GE2025 Jamal Rwambow: Askari ana Haki kukataa Amri Kinyume cha Sheria, hata ikitoka kwa mkubwa wake

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Aliyekua Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Jamal Rwambow ambaye kwa sasa ni mgombea Ubunge kupitia ACT Wazalendo, Jimbo la Mbagala amesema, “askari yeyote anayo haki ya kukataa kufuata maelekezo ya mtu yeyote hata kama ni mkubwa wake kama maelekezo hayo ni kinyume cha sheria.”

Niliwahi kuchangia humu, kuna watu wanadai polisi wanatekeleza amri tu, yanayoendelea na wao hawakubali ila hawana namna zaidi ya kutii amri, nikauliza ukiwa polisi ukaamlishwa umuue mzazi wako utamuua kwasababu unatii amri ? Kiufupi uwezo wetu wa kufikiri sawa sawa kama binadamu anayepaswa kutafakari na kuamua kwa busara ni mdogo. Watu wetu wengi walio kwenye hivi vyombo hawapishani sana na robots ambazo utashi wake unategemea anayeliongoza
 
Anaongea tu huyo

Kuna amri za kukataa na Kuna amri ambazo kamwe kuzikataa utasokotwa mno.

Mfano jana pale mahakamani amri zinatoka juu wafanye vile kwa hiyo pale huwezi kataa hata kwa dawa sababu wakubwa au wanasiasa wapo nyuma ya pazia
 
Uliwa

Hivi uliwahi kupita hata JKT?
Humu mtandaoni kila mtu ni mjuaji hata kwa,azichokijua.

Ndio maana askari huwa anapelekwa kufanya kazi mbali na kwao kwa sababu amri lazima itekekezwe.

Eti akipewa amri sio halali akatae hivi wewe unayepewa amri umepewa madaraka ya kutafsiri kuwa hii amri halali au la?

Hakuna askari atakayekataa amri kwani anajua kitakachomkuta. Inatakiwa utekeleze kwqnza halafu baadae utalalamika na kusikilizwa lakini sio ugome kutekeleza court marshal itakuhusu.
 
Uliwa

Hi kupita hata JKT?
Humu mtandaoni kila mtu ni mjuaji hata kwa,azichokijua.

Ndio maana askari huwa anapelwmekwa kufanya kazi mbali na kwao kwa sababu amri lazima itekekezwe.

Eti akipewa amri sio halali akatae hivi wewe unayepewa amri umepewa madaraka ya kutafsiri kuwa hii amri halali au la?

Hakuna askari atakayekataa amri kwani anajua kitakachomkuta. Inatakiwa utekeleze kwqnza halafu baadae utalalamika na kusikilizwa lakini sio ugome kutekeleza court marshal itakuhusu.
Hamna askari atakayemuua Mama yake Mzazi kisa Amri hayupo, labda Mwendawazimu tu, au akiambiwa awaue wenzake na yeye atekeleze bila kujiuliza atakuwa punguani sio mzima.
 
Anaongea tu huyo

Kuna amri za kukataa na Kuna amri ambazo kamwe kuzikataa utasokotwa mno.

Mfano jana pale mahakamani amri zinatoka juu wafanye vile kwa hiyo pale huwezi kataa hata kwa dawa sababu wakubwa au wanasiasa wapo nyuma ya pazia
Na ndo upuuzi tunaousema hapa, yaani watu hawajavunja sheria, hawajafanya kosa lolote unaambiwa kama mbwa ng’ata hao na wewe unaenda unang’ata ndo maana Wanasiasa Hawaheshimu mtu yeyote, wanajiona wako juu ya Sheria sababu hata waliopewa jukumu ya kuzisimamia sheria wanatekeleza amri za wakubwa na sio kufuata sheria inataka nini. Tuna tatizo kubwa sana kama Nchi huo ndo ukweli. Viongozi wetu wako juu ya sheria na hamna Chombo chenye makali ya kuwadhibiti.
 
Utamuua Mama yako sababu ya Amri ? Afu ukimaliza kumuua utaenda kumuuliza Boss wako sababu za kukupa hiyo amri au utaomboleza kimya kimya?
Ndio maana nimesema kutype raha maana kila kitu unajua.
Ila ungepita JKT ungeelewa maana sheria za jeshi zilifundishwa.

