Jamal Malinzi: Natukanwa sana JamiiForums, Facebook na redio mbali mbali

Jamal Malinzi: Natukanwa sana JamiiForums, Facebook na redio mbali mbali

Angewajibu kwa ile ID nyingine wale waliomtukana
angefungua tu hata id ya bishanga akatujibu...tulipomuunga mkono na kumsifia hakuita press na kutusifia lakini baada ya kuanza kumkosoa kahitisha press @JamaliMalizi jisafishe na tekeleza ahadi ulizoahidi wakati unagombea...
 
Attachments

  • 1456289294115.jpg
    1456289294115.jpg
    58 KB · Views: 20
Malinzi ki ukweli viatu vya TFF avikufai kabisa. Niliona Clip yake analalamika kuambiwa amepanga matokeo hivi alitaka wadau wamlalamikie nani? Kama si yeye mkuu wa chama cha Mpira nchini? Leo mzee Blatter ameachia ngazi FIFA kwa kutuhumiwa tu kwa rushwa sasa namshangaa Malizi.
..
 
Huyu malinzi anatafuta kichaka cha kujificha baada ya kupanga matokeo. Katukanmwa wapi? Ajibu kwanza maswali yetu hizo nyingine mbwembwe tu.
 
Ajiulize kwa nini Anatukanwa?? Huko kote kwenye social networks na media wanamuonea wivu??

Issue ni kuhusika kwenye sakata la upangaji matokeo!! Asitutolee mapovu!! Ajibu tuhuma.
Kwa nini mechi haikurekodiwa kama walivyokubaliana?
Akubali TCRA wapitie mawasiliano yake ya simu!
Taarifa ya kamisaa inasemaje? Kuhusu kipa we Geita kutoka uwanjani na kurudi bila kuadhibiwa!
Dakika kipindi cha pili zilichezwa ngapi?

Huyo Malinzi asijifanye mnafiki kwa kulalamika kuwa anatukanwa humu. Mbona wakati pia tulipokuwa tunamsifu humu humu jf alikuwa hatusifii sis wana JF? Tukisema tu jambo zuri kwake utaona anakuja humu na ile verified ID yake.

Ukiona unasemwa JF jua kwamba una matatizo hivyo jirekebishe.

Na labda kwa kumsaidia tu JF hii hii imeweza kuwa na impact kubwa sana katika nyanja mbalimbali za maisha ya watu na kiutendaji wa watu na inakubalika 100% na watanzania wote kuliko hata yeye anavyokubalika 2% tu ya watanzania wote.

Na najua fika kuwa jana pale katika ile press conference alienda akiwa na ID yangu ya Gentamycine kichwani mwake na ndiyo maana hata yule mtangazaji alipomuuliza tu swali la match fixing ya Tabora na Kigoma akafura sana.

Tena mwambieni kuwa akifanya mzaha tutasema na sakata la siri lililopo kati ya TFF na hao jamaa wa mataa Tazara ambalo nalo kama likifutuka mpira wa Tanzania utaingia katika kashfa kubwa mno.

Ajirekebishe upesi na tunamtaka aiombe radhi JF na wana JamiiForums wote kwani watu hatupo humu kupoteza muda bali tupo humu kufanya kazi ya kuirekebisha nchi na kuiweka sawa ambapo kama ukipatia tutakupongeza na ukikosea tutakupiga madongo vile vile.
 
Atuombe msamaha

Tena HARAKA Kama Siyo UPESI Mno Kwani ANAWEZA KUTUKASIRISHA Sasa TUKALISEMA LINGINE Ambalo Tukiliweka Humu Hatoamini Kuwa TUMELIPATA WAPI Na TUMELIJUAJE. Tunayajua Ya TFF Kuliko Hata Yeye Rais Wa TFF Anavyoijua TFF. Aiombe Radhi UPESI SANA JAMII FORUMS!
 
.
Mkuu unabania nini? funguka Mkuu...
 
Tena HARAKA Kama Siyo UPESI Mno Kwani ANAWEZA KUTUKASIRISHA Sasa TUKALISEMA LINGINE Ambalo Tukiliweka Humu Hatoamini Kuwa TUMELIPATA WAPI Na TUMELIJUAJE. Tunayajua Ya TFF Kuliko Hata Yeye Rais Wa TFF Anavyoijua TFF. Aiombe Radhi UPESI SANA JAMII FORUMS!
Natamani hilo ningekuwa nalijua Mimi kudadadeki nisingesubiri sijui aombe radhi sijui nini?yaani angeikuta mitandaoni siyo JF tu...
 
Natamani hilo ningekuwa nalijua Mimi kudadadeki nisingesubiri sijui aombe radhi sijui nini?yaani angeikuta mitandaoni siyo JF tu...

Namstahi Kwanza Kwakuwa Ni MTANI Wangu Wa KIHAYA Ila Akiendelea " KUNICHEFUA " Nitauweka Utani Wangu Na Yeye Pembeni Halafu Nitamwaga Kila Kitu " NIKINUKISHE " Hapo TFF.
 
Ajiulize kwa nini Anatukanwa?? Huko kote kwenye social networks na media wanamuonea wivu??
Issue ni kuhusika kwenye sakata la upangaji matokeo!! Asitutolee mapovu!! Ajibu tuhuma
Kwa nini mechi haikurekodiwa kama walivyokubaliana?
Akubali TCRA wapitie mawasiliano yake ya simu!
Taarifa ya kamisaa inasemaje? Kuhusu kipa we Geita kutoka uwanjani na kurudi bila kuadhibiwa!
Dakika kipindi cha pili zilichezwa ngapi?
Mimi ni mmojawapo ambaye baada tu ya kuchaguliwa nilimwambia waziwazi kupitia JF kwamba sivutiwi na uwezo wake na nikampa changamoto ya kunibadilisha mtizamo huo. Na mara kadhaa nimekuwa nikikumbushia hilo.

