Nduna shujaa
Senior Member
- Aug 14, 2022
- 163
- 134
Inasikitisha sana kwakeli yani baadhi ya wachungaji wanawaaminisha wanatibu vvu na kuwafanya watu wanaacha dawa hatimaye kufa. Lakini pia niwape kisa kingine nje na hapo juu.
Kwanza nikiri wapo wachungaji wachache wenye karama ya uponyaji, wengine wapiga dili tu.Kisa cha kweli ila sitataja jina la mhanga wala jina la kanisa ila ni kanisa la kilokole pale songea tanga mwenye jina linalofanana na chaji.Wagonjwa wengi waendao kwa mara ya kwanza wanaagizwa wabebe 30000.
Halafu baada ya kukaa naye mezani na kuona tatizo la mhusika akamwambia wewe na mwenzako leteni 200000 wakatowa wale waumini wagonjwa akawa anawaombea mwezi mzima wakiwa wanakaa hapo eneo la ibada hawakupona hatimaye wakaaga kuondoka.
Mchungaji akawambia ataenda nyumbani kwao kutoa madudu yaliyopo pale nyumbani,wahusika walipofika nyumbani wakampigia unakuja lini mchungaji akawambia tuma ela ya mafuta ya gari ikatumwa 50000.Sasa toka hapo walipotuma wakimkumbusha aende anawapa kalenda mwisho wa siku anakuwa mkali na kusema hawezi kwenda kwajili yao labda wao wagonjwa waumini waende tena kanisani.
Wachungaji wa namna hii wanawaharibia cv wenzao na kujipatia kipato na si huduma.Ifike wakati serikali iyachunguze makanisa yote yanayomilikiwa na watu binafsi kuanzia kiutendaji na akaunti zao ili walipe kodi.