Heshima kwako Majasho,
Ni kweli CHADEMA wanakinyongo na Bwana Mrema tangu enzi akiwa NCCR mageuzi.Nakumbuka Mwenyekiti wa CHADEMA wakati huo Mzee E Mtei alikuwa akigombea ubunge mjini Arusha kwa tiketi ya CHADEMA alikuwepo pia Bwana Makongoro Nyerere alikuwa akigombea kwa tiketi ya NCCR Mageuzi.
Mzee Mtei alikuwaakifanya kampeni kwa muda mrefu mjini Arusha lakini Makongoro alikuwa akimsaidia kampeni za urais wa Bwana Mrema Tanzania nzima.Makongoro alifanya kampeni mjini Arusha kwa muda usiozidi siku tatu tu na akashinda.CHADEMA hawakumsimamisha mgombea urais walimuunga mkono Bwana Mrema.Bwana Mrema alipokuja Arusha aliwasimamisha Bwana Mtei na Makongoro Nyerere na kuwaachia mtihani wakazi wa Mji wa Arusha wamchague mgombea wanaemka.Mzee Mtei alisononeka sana kitendo cha Bwana Mrema kumsimamisha Makongoro Nyerere na yeye,alitaka asimamishwe pekee yake.Chuki za CHADEMA dhidi ya Bwana Mrema zikaanza hapo,kila analofanya Mrema ni baya,mbaya zaidi chuki hizo zimeendelezwa na mkwe wa Bwana Mtei ambaye ni mwenyekiti wa CHADEMA Bwana Freeman Mbowe na baadhi ya wanachama wa CHADEMA ambao wanataka kuufanya mtandao wa JF ni mali yao.Nimemsikia mwenyewe Mheshimiwa Zitto Kabwe akimsifia Muungwana mara kibao haikuwa nongwa,Mzee wa kujaza watu mapesa kamsifia Muungwana mara kibao hapakuwa na hoja zozote hapa jamvini za kuwatukana kina Zitto na Cheyo ??????.