Jamani kuna utajiri mkubwa wa dhahabu kwenye claim yangu

kwani gram 1 ni kiasi gani sokoni?

Inategemea uko wapi na ni dhahabu ipi, kuna vikole huko chunya ambavyo vina fetch kati ya 52,000 mpaka 54,000 chunya, vikifika Mbeya 56,000 mpaka 58,000, vikifika Dar 58,000 mpaka 64,000.

Hizi za kusaga na kuunga unga, zina range kama hapo juu less 4,000 per gram.
 

Wewe ni punguani kweli kweli, huyo mtu anataka excavator, excavator si yangu, nikimuunganisha nikapata Million yangu ya halali kama commission, nina shkuru AlhamduliLllah.

CCM inahusu nini hapa? nenda kachimbe dhahabu Chunya, nenda ukaone huko kuna chuo kimeanzishwa na Serikali ya CCM kwa wachimbaji wadogo, nenda kaone Watanzania wenzako wanavyochangamkia fursa.

Wewe umebaki kulalama tu humu, huna mbele huna nyuma na wala fursa huzioni na hautoziona.
 
Mgodi si wake kwani wangu? Million moja unaiona ndogo? labda mwenzetu billionaire wa Arusha.

Acha ubishi mama angu, kuzungumzia milioni moja kwenye dhahabu ni aibu. au ndio maana muheshimiwa aliomba suti. ndo bei zenu hizo sio?
 

Tanzania biashara ni very slow, kitu cha kusema OK au NO, atataka tuandikiane PM tutungiane mashairi, tupatane, sijui hiki kile, its all BS. Ni either YES or NO.

Nenda Dubai ukaone hata madukani hawana time, anakupa bei ukianza kupatana sana anakuacha anashughulika na wateja wengine, si unaona wanavyokuwa kwa haraka. Time is money.
 
Acha ubishi mama angu, kuzungumzia milioni moja kwenye dhahabu ni aibu. au ndio maana muheshimiwa aliomba suti. ndo bei zenu hizo sio?

Wewe ni punguani hapo tunazungumzia anataka excavator, mimi najuwa wapi atalipata na picha nimemuwekea, sitaki zaidi kutoka kwake nataka million 1 tu. Mkwanja wangu mwingine nachukuwa kwa muuzaji, yeye ndiye anaepokea pesa, huyo anachukuwa excavator tu.

Mwache akafanye kazi atengeneze pesa, mimi dhahabu zake sina shida nazo. AlhamduliLllah, nilizonanzo zinatosha na nnajuwa wapi pakuzipata. Si kama wewe limbukeni wa pesa.
 
Aisee, hizi terms za makubaliano umezifikiaje? Chunga sana mkataba utakaoingia nao.

Natamani nikuelezeke kwa consultant, ila sijui kama unaona umuhimu huo.
nielekeze tu halafu mimi nitapima mawazo yako, maana kuna watu wengine wametuambia tufungue kampuni, harafu tuombe mkopo benki, ndiyo tununue, kwa hiyo kuna mawazo mengi tu ambayo tumeyapata.
 

Wewe umeshindwa kuona fursa kwa huyo jamaa alafu unakuja kunifundisha mimi mambo ya fursa? na hao wachimbaji wadogo mnawafundisha nini tena wakati tayari ni wachimbaji? au mnataka mje muuze machimbo yao kwa ahadi ya kuwapa ajira kutoka kwa wawekezaji wakubwa?

alafu usitake kumtapeli huyo jamaa, hii nchi hakuna excavator isiyo na kazi kiasi cha kuchuuzwa kwa milioni moja.
 
kama hutajali niunganishe naye, nitakupa hata 2m mradi tufikie makubaliano mazuri, lakini pia nitakupa tender ya kuweka mgahawa kule site na mambo mengine mazuri nitakayoona yanafaa.

Piga simu hiyo niliyokurushia kwenye PM, mwambie huyo mama unapiga kuhusu excavator, kazi kwako. Nnaamini mtaafikiana na nnangoja commission yangu kama ulivyoahidi, ukinizika nnahakikisha hulali kwa raha maisha yako. NNajuwa mgodi wako uko wapi na nnakujuwa wewe ni nani. Usitake kujuwa najuwaje.
 

Kwa mikwara sasa.
 
sasa mkuu, MAMBO SI HAYO, NAKUOMBA MKUU WANGU USOME VIZURI KWA UMAKINI MAELEZO YANGU, MIMI NAKUOMBEA KWA MUNGU ILI UWEZE KUELEWA VIZURI MAELEZO HAYO NA USEME NENO MOJA TU NA ROHO YANGU ITAPONA.

Usijali, chukulia kuwa mambo yako yameshafanikiwa. Ukimaliza kuongea na simu niliyokurushia, nijulishe.
 
We acha uongo wewe, kipimo cha dhahabu ni ounce, ounce moja ni sawa na gram 28.35, ounce moja kwa sasa haivuki dola 1,700. maana ake gram moja haiwezi kwenda kwa hiyo bei.

mkuu unachobisha ni nini na unachoandika ni kipi?

if 1 ounce = 28.3gm
and 1 ounce =1700usd

1700/28.3=60usd

1usd=tsh1640
60usdx1640= tsh 98500/=

actually wewe umepata gram 1 ni bei kubwa kuliko bei aliyosema msocrates
 
Last edited by a moderator:
nielekeze tu halafu mimi nitapima mawazo yako, maana kuna watu wengine wametuambia tufungue kampuni, harafu tuombe mkopo benki, ndiyo tununue, kwa hiyo kuna mawazo mengi tu ambayo tumeyapata.

mfuko mmoja unatoa gram 4 mpaka 5, mawe tunasaga kwa kutumia bomeri hayo mengine tutajadiliana tukionana.

wakuu nipeni fursa japo na sie tunuse vipesa vya kubadilisha mboga, nipo dare salaam nimejiajiri
 
Usijali, chukulia kuwa mambo yako yameshafanikiwa. Ukimaliza kuongea na simu niliyokurushia, nijulishe.
ok, NASHUKURU NIMEONGEA NAYE, TUTAKUTANA NAYE BAADAYE KWA AJILI YA KUFANYA MAKUBALIANO, KAMA MAMBO YATAENDA VIZURI UTAFURAHI, MUNGU AKUBARIKI SANA.
 
ok, NASHUKURU NIMEONGEA NAYE, TUTAKUTANA NAYE BAADAYE KWA AJILI YA KUFANYA MAKUBALIANO, KAMA MAMBO YATAENDA VIZURI UTAFURAHI, MUNGU AKUBARIKI SANA.

Chukulia kuwa mambo yako yameshafanikiwa. Nangoja mkwanja wangu ulioniahidi.
 
mkuu unachobisha ni nini na unachoandika ni kipi?

if 1 ounce = 28.3gm
and 1 ounce =1700usd

1700/28.3=60usd

1usd=tsh1640
60usdx1640= tsh 98500/=

actually wewe umepata gram 1 ni bei kubwa kuliko bei aliyosema msocrates

Huyo Sangarara achana nae ni pasua kichwa, hana alijualo zaidi ya kubishana kijinga tu.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…