Hakuna mtambo wowote,unaotumia aina yoyote ya nishati,bila kutumia vilainishi(lubricants,Oil)ili mtambo huo ufanye kazi kwa ufanisi.Na oil ni zao la mafuta yanayotoka ardhini,kwa hiyo ujuwe na ufahamu ,bei ya vilainishi itakuwa kubwa kuliko kawaida,hivi sasa vipi vilainishi vina bei kubwa,hasa vyenye ubora wa hali ya juu,na ni wachache wanaomudu kununua.
Mfano mwepesi ni baiskeli,baiskeli bila kilainishi cha grease,hakiwezi kufanyakazi kwa ufanisi,tairi za gari,bila grease hazifanyikazi vizuri,mtambo aina yote bila grease mzunguko haupatikani katika bearings.Bila vilainishi vyuma vya mitambo vitasagana,na havitafanyakazi vizuri,gearbox za mitambo,bila vilainishi havitafanyakazi vizuri,breki za gari bila oil,hazifanyikazi,sukani zinatumia oil za haidroliki,mitambo ya ujenzi inatumia oil za haidroliki,nk.Kwa hiyo usijidanganye kama mafuta yatapoteza solo duniani,ndio yatazidi kupanda bei kwa mafuta ghafi.Tuombe Mungu atusaidie,tutaumia zaidi kwa being kuwa kubwa kwa vilainishi,mafuta ya petrol ndio pia yanayotengenezewa gundi za bila aina unaziziona,za kuunganisha mpaka vitu muhimu vya magari mpaka rangi za ukutani na viatu ulivyovyaa.