Jamaa yangu ana pass Degree lakini tayari kapata kitengo

Jamaa yangu ana pass Degree lakini tayari kapata kitengo

kyanyangwe

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2018
Posts
1,275
Reaction score
3,316
Kuna jamaa yangu tumepiga nae shule, yeye alikua sio mtu wa ile misuli mirefu,kapata pass degree grade.ila cha kufurahisha ni kwamba jamaa tayari kalamba mkataba kwenye kampuni kubwa tu linalojihusisha na utengenezaji na usambazaji wa cement hapo mjini Daslamu.
Binafsi zamani nilikuwa najua mtu akimaliza chuo na pass degree,basi sehemu pekee anayoweza kupata kazi ni serikalini tu,kumbe mambo sivyo.

Mapambano yaendelee job seekers wenzangu.
 
Ingekuwa kufaulu sana ndiyo kuwa na bahati basi wenye PhD wangekuwa mbali sana.

Maisha yana siri nyingi tusizozijua, wakati wewe ukilalamika kitu fulani, kwa mwenzio kinaweza kuwa kitu cha kawaida kabisaaa.

Yani wewe unaweza usiweze kushindia mkate, lakini kwa mwingine mkate akauona kama bonge la menu.

Unforgettable
 
Kwani vigezo vinasemaje ? Usiwe na Pass Degree ?

Achana na Pass hata mtu anaweza asiwe na degree bado akapata kazi na wewe mwenye degree Ukakosa (huenda kuna vitu mwajiri anaviangalia ambavyo wewe hauna)
JK mwenyewe alikuaga na Gentleman na akawa the boss,huku wenye 1st class zao wakimlamba miguu.

That's life.
 
Kuna jamaa yangu tumepiga nae shule, yeye alikua sio mtu wa ile misuli mirefu,kapata pass degree grade.ila cha kufurahisha ni kwamba jamaa tayari kalamba mkataba kwenye kampuni kubwa tu linalojihusisha na utengenezaji na usambazaji wa cement hapo mjini Daslamu.
Binafsi zamani nilikua najua mtu akimaliza chuo na pass degree,basi sehemu pekee anayoweza kupata kazi ni serikalini tu,kumbe mambo sivyo.
Mapambano yaendelee job seekers wenzangu.
Labda ingekuwa kufundisha vyuoni. Huku tuaangalia mtu anajimudu kiasi gani? Karatasi za vyeti zinakusaidia kuwa na absolute minimum requirements tu unapoomba kazi.
 
Ninyi wenye ma upper second na kuendelea subirini kazi za viyoyozi...
 
unadhani kusoma sana ndio kupata kazi sana ee? amka ndotoni wewe
 
It doesn't matter what you know, but whom you know, maisha ni zaidi ya GPA kubwa na waliotoboa wengi Wana GPA ndogo tu mkuu. So tafta connection
 
Unaweza kusoma Sana ukafulia, ya juzjuz walioingizwa majeshini, form four wenye fani za ufund wa veta, wasomi wamelamba lolo.
 
Huo ujinga upo Tanzania tu, lakini huko Nje bila GPA kubwa, ufaulu mzuri hutoboi kizembe, haki ya mtu haiibwi, siwezi kutumia mtu mwenye ufaulu mdogo kwenye ofisi zangu.
Nje ipi umeishi wewe?
Tupe mfano mmoja wa aliyekua na pass degree huko nje unakokusema then akashindwa kutoboa.
 
CONNECTION ina nguvu sana kwenye ajira kuliko GPA kubwa
 
Back
Top Bottom