Kuna Mhudumu mmoja nilikutana nae kwenye Mgahawa mmoja mzuri tu. Yule dada ni mzuri ajabu.
Nikawa napenda kwenda kula pale kila mara kutokana na huduma yake, mchangamfu na anatabasamu kitendo cha kukuona.
Nilipotea kama mwezi bila kwenda pale. Sasa kuna siku nilikutana nae bandarini kavaa na kitambulisho kabisaa.
Tulisalimiana viziru na kumwuliza kulikoni huku tena? Akanieleza kuwa pale alikuwa anajishikiza tu.
Nimsomi wa UD, ana bachelor yake safi ya account na finance. Kwasasa kaajiriwa na kampuni ya kutoa makontena pale.
Nimekuja kutana nae tena kama miez sita baadae, mtoto anaendesha Athlete Crown, hizi tunazoziogopa kwa ulaji mafuta. Ni rafiki yangu sana na kajisaidia kujua vitu vingi.
Aisee,
Toka siku hiyo nina nidham na wahudumu.
Usimdharau mtu usie mjua.
Sent using
Jamii Forums mobile app