Jaman tuwaheshimu waiter/waitress tunapokuwa bar,hotelini au restaurant.

Jaman tuwaheshimu waiter/waitress tunapokuwa bar,hotelini au restaurant.

Thanks mama. Mleta mada hakuweka hiyo taarifa.

Ila huo ni upuuzi. Sehemu nyingi ambazo hawaruhusu waiter mmoja mmoja kuchukua tip, huwa wana basket tip. Hii ni sehemu ambapo tip zote zinaingia na baadaye wote wanagawana pasu kwa pasu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hizo za tip collection ni taratibu za sehemu husika.
 
Mama, I get you lakini hata Kama ni wewe ungekwazika. Lakini kwa sababu tunapata one side of the story, then tuna assume Jamaa alikuwa mwenye makosa

Sent using Jamii Forums mobile app
Najua kuna watu wako humu wako nchi zingine wanaelewa kuwa kumtip waiter au waitress ipo tu kuna nchi nyingine wanaanzia 10-20%ya ulichokitumia.

South Africa 🇿🇦 hapo sio mbali.10%kwa waitress aliyekuhudumiA.
 
Kuna muhudumu wa hotel alimuokoa jamaa mmoja alifika pale hotel akaa kama wiki,kumbe kuna majambazi wanamfatilia ,yule muhudumu aliwasikia mipango yao akamshutua jamaa akahama kimya kimyaa

Ni vizuri kuwapa tip kwa nia njema maana jamaa alikuwa akimpa tip yule dada na akamuokoa na alikuja jua wale watu ni wa karibu tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante kunisaidia kuwaelewesha mkuu
 
Tujifunze kuwaheshimu wadada wa kazi wa nyumbani pia Hawa wameshikilia uhai wetu ni vile hatujuagi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Inasikitisha mkuu asikwambie mtu.
Anakuwa wakwanza kuamka wa mwisho kulala na wakati wa kula achangamani na familia.
Tena haya matukio ya wadada wakazi ninayo mengi mno....
 
Watu huwa wanawadharau sana walinzi Lkn ni watu wenye msaada mkubwa sana na wana information nyingi sana za watu.
Kuna Mlinzi mmoja alimkomesha boss wake wallah huko aliko huyo boss kama hajabadilika sijui..

Tunajisahau tu na hatuna ubinadam wakati mwingine
 
Kuna Mhudumu mmoja nilikutana nae kwenye Mgahawa mmoja mzuri tu. Yule dada ni mzuri ajabu.
Nikawa napenda kwenda kula pale kila mara kutokana na huduma yake, mchangamfu na anatabasamu kitendo cha kukuona.

Nilipotea kama mwezi bila kwenda pale. Sasa kuna siku nilikutana nae bandarini kavaa na kitambulisho kabisaa.

Tulisalimiana viziru na kumwuliza kulikoni huku tena? Akanieleza kuwa pale alikuwa anajishikiza tu.

Nimsomi wa UD, ana bachelor yake safi ya account na finance. Kwasasa kaajiriwa na kampuni ya kutoa makontena pale.

Nimekuja kutana nae tena kama miez sita baadae, mtoto anaendesha Athlete Crown, hizi tunazoziogopa kwa ulaji mafuta. Ni rafiki yangu sana na kajisaidia kujua vitu vingi.

Aisee,
Toka siku hiyo nina nidham na wahudumu.

Usimdharau mtu usie mjua.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli tuweheshim tu watu wa sekta zote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alikudanganya hizo habari za alikua anajishikiza hapo bar.

Hakuna sehemu vijna wa kitengo wamemwagwa kama huko bandarini,sababu mzee baba anaamini kuna wizi umekithiri.

Akili kichwani Bob.
Alimaanisha alikuwa anajishikiza ktk mgahawa hapo awali kabla ya kwenda bandarini
 
Kwanza naomba nionye wazi wazi tip sio lazima na mtu kujisikia kwa huduma aliyopata.
Maana kuna baadhi ya maeneo wahudumu huketa figisu kurejesha chenji wakilazimisha tip.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza naomba nionye wazi wazi tip sio lazima na mtu kujisikia kwa huduma aliyopata.
Maana kuna baadhi ya maeneo wahudumu huketa figisu kurejesha chenji wakilazimisha tip.

Sent using Jamii Forums mobile app
MKuu kuna tofauti kati ya asante ya tip kutoka kwa mteja kwenda kwa waiter.ninachozungumzi ni tip mteja kukupa yeye sio kuchikichia na chenji ya watu.au kama mteja analipa kwa card 💳 anakusignia tip yako wewe waiter.

Hicho unachokizungumzia wewe ni uswahili na pia ukiweza waweza mshtaki kwa boss wake kuwa kakuibia na sheria ikafuatwa
 
Back
Top Bottom