Jamani asiwadanganye mtu — kuokoka ni kutamu!

Jamani asiwadanganye mtu — kuokoka ni kutamu!

Hii sio chit chat. Nimethibitisha kwa macho na masikio yangu, na kuonja kwa nafsi yangu. Tangu nilipompokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wangu, nafaidi utamu huu:
  • Siogopi wachawi wala siogopi kulala kwenye nyumba zenye vibwengo – wachawi wakinijia, nawapiga 'knock out' kwa Jina la Yesu (Isa 54:17).
  • Nikiomba napewa – kila sala yangu imekuwa na matunda (Mt 7:7).
  • Magonjwa ya zinaa hayanipati ng'oo – uasherati kwangu ni mwii... ni mwiko (1 Kor 6:18).
  • Na-save pesa nyingi za matibabu – kwa kuwa magonjwa mengi nayakemea na yanatoweka kwa Jina la Yesu (Isa 53:5).
  • Nina amani isiyoelezeka – amani aliyonipa Yesu haipatikani kwa njia nyingine (Yn 14:27). Nina amani hata katikati ya majaribu na dhoruba (Yn 20:19).
  • Sipati kamwe hangover ya walevi – furaha yangu haina majuto. Nikifurahi leo, sijuti wala kuona aibu kesho (Flp 4:4).
  • Sipatwi na mikosi na mabalaa ya kulogwa – kwakuwa hakuna uchawi unaofanikiwa juu yangu (Hes 23:23).
  • Bwana ndiye Mchungaji wangu, hivyo sipungukiwi na kitu (Zab 23:1). Mungu amekuwa akibariki kazi za mikono yangu kila siku mjini na mashambani (Kum 28:3)
  • Namshinda shetani na mapepo yake kirahisi kabisa – akiinua kichwa, nambamiza chini na kumtimua kwa Jina la Yesu (Yk 4:7).
  • Mungu amenipa maarifa mengi ya kikazi na kimaisha kama alivyofanya kwa Bezaleli(Kut 31:2-5)
  • Sina hofu ya kifo – kufa kwangu ni faida (Flp 1:21). Ni faida kwa sababu nikifa nitafufuka tena na kuvishwa taji ya uzima (2 Tim 4:8), katika makao ambayo Yesu alienda kuniandalia mbinguni (Yn 14:2).
Kama huo sio utamu ni nini?
Ndugu zangu, shetani ni muongo. Anawashawishi watu wasiokoke ili wakose baraka hizo. Kuokoka sio hadithi, sio kuwa taahira — ni maisha ya ushindi, furaha na uhakika wa uzima wa milele.

Mimi nimeonja, na nimethibitisha mwenyewe kuwa kweli Bwana Yesu ni mwema! (Zaburi 34:8). Na wewe onja leo maisha ya wokovu kwa kutubu dhambi zako na kuziacha, kisha umpokee Yesu moyoni mwako kwa imani, awe Bwana na Mwokozi wako.
View attachment 3442615
Dudu unapigwa au umeliweka kando
 
Tahadhari: Mafundisho ya O. O. O. yanatofautiana sana na mafundisho yanayokubalika, ya Kikristo. Wanaomshabikia wanaweza kupotea kiroho kwa sababu wanamwacha Yesu Kristo na kumsujudia mtu. Hizi ni nyakati za hatari zilizotabiriwa kwamba kutatokea manabii wa uongo na Makristo wa uongo.
Mt 24:24
Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.
HUJUI TU HADI HAPO HUJAOKOKA ..KWA KUWA ALISEMA ATARUDI AMERUDI KUTAWALA UNA UTOFAUT GANI NA WAYAHUDI?
 
Nimeokoka na nampenda Yesu,sina stress yoyote namuona Mungu akinivusha kutoka utukufu hadi utukufu.Nathibitisha yote uliyoyasema hapo ni kweli
 
Uko sahihi, hujakosea. Ni kweli magonjwa hayaangalii ulokole. Hata mimi sijasema kwamba walokole hawapatwi na magonjwa, wanaugua, lakini Mungu anatuangalia walokole na kutuponya magonjwa yetu yote.
Zab 103:3
Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote
Kwa hiyo kama sio mlokole Mungu hakuponyi?
 
Kwa hiyo kama sio mlokole Mungu hakuponyi?
Kwa neema ya Mungu, ukiombewa, Mungu anaweza kukuponya, ila kama sio mlokole huwezi kukemea ugonjwa ukatoweka, maana mamlaka hayo wamepewa walokole tu. Tatizo la kusubiri uombewe ni kwamba, unaweza kuangukia mikononi mwa matapeli wanaodai kwanza ununue chumvi na mafuta yao feki ya upako, ndio wakuombee😎
 
Hayo mamlaka walipewa lini na wapi? Kwa hiyo Mungu huwaacha watu wateseke hadi asikie mlokole akikemea ndo hujitokeza?
 
Hayo mamlaka walipewa lini na wapi?
Ukiokoka unakuwa mwnafunzi wa Yesu na papo hapo unapewa mamlaka ya kukemea pepo na kuponya maradhi
Lk 9:1
Akawaita wale Thenashara, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi
Kwa hiyo Mungu huwaacha watu wateseke hadi asikie mlokole akikemea ndo hujitokeza?
Mungu anapenda tumuombe au tumueleze shida zetu. Usipoomba au kukemea ni wazi utaendelea kuteseka(Yak 4:2-3). Hata wewe kama una mtoto ndivyo unavyofanya. Mtoto wako akililia kitu fulani ndio unampa.
Kumbuka pia habari za yule kipofu katika Biblia. Yesu alimuona kabisa kuwa ni kipofu lakini alimuuliza "wataka nikufanyie nini" Alivyosema anataka kuona ndio Yesu akamponya (Mk 10:51)
 
Ukiokoka unakuwa mwnafunzi wa Yesu na papo hapo unapewa mamlaka ya kukemea pepo na kuponya maradhi
Lk 9:1
Akawaita wale Thenashara, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi

Mungu anapenda tumuombe au tumueleze shida zetu. Usipoomba au kukemea ni wazi utaendelea kuteseka(Yak 4:2-3). Hata wewe kama una mtoto ndivyo unavyofanya. Mtoto wako akililia kitu fulani ndio unampa.
Kumbuka pia habari za yule kipofu katika Biblia. Yesu alimuona kabisa kuwa ni kipofu lakini alimuuliza "wataka nikufanyie nini" Alivyosema anataka kuona ndio Yesu akamponya (Mk 10:51)
Wewe ni thenashara au hata umetokana na hicho kizazi cha mathenashara?
 
Wewe ni thenashara au hata umetokana na hicho kizazi cha mathenashara?
Mimi ni mwanafunzi wa Yesu niliyetokana na kazi waliyotumwa kufanya hao thenashara
Mt 28:19
'Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho' Mtakatifu
 
Back
Top Bottom