Jamal Malinzi na wenzako, kwanini msiachie ngazi? Acheni ung'ang'anizi usio na msingi

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Kaka Jamal Malinzi na timu yako ya uongozi hapo TFF, umefika muda wenu wa kuachia ngazi. Timu ya Taifa inaendelea kuboronga na kuendelea kulitia aibu taifa. Ni jana tu Taifa Stars imebamizwa mabao 3-0 na Mafarao (Misri).

Timu ya Taifa haifanyi vyema kweye mashindano yoyote ya kimataifa. Kimsingi, hakuna mafanikio yoyote ya uongozi wa TFF kujivuna juu ya soka la nchi hii. Kwenye viwango vya FIFA Tanzania inaporomoka kila kukicha.

Kaka yangu Jamal Malinzi, mafanikio ya kisoka katika taifa lolote si ligi, ni timu ya taifa. Msijivune lolote juu ya ligi huku timu ya taifa ikiboronga. Wakati umefika kwa nyinyi kukubali kuwa mmeshindwa na kuachia ngazi. Hata kocha wa timu ya Taifa anapaswa kuwajibika au kuwajibishwa. Ikibidi hata timu ya Taifa ifumuliwe na kusukwa upya.

Nikiwa kama mtanzania mpenda soka, natoa rai kwenu kuwajibika.

Msingoje kuondolewa kwa aibu!
 
mi siafiki jamal malinzi kujiudhuru kwani hakuna tz anayeweza kuipeleka stars afcon wala world cup
 
Hhaahahha...kwa hio unaamini watu milioni 45 malinzi ndio mwenye uwezo peke yake?

By the way ukiwa na kumbukumbu zako sawa...Ni wakati huu wa malinzi ndio timu imekosa uhai zaidi

Kocha wa Malinzi...Mart Nooj tangu ameingia pamoja na malinzi ameshinda mechi tatu tu kati ya Mechi 17 za kimataifa ambazo stars imecheza.

Lazima achukue responsibility ya failure hii....Inatosha

This is enough
cc Jamal Malinzi
 
Tenga alionyesha uelekeo angalau, Jamal Malinzi anaturudisha nyuma kabisa, hata ule mwamko waashindano ya coca cola umekufa!
 
Tatizo tumeendekeza njaa katika uchaguzi malinzi sio mtu wa mpira kabisa bora kipindi cha tenga, badala ya kwenda mbele sie tunarudi nyuma, ona sasa 3😱'clock
 
Hhaahahha...kwa hio unaamini watu milioni 45 malinzi ndio mwenye uwezo peke yake?

By the way ukiwa na kumbukumbu zako sawa...Ni wakati huu wa malinzi ndio timu imekosa uhai zaidi

Kocha wa Malinzi...Mart Nooj tangu ameingia pamoja na malinzi ameshinda mechi tatu tu kati ya Mechi 17 za kimataifa ambazo stars imecheza.

Lazima achukue responsibility ya failure hii....Inatosha

This is enough
cc Jamal Malinzi
you get me wrong bro! nimesema kwa sasa hakuna mtu atakaye ipeleka taifa stars afcon wala wc, tenga, ndolanga, rage na wengineo kuanzia mwaka 90 hadi sasa wameipeleka wapi stars? hata malinzi hawezi
 
Nami nakuuliza,Unadhani watanzania Milioni 45 wako limited kwa tenga, ndolanga, rage na wengineo? Yaani wewe unadhani kati ya watanzania Mil 45 hakuna CEOs wazuri wa kuleta result nzuri kwenye mpira zaidi ya hawa uliowataja?
 
