GE2025 Jamal Rwambow: Askari ana Haki kukataa Amri Kinyume cha Sheria, hata ikitoka kwa mkubwa wake

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Wewe umepita hata Jakata mzee maana inaonekana unaongea tu na kwa reply zako inaonesha hata jakata hujapita amri kijeshi haijadiliwi sijui unaelewa kitu haijadiliwi maana ikitolewa nenda katekeleze
Wapuuzi kweli, Viongozi wanavunja sheria wanasigina Katiba afu hawawakamati wanahangaika na raia wasio hata na hatia, eti Amri. Unaambiwa ukapige watu ambao hawana hata wembe una marungu na bunduki na wewe unaenda kutekeleza amri afu unajiona mzima kichwani
 
Hamna askari atakayemuua Mama yake Mzazi kisa Amri hayupo, labda Mwendawazimu tu, au akiambiwa awaue wenzake na yeye atekeleze bila kujiuliza atakuwa punguani sio mzima.
Kama mzazi wako kashika silaha na anashambulia watu na polisi hovyo hovyo, basi ukipewa amri utamuua tu. Kama mzazi wako kamteka Rais na wewe ndiye umepewa jukumu la kumuokoa, basi utamuua tu sababu.

Pia askari wenzako unaweza kuwaua kama wanakuwa wanafanya shambulizi ikulu la kupindua nchi, yani moto utawawashia tu

Kwahiyo unavyotoa mifano, eleza na mazingira.
 
Hayo mazingira ndo yanayofanya Amri iwe halali au haramu, Mzazi wako akiua watu tafsiri yake ni mvunja sheria, ukipewa amri ya kumuua kwasababu wewe unasimamia sheria then upo sawa, lakini Je ukipewa Amri ya kumuua ili hali hajafanya kosa wala kumdhuru yeyote utaua kwa kigezo cha kufuata amri? Tukubali tukatae zipo amri ni Halali na zipo Amri ni haramu, na mtu yeyote mwenye utashi anatakiwa awezs kupambanua kilichosahihi na kisicho sahihi ndo maana tuna ubongo, tofauti na hapo binadamu atakuwa robot tu kama kila kitu akiamridhwa yeye kazi yake itakuwa ni kutekeleza tu,
 
Uliwa

Hivi uliwahi kupita hata JKT?
Humu mtandaoni kila mtu ni mjuaji hata kwa,azichokijua.

Ndio maana askari huwa anapelekwa kufanya kazi mbali na kwao kwa sababu amri lazima itekekezwe.

Eti akipewa amri sio halali akatae hivi wewe unayepewa amri umepewa madaraka ya kutafsiri kuwa hii amri halali au la?

Hakuna askari atakayekataa amri kwani anajua kitakachomkuta. Inatakiwa utekeleze kwqnza halafu baadae utalalamika na kusikilizwa lakini sio ugome kutekeleza court marshal itakuhusu.
Wewe ndio hujui, hiyo haki ipo, any illegal order unaweza kuikataa ndio maana hakuna utetezi wa nilikuwa nafuata order, angalia Nuremberg trial uone askari wa Hitler walivyo pigwa vitanzi kwa kutekeleza illegal orders za wakubwa zao
 
Afadhali umpe darasa huyu jamaa, yaani wanakuwa na maamuzi kama kuku aliyekatwa kichwa, eti anafuata amri, amri ya kipuuzi kabisa. Wananchi wamekaa zao wanafatilia kesi, hawana hata wembe. Wewe askari unaenda na bunduki, virungu, mabomu ya machozi kutawanya watu ambao hata hawahatarishi amani yeyote. Kati ya Raia na huyo aliyekupa amri ya kupiga watu nani anahatarisha amani? Yaani haya majamaa yanafikiri siku utawala ukigeuka yatakua salama sijui hata huwa wanawaza hilo. Siku akiingia mtawala mwengine watu wanaweza kuswekwa ndani na vyeo vyao afu waseme walikuwa wanafuata Amri za maboss wao.
 
Tatizo polisi wengi ni vilaza na hata PGO hawaisomi.
FB_IMG_1758043509871.jpg
FB_IMG_1758043504520.jpg
FB_IMG_1758043531521.jpg
 
Uliwa

Hivi uliwahi kupita hata JKT?
Humu mtandaoni kila mtu ni mjuaji hata kwa,azichokijua.

Ndio maana askari huwa anapelekwa kufanya kazi mbali na kwao kwa sababu amri lazima itekekezwe.

