Jamani mimi mwenzenu,naanzaje kuipenda serikali yake na mauwaji yote yale?

Jamani mimi mwenzenu,naanzaje kuipenda serikali yake na mauwaji yote yale?

mkulimamiwa

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2025
Posts
2,591
Reaction score
5,315
Ndugu zangu, mnifundishe mwenzenu, Naanzaje kumpenda mtu aliyeruhusu mauwaji ya kikatili kiasi kile?

Nimepoteza ndugu zangu wanne katika tukio la maandamano ya 29 October 2015 ya kupinga uchaguzi usio na usawa kwa vyama vilivyopo hususani vya upinzani

Mgawanyiko uliopo kati ya walioumizwa na matukio ya mauwaji na wanaounga mkono upotezwaji wa Roho zile huku wakitulazimisha kuipende serikali yao, nadhani hii ni sawa na matusi mengine kwa tuliopoteza roho za wapendwa zetu

Nyinyi ambao hamjaumizwa wala hamjapoteza ndugu zenu mtoshe nyinyi kushangilia wauwaji wenu

Miaka yote atakayohudumu huyo mtu wenu, mimi stamuunga mkono kwa lolote lile
 
Back
Top Bottom