Jambo ambalo lilikushangaza na hutolisahau baada ya kujiunga na elimu ya sekondari form 1

Antennah

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2015
Posts
6,754
Reaction score
8,750
Salaam.

Nilijiunga form one miaka kadhaa mingi iliopita.

Nilitokea shule ya msingi yakina sisi wanakayumba na kubahatika kuchaguliwa tena kuingia sekondari nayo ikiwa ni ya kata tu......madarasa manne tu vyoo vya kulenga....na ofisi ya waalimu ilikua ni darasa tu likabadilishwa matumizi.

Sio siri ile siku nimevaa suruali naingia darasani nikajikuta kila mda nachecheka mwenyewe kila nkikumbuka kuwa nimetoka kwenye mazoea ya kuvaa bukta.

JAMBO AMBALO SITOLOSAHAU...

Nikama baada ya week mbili kupita tukaanza kusoma.
Nakumbuka mwalimu wa physics alikua ndo yuko speed sana....siku ya tatu tu ya kusoma kwetu tukawa tumeingia ile topic ya ARCHIMENDES PRINCIPLE. (Ni density kama sijasahau)

Sio siri nilishangaa sana yule mzee aliposema eti inatakiwa tumeze gusestensi gote gule gwa Archimendes principle tena gwakingereza.

Yani kwa kifupi nilihisi anajaribu tu kuleta masihara kidogo mule darasani.

Darasa zima tulicheka mana tumetoka st kayumba na kizungu chenyewe hatuelew mpka mwalimu atafsiri kwa kiswahili tena kwa kurudia rudia, afu mtu anakuja tu et ""hii principle yote muimeze iwe kichwani"" khaaa......Tulihisi masihara tu anajaribu kuchekesha darasa kidgo......sio siri nilidata siku ile mpka kuanza kuhisi hata elimu ya sekondari labda nisingemaliza kwa kweli.

Sijui kwa nyie wenzangu....mi ilo ni moja ya mambo huwa nayakumbuka sana.
 

Attachments

  • images.jpg
    18.8 KB · Views: 87
ilikua noma sana ile....bt mambo yakaanza kuset yenyewe automatically[emoji16]
 
Ahsante sana.....yalipita lkn
 
weeeee phys ya advance mi mpka namaliza kuna topic zilikua zinanipiga chenga kabisaa yn....
 
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] sasa ww ndo ulihisi kule unaenda kula vikokosho tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…