Jamani moyo kwanini unamkataa huyu?

Jamani moyo kwanini unamkataa huyu?

Habari zenu wanajamii forum
Ngoja na mm leo niombe ushauri.Kuna binti mmoja nipo naye kwenye mahusiano kuanzia 2013 yeye yupo Dar na mm nipo mkoa moja kaskazini mwa Tanzania.Sasa tatizo langu huyu binti hayupo kabisa moyoni mwangu japokuwa yeye anaonyesaha ananipenda sana mpaka anajua kwamba nitamuoa lakini niseme ukweli mimi hayupo kabisa moyoni mwangu japokuwa namfahamu hadi mama yake mzazi na yeye ameweka karibu asilimia 90 anajua mm ni mtu wake,lakini moyo wangu unakataa jamani kwani nilikuwa namtamani tu,lakini yeye ananiambia ananisubiri nimalize ishu zangu za kutafuta maisha.Kiukweli anajali lakini tatizo moyo wangu unakataa maana mwili unamtamani lakini akili inakataa kuwa mwenza wangu wa maisha.Jamani moyo wa mtu ni kiza kinene.Naombeni ushauri nifanyeje ili nimpoteze mawazo yake ya kuishi na mimi japo nataka aishi na mimi kama rafiki yangu ila sio mke wangu.
Nawasilisha

Wewe huwajui Wanawake, hata yeye ni hivyo hivyo kama unavyofikiria wewe, sema tofauti tu ni kwamba wewe ni mjinga na unafikiri anakupenda kweli, tena siajabu hata huyo mama yake ameshaongea naye na kwamba anakuhitaji tu kwa jambo fulani!
Mwanamke hampendi Mwanaume na wala hajawahi kumpenda Mwanaume hata siku moja, Mwanamke ana maslahi tu ambayo anakurubuni kama mapenzi lkn kiukweli kabisa Mwanamke anampenda mtoto wake tu!
 
achana na moyo tumia akili.. moyo mdanganyifu utakuja kupata wa kumoyo akili ikashindwa kufanya kazi
 
Wewe huwajui Wanawake, hata yeye ni hivyo hivyo kama unavyofikiria wewe, sema tofauti tu ni kwamba wewe ni mjinga na unafikiri anakupenda kweli, tena siajabu hata huyo mama yake ameshaongea naye na kwamba anakuhitaji tu kwa jambo fulani!
Mwanamke hampendi Mwanaume na wala hajawahi kumpenda Mwanaume hata siku moja, Mwanamke ana maslahi tu ambayo anakurubuni kama mapenzi lkn kiukweli kabisa Mwanamke anampenda mtoto wake tu!
Ha ha ha kama na yeye hanipendi kama mm mbona nitafurahi japo sina uhakika sana kama mwanamke hajawahi kumpenda mwanaume
 
Ha ha ha kama na yeye hanipendi kama mm mbona nitafurahi japo sina uhakika sana kama mwanamke hajawahi kumpenda mwanaume

Ndiyo hivyo kama ulikuwa haufahamu ndiyo ufahamu Mwanamke anafwata maslahi tu kwa Mwanaume lkn kamwe hawezi kukupenda na ndiyo maana utasikia kila siku vilio hapa JF sijui nilimsomesha akanimwaga, mara nilimpa kila kitu lkn kanikimbia wengi hawatambui ukweli kwamba Mwanamke hampendi Mwanaume bali Mwanamke anamtumia Mwanume kupata anachokihitaji inaweza kuwa chochote kile aidha mtoto, maisha mazuri, umsaidie afaulu mtihani wake, umsaidie kupata kazi, umpe sex nzuri n.k. lkn siyo kukupenda hilo sahau na kama haumini endelea kutafuta mapenzi kutoka kwa Mwanamke siku moja utakuja kuelewa kwamba Mwanamke kamwe hampendi Mwanaume bali anapenda mtoto wake tu!
 
kawaida bro hata ww naamini ushawahi ku date na mtu ambaye unamtamani sio kumpenda
Sio nimeshawahi, till now i do but not for that long bro. Four years? Kama ulimtamani na hukumpenda kisha ukamtumia mara moja au mbili au miezi mitatu tosha kabisa, sasa wewe miaka minne unasema nitamaa?.
wewe sema umepata mwingine unaempenda kuliko huyo au uliemtamani kuliko huyo.

Kawaida mapenzi yanaaza na tamaa kwanza kisha ukinogewa inakuwa mapenzi, lakini wewe for four years bado ni tamaa tu?
 
Hapo ndipo panapoleta utata,unakopendwa hupendeki na unapopenda hupendwi.....hatariiiii
ila usimuweke mda mrefu zaidi aisee miaka mitatu kama huna future nae mpige chini apate mwingine huku dar wamuoe
 
Imagine utakua na familia, utazaa watoto na watoto wa kike pia kisha binti yako anakuja kufanyiwa upuuzi kama huo!! Si utaua mtu? Please usimfanyie mtu kitu ambacho usingependa ufanyiwe......
 
Imagine utakua na familia, utazaa watoto na watoto wa kike pia kisha binti yako anakuja kufanyiwa upuuzi kama huo!! Si utaua mtu? Please usimfanyie mtu kitu ambacho usingependa ufanyiwe......
Nimekuelewa ndugu,nafsi ndio inayokosa amani mm mwenyewe sipendi ila mtima unakataa
 
"Ole wenu wachungaji wanafiki".

Ni vizuri ukawa mkweli, mwambie ukweli binti wa watu.
 
Nimekuelewa ndugu,nafsi ndio inayokosa amani mm mwenyewe sipendi ila mtima unakataa
Hujakosa amani ila unailizamisha ikose amani, take my word, whether you are kidding or not ila utakuja kumkumbuka huyo binti when it is too late.
 
Wewe huwajui Wanawake, hata yeye ni hivyo hivyo kama unavyofikiria wewe, sema tofauti tu ni kwamba wewe ni mjinga na unafikiri anakupenda kweli, tena siajabu hata huyo mama yake ameshaongea naye na kwamba anakuhitaji tu kwa jambo fulani!
Mwanamke hampendi Mwanaume na wala hajawahi kumpenda Mwanaume hata siku moja, Mwanamke ana maslahi tu ambayo anakurubuni kama mapenzi lkn kiukweli kabisa Mwanamke anampenda mtoto wake tu!
mmmmmhhh acha uongo hamna ukweli wako wanawake wanaopenda kweli au wewe muhanga wa hayo.
 
Kuna wimbo wa zamani sana.... lakini bado unaishi mpaka kesho......
"Usihadaike vile moyo unavyo kutuma...
unadanganya na una kila hila jaribu kuushinda..

Kama hakuna kasoro yoyote kwake ila tu ni kwa vile moyo umemkataa...
Ni bora uishi na mtu anayekupenda kuliko kuishi na mtu unayempenda!
Kupendana ni neno tu lakini kiuhalisia lazima mmoja anamzimikia mwenzie zaidi!
 
aisee noma sana mapenzi haya
 
Back
Top Bottom