Miss Chaga, haya maelezo angekua akitoa mhusika moja kwa moja ingependeza saana kwani tungekua na fursa ya kumuuliza maswali mengi ambayo yapo tokana na habari yenyewe.
Nje ya wale ambao wapo kwenye mahusiano; hata kwa wanandoa kiukweli upande wa wanandoa ni wengi hulalamika kuhusu wenza wao kua na kasoro Fulani Fulani zisizovumilika, labda tokana na kuchoka na hizo tabia, yawezekana tokana na kuchoka hizo tabia za wenza wao, or tokana na kutaka sympathy toka kwako kama rafiki yake, au tu pengine anakutega kuona wewe una msimamo upi tokana na mahusiano yao hayo au tu kuna mwingine raha yake ni kulalamika. Malalamiko hayo hayana maana kabisa kuwa anafikiria sasa ndiyo huyo mtu wake hafai na wala haimaanishi kuwa atataka kumuacha.
Miaka mitano ni mingi sana kwa wapenzi for katika standard ya kawaida kuna wengine walioana na waliachana tokana na kushindwana (hata kama waliolewa). Inawezekana hii story ni kweli; nashindwa kuelewa kabisa kwa mtu ambae anapenda faragha kavumilia vipi kwa miaka mitano kama haridhiki na hawajaoana, na ni vipi kashindwa kabisa kumfundisha mwenzie ni wapi/vipi anataka kukunwa.
Whether tumshauri huyo mwenzio kumuacha au kuendelea na huyo mtu ni lazima tujue haya;
- Hafikishwi kabisa kileleni na mtu wake wakiwa faragha?
- Kipata cha huyo kaka ni cha chini ama sustainable?
- Ni lini kaona kuendelea kua nae ni tatizo?
- Anampenda mtu wake?
- Rafikiyo ana umri gani?
Niongeze pia kauli za "Pesa huna" hazijengi… Si nzuri. Kama huyo mtu kaonekana hafai kwa kutokua na pesa hata kama kakupenda na kukuthamini; walau mpe heshima yake ya yeye kukuona bora na kukuchagua wewe kua another half katika maisha yake (of all the people angeweza kuchagua).
All in all, mshauri huyo dada atafakari. Kama kweli hamtaki asizidi kupoteza mda wake na kumpotezea mda huyo mwenzie.