Jamani mimba yangu, msaada

Status
Not open for further replies.

watetea haki za binaadamu na akina mama, mko wapiiiiiiii
Mimi siwezi kwenda polisi, sababu simfahamu huyu dada, lakini kama kunatatizo, walah nakuambia, baba wa mtoto hawezi kukuelewa mkuu.
Wewe umeona wapi Polisi akaogopa Polisi Mwenzake? umeona wapi wewe kesi ya paka na panya utampelekea mbwa? chezea MziziMkavu wewe utakuwa umekalia kuti kavu wewe utadondoka chini. Unaonaje umsaidie huyo bibie aende kunishitaki Polisi? Itakuwa vizuri zaidi unasemaje?
 

Mkuu, tumuombee kwanza huyu dada awe salama, na huyo dogo aendelee kukua huko tumboni.
 
Hakuna cha kumlaumu MziziMkavu kwa kuwa yeye husaidia kuweka masuala mengi ya afya na remedies nyingi. Kinachotakiwa kama una tatizo wasiliana na MziziMkavu privately akushauri. Kwa mfano mjamzito na anayenyonyosha kitu chochote cha tiba ni lazima umshirikishe dr kabla ya kula au kumeza. Anayefikiri Dr. MzimziMkavu alikosea kuweka huduma zake hapa JF bila hata malipo hana budi kukaa kimya milele.
 
DR, Ultrasound ndio kipimo kinachoweza kudetect kama mimba imeharibika au la? za siku lakini?

Yes, kwa mimba ya umri kama alioutaja wa miezi mitatu yaani wiki 12 ultrasound inatosha.

Nashukuru Mungu mi mzima. Ile ishu yako I hope iliisha salama.
 
Yes, kwa mimba ya umri kama alioutaja wa miezi mitatu yaani wiki 12 ultrasound inatosha.

Nashukuru Mungu mi mzima. Ile ishu yako I hope iliisha salama.

Mi niko fresh, ile imenitoa barabarani financially. ndo maana nawachukia ma-ccm zaidi na zaidi mkuu, ufahamu wa binaadamu kwenye maswala ya tiba ni mpana sana, lakini wanashindwa kucopy na kupest tu bwana.
 

Asante mkuu Zogwale kwa majibu yako mazuri imekuwa kosa kwangu kuwapa ushauri watu bure bila ya malipo.

Ninashangaa huyu bibie.@kukucd kunilaumu kuwa ameona Thread yangu inayohusu Faida ya kitunguu Saumu

akaamuwa kukitumia hicho kitunguu Saumu bila ya kutaka ushauri wangu. Amepatwa na Madhara kwa sababu ya

hiyo mimba yake changa anakuja tena humu ndani na kuweka Thread ya kunilaumu mimi nimemkosea kitu gani

jamani? Na huyu mkuu.@
Sangarara Ameniamkia mimi leo asante sana.
 
Pole na yaliyokukuta natumaini upo salamq na mtoto pia.

Ukiwa una mimba mtu ni lazima kujiangalia na kuyomeaa madawa au kunywa vitu ovyo. Kama hauna wa kuulizq haya google ukiweka pregnancy na neno lingine lazima uyapata info.

Cha kufanyiwa ni inabidi kuingizwa mkono/vidole wacheki kama womb imefunga bado.

Ultrasound wataona kama kuna heartbeat na kama mimba ipo sehemu yaani haijashuka chini.

Pole kwa unalopitia ila omba wakucheki hayo ni muhimu kujua womb imefunga bado na heartbeat ipo na rate inayotakiwa.

Natumaini iwe ni umetoka damu tu tishio la mimba kutoka. Pole sana. Na dawa za maumivu only panadol ndio inakubalika kama zingine ni ukipewa na daktari sizizo haribu mimba. Hata za bp zipo za wakayi wa mimba.
 
Mkuu, tumuombee kwanza huyu dada awe salama, na huyo dogo aendelee kukua huko tumboni.
kwa kuwa hajajibu baya mpaka sasa mimi nitamuombea kwa Mwenyeezi Mungu atamlinda na kuitunza mimba yake apate mtoto mwema hapo ndipo ulipotakiwa kusema sio tangu mwanzo ulikuwa unazungumza maneno ya Pumba. Ewe Mwenyeezi Mungu uliye pekee mlinde na mponyeshe mja wako.@kukuc Kama alivyokuwa anawaombea kuponya wagonjwa bwana Yesu Wafuasi wake Ameen.
 
Sangarara
MziziMkavu akitoa ya dawa hana hatia juu ya mtu aliyemfata aliyoandika. Huuo dada ilibidi aulize kama kweli alijua kuwa mimba ni kitu cha kuangaliwa kwa umakini au ange google.

Wengi wakati wa mimba hata simu tunapigianq na watu na ndugu kuuliza maswalo hata ya vitu kamq pain, symptons za ajabu tunajifunza.

Huyu dada anatatizo akasoma akafata ushauri au womo bila kutafakari sababu wengi hawajui mimba ni aq kutunzwa kama yai na inategemea na mtu na mpango wa Mungu na mwili wako.

Umekurupuka na unaonekana unapenda matatizo yawapate wengine sababu weye yako yamejaa hujui la kufanya.
 
Last edited by a moderator:
Kwa maoni yangu Dr MziziMkavu huna kosa lolote hii dawa ambayo uliizungumzia haikuhusiana na wajawazito. Kilichobaki ni kumuombea mwenzetu ili ujauzito wake usiharibike na hili liwe fundisho kwa wanachama wote hapa kutotumia dawa waliyoifahamu kupitia JF au mtandao mwingine kupata ushauri wa kina kabla ya kuanza kutumia dawa hiyo/hizo.
 
Last edited by a moderator:
Wahi kwa mtaalamu bila kusimama ki2o chochote we
 

Usihofu sana, kama huna maumivu yoyote hiyo inaweza kuwa fungus zilizokubuhu(chronic candidiasis). Nenda hospitali fasta, onana na gynae ikiwezekana instead of daktari wa kawaida(GP)
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo wewe umeona matatizo yangu tu? huyu dada hauoni kama na yeye yuko kwenye matatizo?
 
Dx. Abortion . Umefanya abortion acha kujisafisha. Tunakusubir hapa Muhimbili tukunyooshe.

DR Hemu saidia, ethics na codes of conduct zenu zinasemaje? Daktari hawezi kushitakiwa kama ushauri au maelekezo yake yatamdhuru mgonjwa?
 
Mkuu, sheria zinasemaje lakini?
 
Hamna cha sheria wala nini, unakurupuka tu. Hebu nyamaza doubt kidogo ya hekima yako ibakie.

kila kona hospitalini kumeandikwa 'advice your dr if you suspect/know you are pregnant'. Kuna dawa hata za kupaka kama cream, na vidonge ambavyo huruhusiwi kutumia kama ni mjamzito. Na ukimuambia dr unahisi ujauzito utapimwa kwanza kama hakuna alternative.

wasishatkiwe wanaotapeli watu kutibu ukimwi, hadi watu wanaacha dawa na kuja kuongeza mzigo wa matibabu baadae! Akashtakiwe MziziMkavu kwa kushauri kutumia vitunguu swaumu? Tuondokee hapa bush lawyer!
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…