Eti akipewa amri sio halali akatae hivi wewe unayepewa amri umepewa madaraka ya kutafsiri kuwa hii amri halali au la?

Hakuna askari atakayekataa amri kwani anajua kitakachomkuta. Inatakiwa utekeleze kwqnza halafu baadae utalalamika na kusikilizwa lakini sio ugome kutekeleza court marshal itakuhusu.

Wewe kama ulienda JK, huenda ni ile JK ya miezi mitatu ambayo hamfundishwi hata sheria za jeshi.

Sheria za jeshi, iwe JWTZ au polisi, inasema kuwa kukataa amri HALALI ya mkuu wako ni kosa, tena kosa kubwa. Kazi ipo hapo pa kutofautisha amri halali na isiyo halali. Polisi wanapelekwa chuoni, siyo kujifunza kupiga watu, bali zaidi kupata basics za sheria ili wafanye kazi kwa kufuata sheria. Polisi akitenda kinyume cha sheria, akishtakiwa, hakuna mahali popote atakapojitetea kuwa aliamrishwa na mkubwa wake. Atahukumiwa yeye kwa ujinga na uovu wake.
 
Una haki ya kukataa ila sio directly maana maelekezo au maamuzi ya kiongozi kwako ni amri na amri ni lazima itekelezwe.

Kinyume chake ni kumwambia hauwezi kutekeleza amri ambayo inakiuka haki na sheria za inchi na maadili ya kazi yako kisha urejeshe vitambulisho na kuacha kazi.
Au uitikie wito wa amri ila usifanye chochote kuitekeleza.
 
Ndio maana nimesema kutype raha maana kila kitu unajua.
Ila ungepita JKT ungeelewa maana sheria za jeshi zilifundishwa.

Nikusaidie kidogo kwa nin kuna Court marshal katika majeshi dunia nzima?

Mfano unaweza kutumwa kupiga rake vitani na una uhakikq asilimia 100 utauliwa na adui lakini lazima utaenda.

Endelea kujidanganya katika,key board.
Umeshikilia keyboard unaulizwa amri ikitoka umue mamayo utatekeleza then Ndo ukahoji jibu achan na hilo keyboard
 
Wewe ndio hujui, hiyo haki ipo, any illegal order unaweza kuikataa ndio maana hakuna utetezi wa nilikuwa nafuata order, angalia Nuremberg trial uone askari wa Hitler walivyo pigwa vitanzi kwa kutekeleza illegal orders za wakubwa zao

Afadhali umpe darasa huyu jamaa, yaani wanakuwa na maamuzi kama kuku aliyekatwa kichwa, eti anafuata amri, amri ya kipuuzi kabisa. Wananchi wamekaa zao wanafatilia kesi, hawana hata wembe. Wewe askari unaenda na bunduki, virungu, mabomu ya machozi kutawanya watu ambao hata hawahatarishi amani yeyote. Kati ya Raia na huyo aliyekupa amri ya kupiga watu nani anahatarisha amani? Yaani haya majamaa yanafikiri siku utawala ukigeuka yatakua salama sijui hata huwa wanawaza hilo. Siku akiingia mtawala mwengine watu wanaweza kuswekwa ndani na vyeo vyao afu waseme walikuwa wanafuata Amri za maboss wao.

Wewe kama ulienda JK, huenda ni ile JK ya miezi mitatu ambayo hamfundishwi hata sheria za jeshi.

Sheria za jeshi, iwe JWTZ au polisi, inasema kuwa kukataa amri HALALI ya mkuu wako ni kosa, tena kosa kubwa. Kazi ipo hapo pa kutofautisha amri halali na isiyo halali. Polisi wanapelekwa chuoni, siyo kujifunza kupiga watu, bali zaidi kupata basics za sheria ili wafanye kazi kwa kufuata sheria. Polisi akitenda kinyume cha sheria, akishtakiwa, hakuna mahali popote atakapojitetea kuwa aliamrishwa na mkubwa wake. Atahukumiwa yeye kwa ujinga na uovu wake.
Nitarudi hapa kusoma majibu yake
 
Huyo jamaa hapo anachanganya mambo na anatoa mifano mfu kwamba kama hakuna kujadili amri basi ukipewa amri ya kumuua mama yako umuue basi hahaha!

Kwanini umuue yani itokee tu umuue bila sababu na kiongozi gani huyo mwehu akupe hiyo amri na hakuna kiongozi ambae atakupa hiyo amri kipumbavu kamwe kwa hiyo kwenye justification yako kwenye hoja yako toa hii kitu.

