Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 1,679
- 2,123
Kila siku wifi anaamka alfajiri, anakuchemshia maji ya kuoga. Anafanya usafi wa nyumba, anapika chai, anaogesha watoto. Anaenda kutafuta mkaa, anahakikisha familia imepata chakula.
Sokoni anakazana—anauza maandazi ili watoto wapate ada ya shule maana wewe huwalipii. Jioni inamkuta bado kwenye mishe mishe. Anarudi nyumbani hoi, jua limempiga kutwa nzima. Anaandaa tena chakula cha usiku.
Loo, kaka. Mbona unajiona mfalme? Unaondoka asubuhi kwenda kazini baada ya kunywa chai aliyokupikia wifi. Ukitoka kazini unaenda unakokujua, unarudi usiku wa manane unanuka pombe, na harufu ya wanawake wengine inakufuata. Bila haya, unampiga wifi makonde na kumshutumu eti amechelewa kukufungulia geti. Badala ya kumshukuru amekesha akisubiri urudi, unatishia kumtimua na kumpa talaka.
Anakukaribisha chakula mezani, unakataa kula, eti chakula kibichi wakati hata huonji. Wifi yangu mvumilivu, anakuandalia tena maji ya kuoga. Anakuhudumia kwa heshima unalala fofofo.
Wifi yangu anateseka, siku nyingine analala njaa na watoto, wakati wewe unakula vinono hotelini na hao malaya. Unasahau wifi ndiye anayekufulia nguo, ukienda kazini unaonekana "smart"
Kaka, mara hii umesahau? Wifi yangu alikuvumilia wakati huna pesa. Ni yeye aliyekufuta machozi ulipofukuzwa kazi. Sasa umepata kazi mpya, shukrani yako imekuwa mateke?
Kaka, usisahau: ulikaa ndani ya tumbo la mama miezi 9. Ulinyonya maziwa ya mama. Ulilelewa kwa mikono ya mama. Mheshimu mke wako, yeye naye ni mama.
Kaka, nakuheshimu, lakini nakuambia ukweli: Unayoyafanya, Mungu anakuona. Kilio cha wifi yangu, Mungu anakisikia. Machozi ya wifi yangu, Mungu anayaona. Naomba ubadilike, usisubiri Mungu alipize kisasi.
"Enyi waume, wapendeni wake zenu." (Waefeso 5:25)
==================
Tunaadhimisha siku ya Wanawake Duniani.
Tunakumbushana thamani ya Mwanamke.