Jambazi akamatwa akitubu dhambi Kanisani

Jambazi akamatwa akitubu dhambi Kanisani

Bravo snr

Senior Member
Joined
Aug 16, 2020
Posts
182
Reaction score
477

Jambazi akamatwa akitubu dhambi Kanisani​

Pascal Mwakyoma TZA
on
April 13, 2021

d67e51f8e31f7eb7-660x400.jpeg

Kijana aitwaye Abraham Nduba, mwenye umri wa miaka 26 kutoka kaunti ya Murang’a nchini Kenya amekamatwa na kutupwa jela miaka mitano baada ya kuungama kanisani kwamba ni mwanachama wa genge la uhalifu eneo hilo.

Kijana huyo anayedaiwa kuwa ni jambazi sugu alifika kanisani akiwa mchangamfu na tayari kumpokea Yesu Kristu kama mkombozi wa maisha yake na alikiri kuwa mwanachama wa kundi la Gaica huku akitubu dhambi zake katika kanisa la Kianglikana la Maragua.

Inaripotiwa kwamba Nduba alikwenda kanisani humo bila kufahamu kwamba alikuwa anaandamwa na kikosi kizima cha Polisi.

Nduba aliingia kanisani bila kujua alikuwa ameketi pamoja na maafisa wa polisi waliokuwa wamevalia kiraia. Walimpa muda kutubu dhambi zake zote na kukubali kuishi maisha mapya kama pamba.

Punde baada ya ibada, pasta wa kanisa hilo Peter Kariuki aliarifiwa na polisi amsindikize Ndiba hadi katika Kituo cha Polisi cha Maragua ili ajisalimishe.

Pasta huyo alisimulia namna aliingiza baridi polisi walipomunyoshea bunduki na kuwaomba wamruhusu amwombee kondoo wake ambapo walikubali.

Kwa mujibu wa gazeti la Taifa Leo, Jumanne, Aprili 13, 2021 Abraham Nduba, mwenye miaka 26, alikamatwa mwezi mmoja baada ya kukwepa mtego wa polisi.

Nduba alikiri kuwa mwanachama wa kundi la Gaica huku akitubu dhambi zake katika kanisa la Kiangilakana la Maragua ambapo alikuwa amekwenda kuokoka.

Alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Sivai Agade, siku ya Jumatatu, Aprili 4,2021 ambapo alishtakiwa na makosa matatu ya uhalifu, uuzaji wa pombe haramu na kumiliki kampuni ya kutengeneza pombe haramu.

Nduba aliungama makosa yake na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani au faini ya KSh2 milioni.
 
Uhuwezi kuungama ukaeleza kila kitu kwa mchungaji, kunq dhambi zingine nzito ni Sir God tu anatosha
 
Waliyeanzisha mambo ya kutubu, ile ilikuwa njia ya kuwakamata watu waliyofanya uhalifu

Ova
 
Sijawahi kuielewa Logic ya kukiri dhambi zangu mbele ya binadamu mwenzagu.
Alikosea huyo mwamba , dhambi za wazi ndo unatubu Kwa wazi na Gharama yake inajulikana , dhambi za Siri hakuna mtu anayekujua , unakomaa na Mungu wako kimya kimya .....
Waliyeanzisha mambo ya kutubu, ile ilikuwa njia ya kuwakamata watu waliyofanya uhalifu

Ova
Uhuwezi kuungama ukaeleza kila kitu kwa mchungaji, kunq dhambi zingine nzito ni Sir God tu anatosha
Kuungama sio sawa , watumishu wengine ni spy
Kama nimeuelewa UZI vizuri ni kwamba hao police waliingia kanisani kumfatilia Abraham, hi maanake yake walikua wanamtafauta so hata kama asingeenda mbele kuungama bado wangemkamata but again sijaona mahali alipotaja madhambi yake kwa pastor; it sound (kwa nilivyo usoma uzi) huyu jamaa alikua anajulikana na vyombo vya dola na vilikua vinamfatilia kwa muda mrefu, huenda wameondoka nae nyumbani wakawa wanamfatilia kimya kimya bila ya yeye kujua kama anafatwa na police, wakajikuta wote wapo kanisani. Kwa mtazamo wangu, kuungama kwake kumemsaidi kutengeneza na Mungu wake (ingawa sijaona akitaja hayo makosa mbele ya mchungaji kwa mujibu wa UZI) bila kujali kitakacho mtokea huko mbeleni.
 
Jamaa kafata mkumbo wa wale wanaotoka mbele ya kanisa na kuungama wazi wazi mbele za watu.



Huwa sielewi inatokeaje mtu ana ugomvi na mwenzi wake nyumbani anaenda mbele ya kanisa kuyaongea akitaka suluhisho mara msamaha
 
Ana bahati sana huyo njemba, kwa ninavyowajua polisi wetu, yaani mpaka wamfuate kote huko ilikua wamuue afie mbali, labda jamaa kashtukia na kujipeleka kanisani ili apate pakutokea, na ile kwamba hakimu amemhukumu miaka mitano itakua jamaa hakuungamana madhambi yake yote, kataja vitu vidogo vidogo vya ksababisha afungwe kifungo cha muda mfupi.

Polisi wetu wahangaike kutoka kituoni ili wakufuatilie, raslimali zote hizo uwahangaishe, lazima wakutolee nje nje ufe wakipata mwanya au fursa, ila jamaa kacheza ndefu kwa kuingia kanisani na kumwaga mbele ya nyomi na kuwaacha mapolisi wakiwa solemba bila la ziada ila kumkamata kikawaida kawaida.

Jamaa akinyoosha tabia zake akiwa gerezani, kifungo kinaweza kikapungua hadi hata mwaka mmoja, kimsingi asome Biblia humo, ahubiri hubiri na kuimba nyimbo za sifa na asijiingize kwenye ugomvi wowote, sema kunao wanachama wenzie waliobaki nje wanaweza kuunda njama za kumdhuru ili asimwage mtama.
 
Hili ni kweli kabisa...kuungama kwa pastor ni mtego ambao wengi hawajaustukia[emoji848]
Chukulia mtu anaungama mbele ya mchungaji Modestus Kapilimba yule mchungaji balozi sasa wa Tz Namibia na aliwahi kua mkurugenzi wa usalama wa Taifa.
Nakumbuka mwaka flani nikiwa form 3 tulikua tunaokoka hivyo watu wanataja baadhi ya dhambi zao baada ya kuona mwanga wa wokovu, aisee nilisikia mambo makubwa sana kutoka kwa watu niliwaamini kiasi.

Dada mmoja Alyce yeye akasema mengi sana ila akawa anadai kuna vitu akitaka kuyasema ila zimekwama kooni hivyo anashindwa kuyasema....aliombewa sana ila ziligoma adi akahairisha na hatukumwona tena kwenye kundi la wapokea wokovu.

Duniani kuna mengi sana.
 
Back
Top Bottom