kuvunja ungo hakuendani na akili,manake hata magoigoi wanavunja ungo. ni factor ya hormones, lakini hamna budi kumuandaa kwa hilo pia kabla hajawahiwa na 'mwalimu'. siku akiona tangazo la pedi kwenye tv,akauliza swali mnamshukia na information full package. ili kupunguza concern ya kutokua na adabu, mnaweza kumfunza kuhusu kusubiri. unaweza kumuambia 'ngoja tuangalie taarifa ya habari, na tutaongea kuhusu hili jumamosi wakati tumetulia na tuna nafasi'. hiyo itakupa muda pia wa kujiandaa kwa maswali magumu. na kama unaona hauko comfortable kuongea nae kitu unaweza kumuambia kama surprise tu'actually aunt king'asti ni mtaalamu wa mambo hayo, ngoja atakuja wknd atufundishe pamoja na sie', then unaweza kupata udhuru akabaki na mamake na mtu unaetaka aongee nae. kumfundisha timing ya kuongelea mambo ama kutoa mawazo yake inaweza kuondoa kibri, ajue nani ana kauli hapo. akikosa adabu ama ku-embarass mtu usikose kumuadhibu.mfundishe kuwa sio lazima kila wakati kuonesha kila mtu kuwa unajua kila kitu,inaumiza watu na kuwafanya wasijisikie uzuri.
inaweza kuwa muhimu kufuatilia jinsi gani anatumia muda wake akiwa shuleni kwa kuongea na walimu pia. dawa ya mwanao ni kumpa assignment za kusoma vitabu. akimaliza vya sayansi za kitoto na dini mkomelee history and biographies. unaweza kumpa kitabu asome na wknd mkatumia muda akupe feedback ya characters waliomo. ila itakubidi nawe usome na kujitanua awazo na uzee wako huo,lol.[/QUOTE]
Nimeipenda sana hii ubarikiwe mama na Mungu azidi kukuongezea maarifa, binti akinianzia tu mbona nitakualika useme nae lol