Jamani this is serious, nchi tajiri za Kiarabu kuwa ombaomba Afrika by 2030

Jamani this is serious, nchi tajiri za Kiarabu kuwa ombaomba Afrika by 2030

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Magari ya umeme ndio future ya usafiri ilipangwa kwa sasa; hata wanaozalisha magari wengi wao wanaweka 'hybrid systems' ili hayo magari yaweze kutumika hata pale magari yenye sumu ya moshi yatakapopigwa marufuku. Nchi nyingi za Ulaya zitapiga marufuku magari yenye sumu ya ukaa by 2030. Vinu vya nyuklia vya umeme vitaongezeka kwa kasi Ulaya na Marekani, mabwawa ya umeme na wind mills pia (clean energy).

Afrika peke yetu ndio tutabaki kuwa soko la sumu (fossil fuel) toka kwa waarabu hasa Saudi Arabia, hali itakayofanya waarabu kugombea kutuuzia mafuta inexchange for grains na vyakula vya aina nyingine. Katika kulijua hili na kwa kuona kwake mbali Mh. JPM ameshaanza mchakato wa ujenzi wa bwawa kubwa la umeme almaarufu kama Stieglers Gorge litakaloweza kuzalisha MW 6000 at full capacity, ili magari yanayotumia sumu ya ukaa (fossil fuel) yatakapokuwa phased out na magari ya umeme basi Tanzania tutakuwa tunajidai tu; pia Mh. JPM anaendelea na mchakato wa ujenzi wa reli ya SGR ambayo nayo itatumia umeme.

Waarabu wana hali mbaya sana na Dubai wamegundua hatari hii, ndio maana wanabadilisha utegemezi kutoka kwenye mafuta kwenda kwenye utalii, hadi wanajenga visiwa bahari (Palm island). Waarabu literally watakuja kupiga magoti Tanzania in particular wakiomba tuwapatia walau tani milioni kadhaa za nafaka, kwani bwawa la Stiegler's Gorge litawezesha kilimo cha umwagiliaji hivyo kuongeza uzalishaji mara 50 kiasi cha kuweza kulisha Afrika nzima. STIEGLER'S OYEE, pale Sinza watajaa watoto wakali toka uarabuni, itakua ni kujichagulia tu, STIEGLER'S OYEEE, JPM OYEEE!

Bila kusahau kwamba ongezeko la vinu vya nuklia itasababisha uhitaji mkubwa sana wa madini ya URANIUM, hivyo kwakuwa Tanzania ina migodi ya URANIUM kwa wingi sana huko Lindi, basi Wamarekani na wazungu kwa ujumla hawatakua na budi bali kutulamba miguu ili tuweze kuwapatia hiyo URANIUM tuliyonayo na si ajabu kasi ya uchimbaji madini hayo imeongezeka sana huko Lindi, kiasi by 2030 inaweza ikawa imeisha, ningeomba kwa sasa JPM asitishe usafirishaji/utoroshaji wa Uranium hadi pale mustakabali wa suala hili utakapoeleweka ili tuje kuiuza baadae kwa bei ya kuringa na kunata, kuliko hivi sasa wanavyojichotea Uranium kama ya bibi yao vile, hili halikubaliki.

Kipande kidogo tu cha Uranium kinaweza kuzalisha umeme wa kuilisha Marekani kwa miaka hata 10, acheni utani na masikhara kwenye Uranium yetu, tunaijua thamani yake, waTanzania wa sasa tumeelimika!

================================
Update: 26/04/2020

Bei ya pipa la mafuta ghafi nchini Marekani yashuka na kufikia chini ya $0 - JamiiForums
=================================
Update: 10/01/2021


=================================
Update: 22/01/2021
Ndege za umeme mbioni kuzinduliwa



=================================
Update: 11/02/2021
5EBB89AF-C07D-4DB7-8837-973BCAD79A71.jpeg


===========================
Update: 28/07/2023
Kutumia gari la Sumu ya ukaa Lomdon utalipa dollar 30 kwa siku

451EA720-B379-49F2-A42A-DBE5C0F6921D.jpeg


=======================
Update: 20/08/2023
 
Gas asilia ilisemekana kuwa solution ya energy shortage Tanzania, leo hii ni hadithi za alinacha kama kawaida. Sisemi kuwa hiyo Steigler's gorge itashindwa kama gas asilia, ila historia ina tabia mbaya sana, huwa inajirudia.
 
