Jamani tumsaidie Athman Idd Chuji

Pengo

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2009
Posts
579
Reaction score
10
Ndugu watanzania wenye nia nzuri na maendeleo ya nchi yetu hususani wapenda soka nawaomba kwa hisani yenu kuweza kumpa mawazo yaliyo mema ili kumrudisha kundini kijana Athmani Idd Chuji mchezaji wa klabu ya Yanga na timu ya Taifa.

Kwa mujibu wa rafikie wa karibu aitwae Alela wa Dodoma,ni kwamba Chuji sasa amekuwa mlevi wa kupindukia kiasi cha kumfanya ashindwe kuhimili mikikimikiki ya mchezo huo uwanjani.

Kwa mujibu wa bwana Alela ambaye ni rafiki wa siku nyingi wa Chuji,licha ya kusoma shule moja Jamhuri pia walichezea timu moja ya Mjimpya SC na Polisi zote za Dodoma,tatizo hilo tayari limefika kwa babake Chuji mzee Idd Athman na mzee kafanya kikao cha pamoja kati ya mwanae(Chuji) pamoja na Ambari Mtoro(mchezaji wa zamani wa CDA) lakini Chuji akakivunja kikao kwa kumwambia babake kuwa yeye hatumii hayo mavitu kwani walishawahi kumwona?Kuona hivyo mzee Idd akasema basi mungu ndiye atakaye kuongoza kama kweli hutaki kuacha hayo maulevi.

Pamoja na Chuji kupata pesa kiasi Fulani pale jangwani hadi leo hana hata kiwanja cha kupakaziwa si DSM wala Dodoma,na akifika Dodoma yeye analala kwenye nyumba ya bababe pale Nkuhungu.

Kwa mujibu wa Alela,kocha wa Yanga(Papic) alimpigia simu baba Chuji na kumweleza hali ya mwanae na kuwa hata kuachwa kwaake timu ya taifa ni kutokana na maulevi hayo,akamwomba wamsaidie kuokoa hali ya Chuji kwani anapoelekea si kwema.

Hivi sasa Chuji akijikuna anatoka vipele huku analalamika eti ni sababu ya mazoezi ya kocha mzungu,amesema Alela.

Ndugu zangu wana jamii tafadharini nawaomba sana tumuokoe huyu kijana kwani wenzie wengi kama Christopher Alex Massawe tayari wamehathirika na hawawezi kurudia hali yao ya kawaida.
 
Haya majungu juzi kati hapa wamepimwa afya wachezaji wote wa Yanga na vipimo vilikuwa safi kwa wote.
 
Duh, Pengo ahsante kwa taarifa. Sasa nimeamini hata Maximo hakuwa anafanya makosa kuwatema Taifa Star. Ngoja nijipange kumwanga ushauri, nitarudi maana nikiamua kutumia udictator wangu haitasaidia hapa.
 
Yanga Daima mbele Daima Haturudi Nyuma! Yanga oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Hivi hata sie wekundu tunaruhusiwa kumshauri?? Nikikumbuka ile ishara ya kidole cha kati....:mad2:...
BTW: Hili jukwaa linahusika na mambo ya kispoti kwani?
 

TOA boriti kwanza kwenye jicho lako ndipo utaona kibanzi kidogo kwenye jicho la mwenzio.
 
Hivi hata sie wekundu tunaruhusiwa kumshauri?? Nikikumbuka ile ishara ya kidole cha kati....:mad2:...
BTW: Hili jukwaa linahusika na mambo ya kispoti kwani?


pia ni jukwaa la mahusiano
so hakuna kibaya kumpa maushauri

Hana hata kiwanja!!!! astagfillulah.....
 
TOA boriti kwanza kwenye jicho lako ndipo utaona kibanzi kidogo kwenye jicho la mwenzio.
Hapo ndipo watz wengi mnatofautiana na wapambanaji kama akina Slaa,kwani Slaa hana matatizo yake lakini ameweka wazi ya kwake mumsaidie na yale ya taifa tusaidiane!Acheni mzaha huyu kijana anahitaji msaada wako bila kujali eti wewe ni mpinzani wa Yanga.
Kwa taarifa yenu mimi ni mwanachama wa Yanga na kadi yangu ni namba 000243 unaweza kwanda kuhakikisha katika leja ya klabu.
Lengo langu ni kumsaidia na si kumtangazia mabaya la sivyo tungewaachia CCM waendelee kutafuna malighafi zetu eti kwavile nasi wapinzani tuna matatizo yetu,kuweni kiakili jamani na si kiumri tuu!
 
Haya majungu juzi kati hapa wamepimwa afya wachezaji wote wa Yanga na vipimo vilikuwa safi kwa wote.
Kaka Fidel80 ulitaka wamwage kuku kwenye mchele!Tafadhari mshauri kijana!
 

Inakuwaje wewe unakuwa shabiki wa Yanga! Maana tabia zako haziendani kabisa, jangwani hatuna wajinga wajinga wewe utakuwa na asili ya Pan African ama Yanga asili
 
Inakuwaje wewe unakuwa shabiki wa Yanga! Maana tabia zako haziendani kabisa, jangwani hatuna wajinga wajinga wewe utakuwa na asili ya Pan African ama Yanga asili
Kaka mchungaji ahsante kwa hii post!
 
Timu kubwa kama yanga haina mtaalamu wa ushauri nasaha na masuala ya saikolojia. Wangeajiri kocha asingekuwa na kazi kubwa kama hiyo
 
sasa huku ni kumtakia mema au kumtangaza ndugu yangu?

jee ww umechukua hatua gani ?

au ndio kuchafuana kileo?
 
sasa huku ni kumtakia mema au kumtangaza ndugu yangu?

jee ww umechukua hatua gani ?

au ndio kuchafuana kileo?
Mtu wa pwani tumsaidie kijana wetu,acha masihara!Unafikiri kwanini Alela alinipa taarifa hii?Kwa taarifa yako watu wengi wanaamini hapa JF kuna madaktari washauri wakubwa na kwavile mimi najulikana nipo hapa kurekebisha tabia za baadhi ya watu ndio maana Alela akaniomba kwa kupitia jukwaa hili tumpatie ushauri kijana mwenzie!
 
Jamani kweli Chuji hata ukimwangalia tu,utajua hayuko sahihi.jinsi anvyoonge,hata kutembea kwake.
Ushari wangu ni kwamba kama pombe au sigara kubwa ,na aache siyo nzuri katika maisha ya siku hizi.
Wachezajee bongo vipi jamani,sifa kidogo basiiiiiiiiiiiiiiii??? bichwa.
 

Kwanza Arudi Simba

Au aende kwa Mama Karume aliyesema "Ukichaguliwa kuchezea Yanga ujione kama mfalme". Tehe tehe.........Mfalme kafulia......
 

sounds like GPL! ... "Majungu"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…