Tenga alionyesha uelekeo angalau, Jamal Malinzi anaturudisha nyuma kabisa, hata ule mwamko waashindano ya coca cola umekufa!
kuna vitu hamvielewi nyie watu, kipindi tenga anaingia madarakani karibia wapenda soka wote walikuwa wamechoshwa na utawala wa fat, tofauti kwa malinzi kwani watawala wa tff walitaka wamuweke mtu wao ndio maana hata kwenye kugombania walimuengua eti hana vigezo fifa ndio ikamuokoa malinzi agombee, sasa ile team iliyoshindwa na malinzi (TEAMNYAMLANI) ndio inaleta hujuma kwa uongozi wa sasa,
 
Tenga na Paulsein timu yetu ilikuwa na mwelekeo...Amekuja huyu mppuzzi wa kihaya Jamal Malinzi...hakuna lolote ni kutufanya sisi watanzania tuonekane maboga zaidi
 
kuna vitu hamvielewi nyie watu, kipindi tenga anaingia madarakani karibia wapenda soka wote walikuwa wamechoshwa na utawala wa fat, tofauti kwa malinzi kwani watawala wa tff walitaka wamuweke mtu wao ndio maana hata kwenye kugombania walimuengua eti hana vigezo fifa ndio ikamuokoa malinzi agombee, sasa ile team iliyoshindwa na malinzi (TEAMNYAMLANI) ndio inaleta hujuma kwa uongozi wa sasa,

hebu acha kuongea vitu bila kujielewa bana

Eti anafanyiwa hujuma?

Anafanyiwa hujuma kivipi?

Onesha fact........

Watu tunaona timu inaboronga alafu wewe unaleta stori za uchaguzi hapa
 
watu tuliopitia utapiamlo wakati tupo watoto mnataka tuwapeleke afcon na wc? maajabu hayataisha
 
Malinzi ajitoetu sijaona alilofanya...tanzania kushiriki rasmi afcon itakuwa 2080
 
Acheni kumlaumu malinzi hata aje morinho hapa kuja kufundisha mpira hatufiki popote .Tanzania wachezaji wapo wazuri kwani wapo wanaocheza nje ya nchi .mfano.tp mazembe ,uarabuni.asia wapo wachezaji wengi wazuri wa kitanzania japo kuwa uzuri wao ni kwa ajili ya nchi zilizo na viwango duni kidunia ya mpira.
Tatizo Tanzania hatuna wachezaji wanaocheza uingereza.italy,spain na ulaya kwa ujumla.
 
kuna vitu hamvielewi nyie watu, kipindi tenga anaingia madarakani karibia wapenda soka wote walikuwa wamechoshwa na utawala wa fat, tofauti kwa malinzi kwani watawala wa tff walitaka wamuweke mtu wao ndio maana hata kwenye kugombania walimuengua eti hana vigezo fifa ndio ikamuokoa malinzi agombee, sasa ile team iliyoshindwa na malinzi (TEAMNYAMLANI) ndio inaleta hujuma kwa uongozi wa sasa,
Vyovyote vile, ukweli unabaki, Jamal Malinzi kaboronga, ilitakiwa aendelee na kuboresha alipoachia Tenga!
 
Acheni kumlaumu malinzi hata aje morinho hapa kuja kufundisha mpira hatufiki popote .Tanzania wachezaji wapo wazuri kwani wapo wanaocheza nje ya nchi .mfano.tp mazembe ,uarabuni.asia wapo wachezaji wengi wazuri wa kitanzania japo kuwa uzuri wao ni kwa ajili ya nchi zilizo na viwango duni kidunia ya mpira.
Tatizo Tanzania hatuna wachezaji wanaocheza uingereza.italy,spain na ulaya kwa ujumla.

Acha uongo wewe, Meximo na Poulsen tulikuwa tumewasha angalau indicator, tulikuwa tunacheza mpira unaona kabisa hapa tunahitaji kufanya kitu fulani ili kupanda daraja lingine, misingi ilowekwa na malinzi ni mibovu hivyo tunarudi nyuma!
Hao wachezaji wataenda vipi nje wakati misingi mibovu? angalau wakati wa Tenga, kina Samatta, ulimwengu, Kazimoto, yule wa Zesco ya zambia walitoka!
 
Vyovyote vile, ukweli unabaki, Jamal Malinzi kaboronga, ilitakiwa aendelee na kuboresha alipoachia Tenga!
ataboresha vipi wakati wafuasi wa aliyepita wameukosa urais na wanamtandao kuhujumu utawala wa sasa
 
Back
Top Bottom