Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Kaka Jamal Malinzi na timu yako ya uongozi hapo TFF, umefika muda wenu wa kuachia ngazi. Timu ya Taifa inaendelea kuboronga na kuendelea kulitia aibu taifa. Ni jana tu Taifa Stars imebamizwa mabao 3-0 na Mafarao (Misri).
Timu ya Taifa haifanyi vyema kweye mashindano yoyote ya kimataifa. Kimsingi, hakuna mafanikio yoyote ya uongozi wa TFF kujivuna juu ya soka la nchi hii. Kwenye viwango vya FIFA Tanzania inaporomoka kila kukicha.
Kaka yangu Jamal Malinzi, mafanikio ya kisoka katika taifa lolote si ligi, ni timu ya taifa. Msijivune lolote juu ya ligi huku timu ya taifa ikiboronga. Wakati umefika kwa nyinyi kukubali kuwa mmeshindwa na kuachia ngazi. Hata kocha wa timu ya Taifa anapaswa kuwajibika au kuwajibishwa. Ikibidi hata timu ya Taifa ifumuliwe na kusukwa upya.
Nikiwa kama mtanzania mpenda soka, natoa rai kwenu kuwajibika.
Msingoje kuondolewa kwa aibu!