DOKEZO Jamani jamani kunguni ndani ya MV Victoria zitatuua

DOKEZO Jamani jamani kunguni ndani ya MV Victoria zitatuua

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Screenshot_2022-11-08-08-59-58-00_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg
 
Kwani mawaziri na manaibu wao wana kazi gani? Si ndiyo hizi za kushughulika na kunguni.
UKo serious au utani tuu? yaani swala la uchafu kwenye meli waziri awasaidie? meneja wa MV victoria na wasaidizi wake vipi? kuna wakurugenzi wa shirika linalomiliki hiyo meli wanaweza kumwajibisha huyo meneja wa MV victoria naona tuanzie hapo
 
Hata wafanyeje hawawezi , kunguni wakiingia hawana dawa , solutions ni dawa + abandon , kitu ambacho ni impossible mana meli lazima ipige kazi , lazima mazalia yataendelea kuwepo
Hii sio kweli boss, kuna dawa za kuua kunguni 100%
 
Kuna watu wapo kwenye nafasi ambao hawastahili kuwepo, hiyo meli kuna uongozi unaotakiwa kuitazama lakini hawana habari.

Hata meli ya kutoka Pemba kwenda Tanga nayo tatizo ni hilo hilo, kunguni, hawa jamaa nauli wanazochukia kwa abiria sijui huwa wanazifanyia kitu gani.
 
Hivi meli zetu zipo chini yq TEMESA au bodi gani inazisimamia?
Wakaguzi wafutwe kazi
Wahudumu wapewe ngalawa wakavue samaki
Serikali iajiri watu wanaojua wajibu wao
MSCL=Marine Services Company limited. Kamouni ya Huduma za Meli
 
MSCL=Marine Services Company limited. Kamouni ya Huduma za Meli
Ukifuatilia kwa undani utakuta kuna upigaji wa pesa za ukarabati na usafi.

Msimamizi wa meli hiyo anapaswa kuwajibika. Meli haisafirishi bure abiria na mizigo, wanashindwa kuihudumia na itakuja kuchakaa soon
 
Kabisa. Na bei zao zimechangamka sana.
 
Kabisa. Na bei zao zimechangamka sana.
Hiyo hali ya Mv Vicky kukosa matunzo ni sawa na vile vivuko pale fery ya Dar.

Sasa hivi vinatembea viuno vimepinda. Vikija kupiga sarakasi wale wavuvi pale watageuka mashujaa wa uokoaji
 
Hiyo hali ya Mv Vicky kukosa matunzo ni sawa na vile vivuko pale fery ya Dar.

Sasa hivi vinatembea viuno vimepinda. Vikija kupiga sarakasi wale wavuvi pale watageuka mashujaa wa uokoaji
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣. Sijui tutajifunza lini kuwa serious.
 
Mara ya kwanza nilipoandika uzi kuhusu kunguni katika meli yetu pendwa ya MV Victoria, ulifutwa mara moja.

Naomba admin mjue sisi abiria ndo tunaumia. Wingi wa kunguni hata Jela haifui dafu. Jamani wahusika tusaidieni. Najua mnamtafutia mama lawama, lakini kwa hili hahusiki.

Meli imekuwa mazalio ya kunguni na viroboto. Sasa abiria tunajiuliza, ni uzembe au ni ile tu watu kuwa irresponsible? Wahusika, waziri wetu wa uchukuzi, ingilia hili jambo.
hili swala kunguni sio huko kanda ya ziwa tu hata huku kwenye boat kadhaa upande wa pwani swala la kunguni bado lipo na ni mtihani mkubwa tu
 
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣. Sijui tutajifunza lini kuwa serious.
Tangu MV Bukoba ilipoua wapendwa wetu, tulichojifunza ni kujikita kwenye kukamata Dola dhidi ya wananchi ndo maana hao wapinzani wanapotaka kufanya mikutano yao halali kisheria wanaambiwa hakuna ulinzi lakini wakikusanyika wanapelekewa idadi kubwa ya walinzi wa kuwapiga.

Hatutqweza kujifunza chochote nje ya Katiba Mpya. Amejisemea sifi leo kuwa bila katiba mpya tutaendelea na misiba ya ndugu zetu kwa uzembe wa wahusika
 
Back
Top Bottom