Siku ukiona ukuu wa Mungu hutasema haya hata sisi tulikuwa wabishi sn ...
Walokole tafuteni kitu kingine cha kuongelea.. nyie kila saa ni uchawi na mapepo. Ingekuwa magonjwa yanatoweka kwa kukemea basi walokole wote msingekua mnaenda hospitali.
Safi kabisaHii sio chit chat. Nimethibitisha kwa macho na masikio yangu, na kuonja kwa nafsi yangu. Tangu nilipompokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wangu, nafaidi utamu huu:
Kama huo sio utamu ni nini?
- Siogopi wachawi wala siogopi kulala kwenye nyumba zenye vibwengo – wachawi wakinijia, nawapiga 'knock out' kwa Jina la Yesu (Isa 54:17).
- Nikiomba napewa – kila sala yangu imekuwa na matunda (Mt 7:7).
- Magonjwa ya zinaa hayanipati ng'oo – uasherati kwangu ni mwii... ni mwiko (1 Kor 6:18).
- Na-save pesa nyingi za matibabu – kwa kuwa magonjwa mengi nayakemea na yanatoweka kwa Jina la Yesu (Isa 53:5).
- Nina amani isiyoelezeka – amani aliyonipa Yesu haipatikani kwa njia nyingine (Yn 14:27). Nina amani hata katikati ya majaribu na dhoruba (Yn 20:19).
- Sipati kamwe hangover ya walevi – furaha yangu haina majuto. Nikifurahi leo, sijuti wala kuona aibu kesho (Flp 4:4).
- Sipatwi na mikosi na mabalaa ya kulogwa – kwakuwa hakuna uchawi unaofanikiwa juu yangu (Hes 23:23).
- Bwana ndiye Mchungaji wangu, hivyo sipungukiwi na kitu (Zab 23:1). Mungu amekuwa akibariki kazi za mikono yangu kila siku mjini na mashambani (Kum 28:3)
- Namshinda shetani na mapepo yake kirahisi kabisa – akiinua kichwa, nambamiza chini na kumtimua kwa Jina la Yesu (Yk 4:7).
- Mungu amenipa maarifa mengi ya kikazi na kimaisha kama alivyofanya kwa Bezaleli(Kut 31:2-5)
- Sina hofu ya kifo – kufa kwangu ni faida (Flp 1:21). Ni faida kwa sababu nikifa nitafufuka tena na kuvishwa taji ya uzima (2 Tim 4:8), katika makao ambayo Yesu alienda kuniandalia mbinguni (Yn 14:2).
Ndugu zangu, shetani ni muongo. Anawashawishi watu wasiokoke ili wakose baraka hizo. Kuokoka sio hadithi, sio kuwa taahira — ni maisha ya ushindi, furaha na uhakika wa uzima wa milele.
Mimi nimeonja, na nimethibitisha mwenyewe kuwa kweli Bwana Yesu ni mwema! (Zaburi 34:8). Na wewe onja leo maisha ya wokovu kwa kutubu dhambi zako na kuziacha, kisha umpokee Yesu moyoni mwako kwa imani, awe Bwana na Mwokozi wako.
Ukuu wa Mungu upo kwa kila mtu sio lazima niwe mlokole ndo nione ukuu wa Mungu.Siku ukiona ukuu wa Mungu hutasema haya hata sisi tulikuwa wabishi sn ...
Outstanding. Huo ni ushuhuda msafi kabisa. Miaka 25 unakula utamu. Wow, shuhuda za namna hii shetwani hapendi watu wazisikie. Lakini leo tumemwaibisha. Mungu akubariki sana ndugu yangu kwa ku-share jinsi unavyouona wema wa Mungu tangu O-level. Hakika kila amwaminiye Mwana wa Mungu anao ushuhuda (1 Yohana 5:10). Haleluya!Hakika Kumwamini Yesu kuna baraka sana. 2kor 5:17, "Hata imekuwa, Mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita, tazama yamekuwa mapya". Nimeokoka nikiwa mwanafunzi wa sekondari O'level, na sasa ni zaidi ya miaka 25, ninauona wema wa Mungu maishani mwangu. Yesu yu karibu kurudi, fanya hima ndugu kuokoka, kabla neema hii haijafungwa.
Nipo duniani ndugu yangu. Nikiingia mbinguni sitakuwa na mawasiliano tena na wewe. Mungu amenituma nikuambie wewe na wengine, uzuri wa kuokoka: Unabarikiwa hapa duniani na mbinguni utapata raha ya milele. Usikawie kuokoka. Yesu akirudi kabla hujaokoka, utalia na kusaga meno, maana utaachwa katika dhiki kuu ambayo haijawahi kuwepo tangu kuumbwa kwa ulimwengu.Upo duniani au umeshakwenda mbingu?
Rubbish.Leo shetwani amemeza wembe; unamkatakata matumbo!
Your curt repudiation, though perhaps cathartic to your own inclinations, is the rhetorical equivalent of attempting to eclipse the sun with a thimble. The transformative veracity of salvation is neither contingent upon your concurrence nor susceptible to the erosion of casual derision; it is self-authenticating, anchored in an immutable ontological constancy that transcends the ephemeral tides of human opinion. But alas, one cannot fault the blind for failing to appreciate the sunrise.Rubbish.
Rubbish.Your curt repudiation, though perhaps cathartic to your own inclinations, is the rhetorical equivalent of attempting to eclipse the sun with a thimble. The transformative veracity of salvation is neither contingent upon your concurrence nor susceptible to the erosion of casual derision; it is self-authenticating, anchored in an immutable ontological constancy that transcends the ephemeral tides of human opinion. But alas, one cannot fault the blind for failing to appreciate the sunrise.