ras jeff kapita
JF-Expert Member
- Jan 4, 2015
- 22,728
- 34,860
Dudu unapigwa au umeliweka kandoHii sio chit chat. Nimethibitisha kwa macho na masikio yangu, na kuonja kwa nafsi yangu. Tangu nilipompokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wangu, nafaidi utamu huu:
Kama huo sio utamu ni nini?
- Siogopi wachawi wala siogopi kulala kwenye nyumba zenye vibwengo – wachawi wakinijia, nawapiga 'knock out' kwa Jina la Yesu (Isa 54:17).
- Nikiomba napewa – kila sala yangu imekuwa na matunda (Mt 7:7).
- Magonjwa ya zinaa hayanipati ng'oo – uasherati kwangu ni mwii... ni mwiko (1 Kor 6:18).
- Na-save pesa nyingi za matibabu – kwa kuwa magonjwa mengi nayakemea na yanatoweka kwa Jina la Yesu (Isa 53:5).
- Nina amani isiyoelezeka – amani aliyonipa Yesu haipatikani kwa njia nyingine (Yn 14:27). Nina amani hata katikati ya majaribu na dhoruba (Yn 20:19).
- Sipati kamwe hangover ya walevi – furaha yangu haina majuto. Nikifurahi leo, sijuti wala kuona aibu kesho (Flp 4:4).
- Sipatwi na mikosi na mabalaa ya kulogwa – kwakuwa hakuna uchawi unaofanikiwa juu yangu (Hes 23:23).
- Bwana ndiye Mchungaji wangu, hivyo sipungukiwi na kitu (Zab 23:1). Mungu amekuwa akibariki kazi za mikono yangu kila siku mjini na mashambani (Kum 28:3)
- Namshinda shetani na mapepo yake kirahisi kabisa – akiinua kichwa, nambamiza chini na kumtimua kwa Jina la Yesu (Yk 4:7).
- Mungu amenipa maarifa mengi ya kikazi na kimaisha kama alivyofanya kwa Bezaleli(Kut 31:2-5)
- Sina hofu ya kifo – kufa kwangu ni faida (Flp 1:21). Ni faida kwa sababu nikifa nitafufuka tena na kuvishwa taji ya uzima (2 Tim 4:8), katika makao ambayo Yesu alienda kuniandalia mbinguni (Yn 14:2).
Ndugu zangu, shetani ni muongo. Anawashawishi watu wasiokoke ili wakose baraka hizo. Kuokoka sio hadithi, sio kuwa taahira — ni maisha ya ushindi, furaha na uhakika wa uzima wa milele.
Mimi nimeonja, na nimethibitisha mwenyewe kuwa kweli Bwana Yesu ni mwema! (Zaburi 34:8). Na wewe onja leo maisha ya wokovu kwa kutubu dhambi zako na kuziacha, kisha umpokee Yesu moyoni mwako kwa imani, awe Bwana na Mwokozi wako.
View attachment 3442615
Ila mtafute Mungu katika roho na kweli..kaa kwenye mapito yake...Ukuu wa Mungu upo kwa kila mtu sio lazima niwe mlokole ndo nione ukuu wa Mungu.
HUJUI TU HADI HAPO HUJAOKOKA ..KWA KUWA ALISEMA ATARUDI AMERUDI KUTAWALA UNA UTOFAUT GANI NA WAYAHUDI?Tahadhari: Mafundisho ya O. O. O. yanatofautiana sana na mafundisho yanayokubalika, ya Kikristo. Wanaomshabikia wanaweza kupotea kiroho kwa sababu wanamwacha Yesu Kristo na kumsujudia mtu. Hizi ni nyakati za hatari zilizotabiriwa kwamba kutatokea manabii wa uongo na Makristo wa uongo.
Mt 24:24
Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.
unamshabikia Yesu kristo ambaye karudi kwa jina jipya la Olumba Olumba Obu
Hata mimi imenivutiaSafi sana hiyo nyimbo nimeipenda
Mungu ni wa woteIla mtafute Mungu katika roho na kweli..kaa kwenye mapito yake...
Kwa hiyo kama sio mlokole Mungu hakuponyi?Uko sahihi, hujakosea. Ni kweli magonjwa hayaangalii ulokole. Hata mimi sijasema kwamba walokole hawapatwi na magonjwa, wanaugua, lakini Mungu anatuangalia walokole na kutuponya magonjwa yetu yote.
Zab 103:3
Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote
Kwa neema ya Mungu, ukiombewa, Mungu anaweza kukuponya, ila kama sio mlokole huwezi kukemea ugonjwa ukatoweka, maana mamlaka hayo wamepewa walokole tu. Tatizo la kusubiri uombewe ni kwamba, unaweza kuangukia mikononi mwa matapeli wanaodai kwanza ununue chumvi na mafuta yao feki ya upako, ndio wakuombee😎Kwa hiyo kama sio mlokole Mungu hakuponyi?
Hayo mamlaka walipewa lini na wapi? Kwa hiyo Mungu huwaacha watu wateseke hadi asikie mlokole akikemea ndo hujitokeza?Kwa neema ya Mungu, ukiombewa, Mungu anaweza kukuponya, ila kama sio mlokole huwezi kukemea ugonjwa ukatoweka, maana mamlaka hayo wamepewa walokole tu. Tatizo la kusubiri uombewe ni kwamba, unaweza kuangukia mikononi mwa matapeli wanaodai kwanza ununue chumvi na mafuta yao feki ya upako, ndio wakuombee😎
Ukiokoka unakuwa mwnafunzi wa Yesu na papo hapo unapewa mamlaka ya kukemea pepo na kuponya maradhiHayo mamlaka walipewa lini na wapi?
Mungu anapenda tumuombe au tumueleze shida zetu. Usipoomba au kukemea ni wazi utaendelea kuteseka(Yak 4:2-3). Hata wewe kama una mtoto ndivyo unavyofanya. Mtoto wako akililia kitu fulani ndio unampa.Kwa hiyo Mungu huwaacha watu wateseke hadi asikie mlokole akikemea ndo hujitokeza?
Wewe ni thenashara au hata umetokana na hicho kizazi cha mathenashara?Ukiokoka unakuwa mwnafunzi wa Yesu na papo hapo unapewa mamlaka ya kukemea pepo na kuponya maradhi
Lk 9:1
Akawaita wale Thenashara, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi
Mungu anapenda tumuombe au tumueleze shida zetu. Usipoomba au kukemea ni wazi utaendelea kuteseka(Yak 4:2-3). Hata wewe kama una mtoto ndivyo unavyofanya. Mtoto wako akililia kitu fulani ndio unampa.
Kumbuka pia habari za yule kipofu katika Biblia. Yesu alimuona kabisa kuwa ni kipofu lakini alimuuliza "wataka nikufanyie nini" Alivyosema anataka kuona ndio Yesu akamponya (Mk 10:51)
Mimi ni mwanafunzi wa Yesu niliyetokana na kazi waliyotumwa kufanya hao thenasharaWewe ni thenashara au hata umetokana na hicho kizazi cha mathenashara?