Jamaa yangu ananuka mdomo sana. Nitumie njia gani kumfikishia ujumbe?

Jamaa yangu ananuka mdomo sana. Nitumie njia gani kumfikishia ujumbe?

DOTHRAK

Member
Joined
May 22, 2021
Posts
15
Reaction score
154
Habari!

Ni mshkaji niliefahamiana nae mwaka jana na tuna miezi kama tisa kwenye urafiki, ila mdomo wake unatoa harufu mbaya tukiwa katika katika mazungumzo. Sijajua shida ni hapigi mswaki vizuri, huwa hapigi mswaki kabisa au anapiga kwa matukio.

Hii hali nilikuwa najitahid kuivumilia kwa kumkwepe kwepa akinielekezea mdomo lakini leo katika story za hapa na pale kuhusu mwenendo wa UEFA naona harufu imekuwa kali zaidi ikabid nipunguze stor ili maongezi yasiwe mengi sana.

Hali kama hizi huwa mnapambana nazo vipi? Maana naona aibu kumwambia ila natamani sana awe na kinywa kisicho na harufu, isitoshe sisi bado ni vijana kabisa.

Naomba Ushauri wenu wakuu.

Natanguliza shukrani.
 
Hali tatizo la kunuka midomo linazidi kuwa kubwa si kwa vijana wala wazee, nadhani na ongezeko la watu wanaotumia vilevi bila utaratibu maalimu kama ugoro, viroba n.k

Sasa huyo jamaa yako huenda nayeye yupo humo, kama vipi mwambie kwa utani utani huku unapiga mshono.
 
Nunua hydrogen peroxide au nenda duka la dawa waambie unataka dawa kwa ajili ya mtu anayenuka mdomo inauzwa 1500 mpe mwambie sukutua na hii Karla hunapiga mswaki mdomo una harufu mbaya me mke want Kuna kipindi ilitokea hivyo nkamnunulia dawa na nikamchana alifurahi hakumind
 
Kimbembe ni kwa mke wake kama anae, raia kama hao alale usiku mzima kabunda afu ile alfajiri aanze kuongea, wanawake mnavumilia mengi aiseeh [emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Habari!

Ni mshkaji niliefahamiana nae mwaka jana na tuna miezi kama tisa kwenye urafiki , ila mdomo wake unatoa harufu mbaya tukiwa katika katika mazungumzo. Sijajua shida ni hapigi mswaki vizuri, huwa hapigi mswaki kabisa au anapiga kwa matukio. Hii hali nilikuwa najitahid kuivumilia kwa kumkwepe kwepa akinielekezea mdomo lakini leo katika story za hapa na pale kuhusu mwenendo wa UEFA naona harufu imekuwa kali zaidi ikabid nipunguze stor ili maongezi yasiwe mengi sana.
Hali kama hizi huwa mnapambana nazo vipi? Maana naona aibu kumwambia ila natamani sana awe na kinywa kisicho na harufu, isitoshe sisi bado ni vijana kabisa.
Naomba Ushauri wenu wakuu.

Natanguliza shukrani.
Wakati mwingine hiyo hutokana na maambukizi ya kinywa na sio kutopiga mswaki....Jifanye umeamua kumpa somo la kinywa na kwamba ww pia uliwahi kupata tatizo hilo sema ukalitatua kwa matibabu ya hospitali na ushauri wa kupiga Mswaki at least twice a day naye afanye hivyo
 
Halafu nimegundua watu bado wana uelewa mdogo na hili tatizo, hili tatizo mara nyingi huwa ni la kiafya zaidi na wala si upigaji mswaki. walio wengi wanapiga mswaki vyema tu ila tatizo bado lipo pale pale.
 
Habari!

Ni mshkaji niliefahamiana nae mwaka jana na tuna miezi kama tisa kwenye urafiki, ila mdomo wake unatoa harufu mbaya tukiwa katika katika mazungumzo. Sijajua shida ni hapigi mswaki vizuri, huwa hapigi mswaki kabisa au anapiga kwa matukio.

Hii hali nilikuwa najitahid kuivumilia kwa kumkwepe kwepa akinielekezea mdomo lakini leo katika story za hapa na pale kuhusu mwenendo wa UEFA naona harufu imekuwa kali zaidi ikabid nipunguze stor ili maongezi yasiwe mengi sana.

Hali kama hizi huwa mnapambana nazo vipi? Maana naona aibu kumwambia ila natamani sana awe na kinywa kisicho na harufu, isitoshe sisi bado ni vijana kabisa.

Naomba Ushauri wenu wakuu.

Natanguliza shukrani.
Nilipata kuwa na rafiki kama huyo, ilikuwa ni changamoto sana wakati wa kupiga story hasa wakati wa kazi za pamoja maana tulikuwa tunafanya kazi ofisi Moja.

Nilichofanya ni kwenda hosp moja wana deal na vinywa na meno maeneo ya Philips Arusha nikamweleza Dr akanambia ni vema niende nae pale.... what i dd, nikamwambia kesho yake anisindikize nina tatizo la jino so kwa kuwa tulikuwa tayar tumepanga na Dr. tulipofika pale mi niliingia nikachekiwa kwa kuzuga nilipotoka nikamwambia Dr akamwambia Hello njoo na weee tukuchek bana unajua ugonjwa sio lazima uje ukishidwa kutembea......Nashukuru jamaa alipata tiba na hadi sasa ni mzima hatoi ile fumes mbaya yoyote tena! Baadae nikimweleza what i dd nalifurahi sana na alikiri ni jambo lilikuwa linamtatiza maana madogo walikuwa wanamweleza live anapoongea nao.

Kama upo na nia njema ya kumsaidia jaribu njia hiyo nasikia tatizo lipogo kwenye mfumo wa kinywa kwa ujumla wake na lipo ndani sio suala la kupiga mswaki pekee!!
 
Usimwambie kwa kiswahili kuwa UNANUKA MDOMO. Atajisikia vibaya mwambie kwa Kiingereza kuwa UNA BAD SMELL (wala usitumie neno bad breath) hapo hataku mind atatabasamu tu na kukwambia ok.... "Unajua leo nlikuwa nmefunga ndo maana"
 
Nunua hydrogen peroxide au nenda duka la dawa waambie unataka dawa kwa ajili ya mtu anayenuka mdomo inauzwa 1500 mpe mwambie sukutua na hii Karla hunapiga mswaki mdomo una harufu mbaya me mke want Kuna kipindi ilitokea hivyo nkamnunulia dawa na nikamchana alifurahi hakumind
Hii dawa nzuri, nimeshaitumia Mara kadhaa kwa watu wangu wa karibu na imewasaidia.
 
Dah wanawake wanakutana na vingi sana kiongozi imagine mwanaume kachanhanya ugoro, pombe ya matapu tapu na sigara tumbaku juu hiyo harufu sio ya kawaida.
Jana jioni nipo Uyole nasubiri private yoyote, kaja mpiga debe ananiuliza "unaenda wapi jombaa" daaah hiyo harufu nilitamani kutapika.
 
Mpenyezee kimemo chini ya mlango wake bila kukuona, mwambie piga mswaki vizuri mdomo wako unanuka sana
Sio kesi ya mswaki kunawatu midomo yao hunuka hata apige mswaki linatokana na nn labda awaone wataalamu wa kinywa
 
Back
Top Bottom