Mussa Mussa
Senior Member
- Jan 10, 2012
- 138
- 42
Wana JF leo nimejaribu kuangalia taarifa ya habari kupitia TBC lengo lilikuwa ni kuona Je watazingumzia kesi ya lwakatare hasa baada ya kufutiwa mashtaka ya ugaidi. Kweli sijaamini kilichotokea hawajatangaza kabisa kama hawakuwepo mahakamani hapo. Nina uhakika Lwakatare asingefutiwa mashataka hayo wangeitangaza kwa mbwembwe sana. Ninaomba wakumbuke kuwa watahukumiwa kwa wanayofanya kwani hiki ni chombo cha umma si cha CCM. Pia naomba msiniponde kuwa huwanaangalia TBC nimeangalia leo tu nikiwa naangalia zotezote ili nihakikishe kuwa TBC hawapo objective. Ninaapa mbele ya dunia hii nitaangalia TBC kipindi cha bunge tu! Na wakifuta kurusha LIVE bunge basi nitatamani niifute kabisa katika list ya channel za kuangalia kwenye king'amuzi changu. Bora uangalie taarabu kuliko kuangalia taarifa ya habari TBC. TBC NI TV YA CCM.