Jamaa karudi home ghafla na kupata mshtuko kukuta
mkewe kipenzi ana bwana ndani, baada ya zogo
kubwa, wanaume wakaenda ukumbini kumalizana
kiungwana;
MUME: Sikiliza mi nakusamehe niachie
mke wangu ananipenda ila ni shetani tu kampitia
MGONI: Lakini mimi niko nae siku nyingi, hawezi kuniacha ananipenda sana
MUME: Hebu tufyatue risasi
na kujifanya tumeuwana atakayeliliwa zaidi achukue
mke....wakafyatua risasi mke akaja mbio akipiga
kelele na kukuta wanaume wamelala chini......akaanza kucheka na kurudi chumbani
MKE: Mpenzi wangu
toka huko uvunguni wale mafala wamejipiga risasi wamekufa wote..!!