Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,817
Habari zenu wanajamii forum
Ngoja na mm leo niombe ushauri.Kuna binti mmoja nipo naye kwenye mahusiano kuanzia 2013 yeye yupo Dar na mm nipo mkoa moja kaskazini mwa Tanzania.Sasa tatizo langu huyu binti hayupo kabisa moyoni mwangu japokuwa yeye anaonyesaha ananipenda sana mpaka anajua kwamba nitamuoa lakini niseme ukweli mimi hayupo kabisa moyoni mwangu japokuwa namfahamu hadi mama yake mzazi na yeye ameweka karibu asilimia 90 anajua mm ni mtu wake,lakini moyo wangu unakataa jamani kwani nilikuwa namtamani tu,lakini yeye ananiambia ananisubiri nimalize ishu zangu za kutafuta maisha.Kiukweli anajali lakini tatizo moyo wangu unakataa maana mwili unamtamani lakini akili inakataa kuwa mwenza wangu wa maisha.Jamani moyo wa mtu ni kiza kinene.Naombeni ushauri nifanyeje ili nimpoteze mawazo yake ya kuishi na mimi japo nataka aishi na mimi kama rafiki yangu ila sio mke wangu.
Nawasilisha
Wewe huwajui Wanawake, hata yeye ni hivyo hivyo kama unavyofikiria wewe, sema tofauti tu ni kwamba wewe ni mjinga na unafikiri anakupenda kweli, tena siajabu hata huyo mama yake ameshaongea naye na kwamba anakuhitaji tu kwa jambo fulani!
Mwanamke hampendi Mwanaume na wala hajawahi kumpenda Mwanaume hata siku moja, Mwanamke ana maslahi tu ambayo anakurubuni kama mapenzi lkn kiukweli kabisa Mwanamke anampenda mtoto wake tu!