Ana bahati sana huyo njemba, kwa ninavyowajua polisi wetu, yaani mpaka wamfuate kote huko ilikua wamuue afie mbali, labda jamaa kashtukia na kujipeleka kanisani ili apate pakutokea, na ile kwamba hakimu amemhukumu miaka mitano itakua jamaa hakuungamana madhambi yake yote, kataja vitu vidogo vidogo vya ksababisha afungwe kifungo cha muda mfupi.
Polisi wetu wahangaike kutoka kituoni ili wakufuatilie, raslimali zote hizo uwahangaishe, lazima wakutolee nje nje ufe wakipata mwanya au fursa, ila jamaa kacheza ndefu kwa kuingia kanisani na kumwaga mbele ya nyomi na kuwaacha mapolisi wakiwa solemba bila la ziada ila kumkamata kikawaida kawaida.
Jamaa akinyoosha tabia zake akiwa gerezani, kifungo kinaweza kikapungua hadi hata mwaka mmoja, kimsingi asome Biblia humo, ahubiri hubiri na kuimba nyimbo za sifa na asijiingize kwenye ugomvi wowote, sema kunao wanachama wenzie waliobaki nje wanaweza kuunda njama za kumdhuru ili asimwage mtama.