Tuna madini lakini wananchi masikini, gesi wakaja na sound za umeme utakuwa wa bei ya chini lakini bado gharama zipo juu kwa hiyo hata hiyo Uranium sio yetu, unaweza ukakuta kapewa mzungu tokea awamu ya Kikwete. Ila kuhusu soko la mafuta wataalam wanatabiri 2035 waarabu watakuwa na hali mbaya na 2050 ndio watakuwa na hali mbaya kabisa.
 
Hizi ndoto tu Misri yenyewe wanatumia mto Nile kulima na kuuza chakula na kuna mwaka walitukopesha msosi wa msaada. Waarabu walishaplan hizo ishu za kama mafuta yakiwaishia au uzalishaji ukipungua sana. Afrika ndo bara ambalo lina matatizo ya njaa ingawa ardhi inyofaa kwa kilimo ni kubwa kuliko hata idadi ya watu. Serikali zetu bado zipo usingizini
 
Inakuwaje Ethiopia wameweza kutumia maji kuzalisha megawati 40000 za umeme huku sie daily tunapiga mark time na megawati zetu zisizofika hata 10000
 
Dhahabu, Tanzanite na gesi tuliyoambiwa ikifika Dar itakua oyaoya vimetusaidia nini? Wenye akili wakiamua kutumia rasilimali zetu ni simple tu wanazibeba. Siku tukiamua kuwekeza kwenye elimu na kuwafanya watanzania waweze kutumia rasilimali zao hapo tunaweza kuwatisha watu weupe.
 
Inakuwaje ethiopia wameweza kutumia maji kuzalisha megawati 40000 za umeme huku sie daily tunapiga mark time na megawati zetu zisizpfika hta 10000
Sasa kama unalijua hilo kwanini Magufuli anapojisikia uchungu juu ya hilo na kuamua kuanza kujenga bwawa la Stiegler's mnaanza kupiga kelele za mazingira? Ni kweli tumechelewa, ila its never too late, JPM aachwe afanye kazi yake
 
Sasa kama unalijua hilo kwanini Magufuli anapojisikia uchungu juu ya hilo na kuamua kuanza kujenga bwawa la Stiegler's mnaanza kupiga kelele za mazingira? Ni kweli tumechelewa, ila its never too late, JPM aachwe afanye kazi yake
Hujanielewa! Mi concern yangu ni kuwa why 6000 megawati na sio hta 20000 mi naamini baada ya miaka 5.tutahitaji megawati zaidi hizo megawati zitakuwa hazitoshi
 
Hakuna mtambo wowote,unaotumia aina yoyote ya nishati, bila kutumia vilainishi(lubricants,Oil)ili mtambo huo ufanye kazi kwa ufanisi.Na oil ni zao la mafuta yanayotoka ardhini,kwa hiyo ujuwe na ufahamu, bei ya vilainishi itakuwa kubwa kuliko kawaida,hivi sasa vipi vilainishi vina bei kubwa, hasa vyenye ubora wa hali ya juu,na ni wachache wanaomudu kununua.

Mfano mwepesi ni baiskeli,baiskeli bila kilainishi cha grease, hakiwezi kufanyakazi kwa ufanisi, tairi za gari, bila grease hazifanyikazi vizuri, mtambo aina yote bila grease mzunguko haupatikani katika bearings.

Bila vilainishi vyuma vya mitambo vitasagana,na havitafanyakazi vizuri, gearbox za mitambo, bila vilainishi havitafanyakazi vizuri,breki za gari bila oil, hazifanyikazi, sukani zinatumia oil za haidroliki, mitambo ya ujenzi inatumia oil za haidroliki, nk.

Kwa hiyo usijidanganye kama mafuta yatapoteza solo duniani,ndio yatazidi kupanda bei kwa mafuta ghafi. Tuombe Mungu atusaidie, tutaumia zaidi kwa being kuwa kubwa kwa vilainishi,mafuta ya petrol ndio pia yanayotengenezewa gundi za bila aina unaziziona,za kuunganisha mpaka vitu muhimu vya magari mpaka rangi za ukutani na viatu ulivyovyaa.
 
Back
Top Bottom