Jamani biashara hii ya daladala ni pasua kichwa

Mr Equalizer

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2013
Posts
611
Reaction score
727
Baada ya kutoka chuo kikuu, niliamua kufanya biashara ya daladala ili maisha yasonge, cha ajabu hii biashara ni pasua kichwa. Utasikia mara tochi, bao mara gari imeharibika nk

Binafsi napenda sana biashara ya usafirishaji, kama kuna mtu ana uzoefu nayo zaidi naomba anisadie.

Pili, kama kuna fursa zingine nzuri zaidi naomba tushirikishane jamani, naweza nikapiga hii chini nikawekeza kwingine.
 
Jenga nyumba nyingi kadri uwezavyo....
 
Kilimo ndio mpango.... Tafuta eneo lenye maji ulime kilimo cha umwagiliaji.
 
Kama huna kazi nyingine geuza hiyo gari yako kua ofisi yako, endesha mwenyewe, kila baada ya ruti moja ukifika chukua mafao kwa konda, lipia gari vibali vyote vya Serekali, endesha kwa kufuata taratibu na sheria za nchi uwapo barabarani. Ukifanya hivyo hutajuta na utakuja kunipa asante yangu
 
Kaka asante kwa ushauri mzuri, ila ninafanya kazi ya ualimu wa sekondari, labda nipange ratiba yangu upya.
 
Umeshatoa hitimisho kuwa ni biashara kichaa! sasa unahitaji ushauri wa nn?nipo kwenye biashara ya Dalalada long time ago na sifikiri hata siku moja nitakuja kuacha!kama vp tufanye biashara hiyo hiace uliyonayo uendelee kufundisha
Sawa mkuu, unaonekana una uzoefu kuliko mimi, lengo langu hapa ni kutafuta ushauri kwa watu wenye uzoefu zaidi kuhusu hii biashara, huenda labda mimi ninapungukiwa maarifa fulani.
 
Komaa mkuu
 
Hakuna biashara ngumu kama ya usafiri ni pasua kichwa hasa na usipokuwa makini inaweza kukufilisi kabisa.

 
Biashara ya gari ukitakaa iwe nzuri uwe konda wewe mwenyewe

Au umpate dereva muaminifu haswa

Wengi madereva sio waaminifu
 
Hiyo ndio athari ya kuvamia fani za watu me siamini kama unajua kauli za kumtongoza trafiki ukijifanya unalipa kila faini utaishia kuwafanyia kazi hao.
 
hiyo ndo athari ya kuvamia fani za watu me siamini kama unajua kauli za kumtongoza trafiki ukijifanya unalipa kila faini utaishia kuwafanyia kazi hao
Fani za watu maana yake nini? Mbona watanzania tuna mitazamo ya kukatishana tamaa, kwani ukinishauri positively utapungukiwa nini mkuu, haya bwana wewe ni mjanja mimi ni mshamba......... endelea......
 
Siku zote usicheke na Konda, dereva! Hao watu wakikuona laini laini tu umekwisha, kama mmekubaliana kwa siku ni sh 50000/=

Hakikisha inatimia. Kingine kwakuwa wao ndo wanashinda na gari, service ndogo ndogo na faini visiwe juu yako wewe, vinginevyo utafanya services na faini fake kila siku mwisho wa siku gari inakufa wanakuacha huna kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…