JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Kuanzia Ofisi za Walimu, wamejibana kwenye chumba kimoja ambacho ubora wake unatia mashaka.
Eneo lingine la ofisi limeporomoka kutokana na uchakavu, hali hiyo inawalazimu Walimu kubanana kwenye kipande kidogo cha chumba kilichobakia.
Hali hiyo nimeambiwa kwamba imedumu kwa muda sasa, ambapo Walimu wakati mwingine wanalazimika kukaa kwenye kibalaza ili kutekeleza majukumu yao mfano wakiwa wanasahihisha madaftari ya Wanafunzi.
Nimesikitika sana kwa kuwa Shule hiyo Mjini Jijini tena katikati ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, eneo ambalo kikawaida nilitegemea miundombinu yake ingekuwa rafiki na yenye hadhi, kibaya zaidi hata baadhi ya vyumba vya madarasa vinaonekana kuchoka na kuchakaa.
Kwa hali niliyoshuhudia kwa macho yangu nitumie jukwaa hili kutoa wito wangu kwa mamlaka za Kiserikali ikiwemo Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, TAMISEMI wafuatilie suala hilo na kufanya marekebisho ambayo yatawaweka Walimu na Wanafunzi katika mazingira salama na rafiki.
Kuacha hali hiyo iendelee ni kuhatarisha usalama wa Walimu na Wanafunzi lakini vilevile inaweza kuchangia kushusha morali za Walimu katika kuwafundisha Wanafunzi wetu.