Kama ni mhalifu anapigwa tu chuma hata kama ni baba yako na mara nyingi wakijua wewe una undugu na huyo faza basi kwenye hiyo mission unaondolewa

Ukija kwenye siasa hakuna Jeshi lililo salama ukitoa Zimamoto yote yanatumika na wanasiasa sababu wanajua kabisa hawa jamaa udhaifu wao ni kupokea amri na kuitekeleza iwe JW, PT, MT na UT yote yanatumika sema wananchi hamuoni na mlivo wajinga hamtakuja kung'amua hichi kitu na sababu kubwa ya yote hii ni WANANCHI WAJINGA kwenye hii nchi ikiwemo muanzisha mada kutoka kuitetea nchi yake let's say kwenye maandamano hatoki halafu anakuja kwenye mitandao kulalamikia vyombo vya ulinzi na usalama hivi unadhani wao wanapenda kufanya hayoo?

Mmeruhusu viongozi wajinga wawatawale halafu mnaanza ooh vyombo vya ulinzi viko wapi mara sijui vinaonea watu naumiaga sana nkiona hii kauli kwa sababu Mwananchi huyu anategemea akombolewe huku yeye akiwa nyumbani ngoja nkwambie kitu hivi vyombo vinaapa kulinda Serikali zinazokuepo madarakani sasa bila Mwananchi mwenyewe kuingia mtaani hivi vyombo haviwezi kuwa upande wako hadharani sababu wameapa kumtii Rais
 
Jamal Rwambow
Andengenye
Susan Kaganda
Tibaigana
Ni kati ya viongozi wa polisi waliokua na utu katika jeshi la polisi.
Kama kuna wengine tufahamisheni.
 
Huyo jamaa hapo anachanganya mambo na anatoa mifano mfu kwamba kama hakuna kujadili amri basi ukipewa amri ya kumuua mama yako umuue basi hahaha!

Kwanini umuue yani itokee tu umuue bila sababu na kiongozi gani huyo mwehu akupe hiyo amri na hakuna kiongozi ambae atakupa hiyo amri kipumbavu kamwe kwa hiyo kwenye justification yako kwenye hoja yako toa hii kitu.

Kama ni mhalifu anapigwa tu chuma hata kama ni baba yako na mara nyingi wakijua wewe una undugu na huyo faza basi kwenye hiyo mission unaondolewa

Ukija kwenye siasa hakuna Jeshi lililo salama ukitoa Zimamoto yote yanatumika na wanasiasa sababu wanajua kabisa hawa jamaa udhaifu wao ni kupokea amri na kuitekeleza iwe JW, PT, MT na UT yote yanatumika sema wananchi hamuoni na mlivo wajinga hamtakuja kung'amua hichi kitu na sababu kubwa ya yote hii ni WANANCHI WAJINGA kwenye hii nchi ikiwemo muanzisha mada kutoka kuitetea nchi yake let's say kwenye maandamano hatoki halafu anakuja kwenye mitandao kulalamikia vyombo vya ulinzi na usalama hivi unadhani wao wanapenda kufanya hayoo?

Mmeruhusu viongozi wajinga wawatawale halafu mnaanza ooh vyombo vya ulinzi viko wapi mara sijui vinaonea watu naumiaga sana nkiona hii kauli kwa sababu Mwananchi huyu anategemea akombolewe huku yeye akiwa nyumbani ngoja nkwambie kitu hivi vyombo vinaapa kulinda Serikali zinazokuepo madarakani sasa bila Mwananchi mwenyewe kuingia mtaani hivi vyombo haviwezi kuwa upande wako hadharani sababu wameapa kumtii Rais
Wananchi wana haki ya kuogopa, sababu hata wanapokuwa hawajavunja sheria na kutekeleza haki yao ya kikatiba, watunza sheria na walioapa kuilinda katiba ndo wakwanza kutumika na Wanasiasa kuwapiga raia wema na kuwatia hofu ya kushindwa kutekeleza haki yao kikatiba. Kama hivi vyombo vingekuwa rafiki na vipo kwa maslahi ya Wananchi na sio kundi dogo, Wananchi wasingekuwa na hofu. Hapa tunachosubiri ni siku ambayo Watanzania wataona ni gharama kubwa sana kuwa na Hofu kuliko kutokuwa na Hofu katika kutetea maslahi yao. Na siku tukifika hapa athari yake zinaweza kuwa kubwa sana sababu ni kitu ambacho hatujawahi kukipitia na wengi wetu hatuamini kama inawezekana. Muda ndo utaamua hilo
 
Back
Top Bottom