Vipimo vinaanza kuonyesha kuanzia siku ya 10 hadi 90 baada ya maambukizi sio kwamba virusi wanaanza kuonekana baada ya siku 90, huo ni uongo. Hiyo elimu yako ya ukimwi utakua umeipata vichakani.
Rudi shule ujifunze kuhusu vipimo vya ukimwi vinavyofanya kazi.
PCR inaonyesha kuanzia siku 10 hadi 33.
Rapid test za fourth generation kama ELISA zinaonyesha kuanzia siku 21 hadi 44, hii ni combo ya antibody na antigen. Wataalam wengi siku hizi wanatoa conclusive result kwa ELISA ndani ya siku 50.
Rapid za antibody za third and second generation kama hizi za Bioline/unigold zinaonyesha maambukizi ya kati ya siku 21 hadi 90.
Hizo ni general guidelines za WHO, CDC na taasisi nyingi za Afya Duniani. Ndio maana window period maximum imewekwa siku 90 kwamba 99.9% wa watu wataonyesha reaction ndani ya huo muda.
Kusema virusi vinaonekana baada ya siku 90 unaonyesha kabisa una elimu finyu kuhusu Ukimwi.