Lakini lazima tukubaliane kwamba kuna kukosoana na kuzodoana, kuambizana na kutukanana. Inaweza kuwa Malinzi amefanya makosa kwenye maamuzi au utendaji wake. Lakini huwezi kukosoa kosa kwa kufanya kosa (la kumtukana); kasoro mbili hazizai sahihi moja. Na kama nia ni kumkosoa na sio kumzodoa, hakuna haja na si uungwana - ni kinyume cha sheria kabisa - kumrushia matusi. Mara nyingi anayetukana anakusudia kuudhi na kudhalilisha. Sasa kumuudhi na kumdhalilisha kuongoza wa Juu wa TFF kutasaidiaje kufanikisha uongozi wa TFF na utendaji wa kiongozi mwenyewe?

Kama sio kwa nia ya kuudhi na kudhalilisha, matusi ni ushahidi usiowacha shaka kwamba aliyeyatoa ameishiwa hoja. Matusi ya aina hiyo mara nyingi mhusika huwa hamalizi kuyasoma, na hashawishiki kusoma maoni yajayo ya mtukanaji huyo hata yasipokuwa na matusi. Kwa hivyo nayo hayasaidii.
Licha ya kutoridhishwa naye, lakini lazima tukubali kwamba angalau ni muungwana. Alihusikaje na kuruhusiwa Azam kwenda Zambia kwenye Bonanza wakati yeye si kiongozi wa Bodi ya Ligi?

Na bado akakubali makosa. Mtu namna hiyo ndiye wa mwisho anayestahiki kutukanwa, kama matusi yangekubalika. Hoja yangu ya msingi ni kwamba wanaotukana Malinzi kwenye JF wanampa uhalali wa kutojibu hoja zao na - pamoja nao - hata za wasiomtukana.

Wanaikosea adabu JF na wanatuzindua kwamba hata wao wenyewe hawana busara za kuongoza. Kwa hivyo wao kumkosoa kiongozi ni sawa na chungu kulikosoa birika kwa weusi wake.
 
Mimi ni mmojawapo ambaye baada tu ya kuchaguliwa nilimwambia waziwazi kupitia JF kwamba sivutiwi na uwezo wake na nikampa changamoto ya kunibadilisha mtizamo huo. Na mara kadhaa nimekuwa nikikumbushia hilo. Lakini lazima tukubaliane kwamba kuna kukosoana na kuzodoana, kuambizana na kutukanana. Inaweza kuwa Malinzi amefanya makosa kwenye maamuzi au utendaji wake. Lakini huwezi kukosoa kosa kwa kufanya kosa (la kumtukana); kasoro mbili hazizai sahihi moja. Na kama nia ni kumkosoa na sio kumzodoa, hakuna haja na si uungwana - ni kinyume cha sheria kabisa - kumrushia matusi. Mara nyingi anayetukana anakusudia kuudhi na kudhalilisha. Sasa kumuudhi na kumdhalilisha kuongoza wa Juu wa TFF kutasaidiaje kufanikisha uongozi wa TFF na utendaji wa kiongozi mwenyewe? Kama sio kwa nia ya kuudhi na kudhalilisha, matusi ni ushahidi usiowacha shaka kwamba aliyeyatoa ameishiwa hoja. Matusi ya aina hiyo mara nyingi mhusika huwa hamalizi kuyasoma, na hashawishiki kusoma maoni yajayo ya mtukanaji huyo hata yasipokuwa na matusi. Kwa hivyo nayo hayasaidii.
Licha ya kutoridhishwa naye, lakini lazima tukubali kwamba angalau ni muungwana. Alihusikaje na kuruhusiwa Azam kwenda Zambia kwenye Bonanza wakati yeye si kiongozi wa Bodi ya Ligi? Na bado akakubali makosa. Mtu namna hiyo ndiye wa mwisho anayestahiki kutukanwa, kama matusi yangekubalika. Hoja yangu ya msingi ni kwamba wanaotukana Malinzi kwenye JF wanampa uhalali wa kutojibu hoja zao na - pamoja nao - hata za wasiomtukana. Wanaikosea adabu JF na wanatuzindua kwamba hata wao wenyewe hawana busara za kuongoza. Kwa hivyo wao kumkosoa kiongozi ni sawa na chungu kulikosoa birika kwa weusi wake.
Wewe ni mkongwe humu tusaidie kuonyesha hayo matusi anayotukanwa au waripoti wanao mtukana....
 
Wewe ni mkongwe humu tusaidie kuonyesha hayo matusi anayotukanwa au waripoti wanao mtukana....
Ni mengi. Ila kwa kawaida kukariri tusi ni kutukana pia. Lakini mtu anapodhalilisha kabila lako hadi ukoo wako kwa sababu tu wewe ni kiongozi uliyeamua kinyume na matarajio yake, utasema hajakutukana? Unapoanzisha uzi kwa hiari yako ili wadau wakuhoji, nao wakakuita majina na kukupa sifa za kudhalilisha (useless [[HASHTAG]#1104[/HASHTAG]], MAANDAZI [[HASHTAG]#1061[/HASHTAG]], Janga la Taifa [[HASHTAG]#1074[/HASHTAG]], Janga la Kimataifa [[HASHTAG]#1086[/HASHTAG]], mpuuzi ..... hovyo kabisa [[HASHTAG]#1090[/HASHTAG]]) na mengine zaidi ya hayo, utasema hujatukanwa?
 
Back
Top Bottom