gfsonwin
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 18,272
- 20,692
Kuku dume kwanza pole sana, halafu naomba nikwambie haya kama ushauri tu japo kuwa siyo lazima yawe applied mia kwa mia.
Kwa umri wako wa miaka 22 bado ni kijana mdogo sana, kiukweli sikushauri hata kidogo uingie kwenye maswala ya ndoa ukiwa that much young. Yapo mambo mengi sana ambayo hutoweza kuyamudu kimaisha kwani ndoa ni zaid ya kuwa na mke na kulala naye.
Mama yako napata picha ni mchaga tena ambaye bado yuko migombani anachuma kahawa na kupalilia migomba kama kawaida ya wazazi wetu. Yaelekea wewe ni mzaliwa wake wa kwanza tena wakiume, kwa mtazamo wake kama baba hayupo(amefariki. hapa nitakuomba unisamehe kama nitakuwa nimekuwa tofauti na mod please usinipe ban), basi yeye atawaza wewe uoe ili uwe na mke na watoto akijua kuwa mkamwana atakwenda kukaa naye pale home alime, na kulisha ng'ombe ili kuongeza mali home na siku wewe ukienda likizo ukute maendeleo makubwa. Hapa anaangalia zaid uwezo wa kupata cheap labour akasahau kabisa kuwa siku hizi hakuna wachaga wanao acha wake zao huko moshi wakichuma kahawa halafu wao wakaja mjini. Kwahili naona wala huna haja ya kumwambia mtu yeyote yule zaid ya hapa jf ambao hatukujui.
usitake mambo haya ya familia yenu yawe hadharani kwa watu bwana, ushauri wangu kwako likizo nenda home, kisha mwambie mama kuwa umepata mchumba lakini kwa sasa yuko masomini hivyo unamsubiri amalize shule kwa hiyo akuvumilie kwanza. kwa desturi ya akina mama wa kichaga ya kupenda kuja harusini watambulishwe ukumbuni kama wazazi wa bwana harusi huku akiwa amesindikizwa na rafiki na ndugu huwa yaani anaona fahari sana na usikute hili ndilo linalomsukuma zaid moyoni. sasa mwambie akupe muda uipange na usubirie mwenzi wako amalize chuo. pia mweleze ajue kuwa wewe unatakiwa uwe na life yako hivyo akupe nafasi ujipange vizuri.
kamwe usimweleze kwa ukali, wala usimwonyeshe kuwa mawazo yake yamepitwa na wakati. ukitaka kumfuraisha zaid mweleze bayana kuwa unampenda sana na unatamani uoe ili umletee mkamwana wawe wanavaa vitenge sare. mpambe kwa maneno matamu ili akuelewe bwana.
kuhusu binam yako kamwe usimwendekeze, huyo mpe kubwa kuwa hutaki mawasiliano naye hasa ya kimapenzi kwani hana mvuto kwako. usimwogope na kamwe usikae nae karibu kwenye unywaji asije akakufanya ukaingia dhambini naye. Otherwisw soma sana