Nikusaidie kidogo kwa nin kuna Court marshal katika majeshi dunia nzima?

Mfano unaweza kutumwa kupiga rake vitani na una uhakikq asilimia 100 utauliwa na adui lakini lazima utaenda.

Endelea kujidanganya katika,key board.
 
vita ni jukumu la msingi la askari kulinda na kulitetea taifa lake, na katika vita matokeo yanafahamika hata kabla ya kwenda. Hilo la vita na amri ya kumuua mzazi wako ni vitu viwili tofauti. Zipo amri ambazo huweza kuwafanya askari wakakaidi amri na wakashtakiwa kwasababu kwa utashi wao waliona hizo Amri zipo kinyume na mambo wanayoyaamini, wanayoyatetea au ziko kinyume na maslahi yao. Akitokea Kiongozi akatoa Amri Msilipwe posho zenu tutaona kama watatii Amri.
 
Niliwahi kuchangia humu, kuna watu wanadai polisi wanatekeleza amri tu, yanayoendelea na wao hawakubali ila hawana namna zaidi ya kutii amri, nikauliza ukiwa polisi ukaamlishwa umuue mzazi wako utamuua kwasababu unatii amri ? Kiufupi uwezo wetu wa kufikiri sawa sawa kama binadamu anayepaswa kutafakari na kuamua kwa busara ni mdogo. Watu wetu wengi walio kwenye hivi vyombo hawapishani sana na robots ambazo utashi wake unategemea anayeliongoza
"Amri Halali ya Jeshi" ndio inayopaswa kutekelezwa na Police aliyekwenda shule ya upolice iliyokamilika.
Ile CCP pale Moshi na hapo Mgulani wanafundishwa nidhanu ya woga na kulinda viongozi na kupiga raia... Hamna kitu pale, ni ubabe tu.
 
vita ni jukumu la msingi la askari kulinda na kulitetea taifa lake, na katika vita matokeo yanafahamika hata kabla ya kwenda. Hilo la vita na amri ya kumuua mzazi wako ni vitu viwili tofauti. Zipo amri ambazo huweza kuwafanya askari wakakaidi amri na wakashtakiwa kwasababu kwa utashi wao waliona hizo Amri zipo kinyume na mambo wanayoyaamini, wanayoyatetea au ziko kinyume na maslahi yao. Akitokea Kiongozi akatoa Amri Msilipwe posho zenu tutaona kama watatii Amri.
Wewe unachoeleza ni maoni yako mimi ninaeleza utaratibu ulivyo, hiyo ndio tofauti yetu.
 
"Amri Halali ya Jeshi" ndio inayopaswa kutekelezwa na Police aliyekwenda shule ya upolice iliyokamilika.
Ile CCP pale Moshi na hapo Mgulani wanafundishwa nidhanu ya woga na kulinda viongozi na kupiga raia... Hamna kitu pale, ni ubabe tu.
Wapuuzi kweli, Viongozi wanavunja sheria wanasigina Katiba afu hawawakamati wanahangaika na raia wasio hata na hatia, eti Amri. Unaambiwa ukapige watu ambao hawana hata wembe una marungu na bunduki na wewe unaenda kutekeleza amri afu unajiona mzima kichwani
 
Wewe unachoeleza ni maoni yako mimi ninaeleza utaratibu ulivyo, hiyo ndio tofauti yetu.
Utaratibu unasemaje kwa viongozi wanaokiuka sheria na katiba, mbona hamuwakamati?
 
Hamna askari atakayemuua Mama yake Mzazi kisa Amri hayupo, labda Mwendawazimu tu, au akiambiwa awaue wenzake na yeye atekeleze bila kujiuliza atakuwa punguani sio mzima.
Hiyo amri atakupa nani? Hakuna mkubwa atakae kupa amri wewe ukamuue mama yako na ndo maana hata kwenye ma-oparesheni mbalimbali askari ambao sio wakazi wa kuzaliwa wa eneo hilo ndo upelekwa ili kuondoa huo ukakasi lakini vitu vingine fanya hata kama una malalamiko fanya kazi kwanza utalalamika ukishmaliza hiyo kazi
 
Back
Top Bottom