Jamani TBC leo hawakuwepo kabisa mahakamani kwenye kesi ya Lwakatare

Mussa Mussa

Senior Member
Joined
Jan 10, 2012
Posts
138
Reaction score
42
Wana JF leo nimejaribu kuangalia taarifa ya habari kupitia TBC lengo lilikuwa ni kuona Je watazingumzia kesi ya lwakatare hasa baada ya kufutiwa mashtaka ya ugaidi. Kweli sijaamini kilichotokea hawajatangaza kabisa kama hawakuwepo mahakamani hapo. Nina uhakika Lwakatare asingefutiwa mashataka hayo wangeitangaza kwa mbwembwe sana. Ninaomba wakumbuke kuwa watahukumiwa kwa wanayofanya kwani hiki ni chombo cha umma si cha CCM. Pia naomba msiniponde kuwa huwanaangalia TBC nimeangalia leo tu nikiwa naangalia zotezote ili nihakikishe kuwa TBC hawapo objective. Ninaapa mbele ya dunia hii nitaangalia TBC kipindi cha bunge tu! Na wakifuta kurusha LIVE bunge basi nitatamani niifute kabisa katika list ya channel za kuangalia kwenye king'amuzi changu. Bora uangalie taarabu kuliko kuangalia taarifa ya habari TBC. TBC NI TV YA CCM.
 
Hata kama walikuwepo, Mshana hawezi kuruhudu editor aweke news ya anguko la Chama chake. Hii ni TV ya Chama si ya Taifa, hilo jina inabidi libadilishwe.Halafu inakufa kifo cha taratibu!!!!
 
hivi kuna watu bado wanagalia taarifa za habari Tbc?
TV ya taifa imebaki ITV baada ya star tv kujiunga na tbccm!
 
Kwa ruhusa ya Mwigulu watangaze?
 
mbona thread yako haieleweki!
upuuzi mtupu.
 
TBC haina uwezo wa kukamata habari zinazohusu chadema kwa mazuri.
Inaweza kunasa mabaya tu
 
Wana JF leo nimejaribu kuangalia taarifa ya habari kupitia TBC lengo lilikuwa ni kuona Je watazingumzia kesi ya lwakatare hasa baada ya kufutiwa mashtaka ya ugaidi. Kweli sijaamini kilichotokea hawajatangaza kabisa kama hawakuwepo mahakamani hapo. Nina uhakika Lwakatare asingefutiwa mashataka hayo wangeitangaza kwa mbwembwe sana. Ninaomba wakumbuke kuwa watahukumiwa kwa wanayofanya kwani hiki ni chombo cha umma si cha CCM. Pia naomba msiniponde kuwa huwanaangalia TBC nimeangalia leo tu nikiwa naangalia zotezote ili nihakikishe kuwa TBC hawapo objective. Ninaapa mbele ya dunia hii nitaangalia TBC kipindi cha bunge tu! Na wakifuta kurusha LIVE bunge basi nitatamani niifute kabisa katika list ya channel za kuangalia kwenye king'amuzi changu. Bora uangalie taarabu kuliko kuangalia taarifa ya habari TBC. TBC NI TV YA CCM.

mkuu hivi unafikiri barcelona tv wanaweza kuonyesha vile vipigo vya bayern?wanachotakiwa kujua ukizoea vya kuchinja vya kunyonga pia vinausika
 
Wanini hao? Wafe tu, hata wasiwepo mahakamani wala wasiripoti lolote sisi tutasonga mbele tu!!!!!
 
wale watu wa kasulu zile radi za sh 20 si bado zipo?
hebu tumeni radi fasta kwenye vimtambo vyao sioni faida yake
tunakatwa kodi zetu kwa ajili ya kutunisha chombo cha CCM
haina faidia.
kama tv ni ya serikali inashabikia chama tawala bora ife kabisa
 
Tbc haiko kwa ajili ya Watanzania. Iko kwa ajili ccm.
 
Back
Top Bottom