Jambo ambalo umsamehe mpenzi wako kikawaida na asingesitahili msamaha

Jambo ambalo umsamehe mpenzi wako kikawaida na asingesitahili msamaha

Umeshasalitiwa kabla ya ndoa bado unaitaka ndoa tena na huyo huyo aliyekusaliti? Kishakuonyesha tabia yake kwanini hutaki kumuamini? 😳

Mume wa mtu itakuwa kwa hiyo huyo ni kimada tu, haiwezekani kwa mpenzi wa kawaida na kama una malengo ya kuwa pamoja kwa ndoa.
 
Dah acha kabisa. Wiki 3 ama 4 zilizopita. Girlfriend wangu nilimfumania na jamaa mwingine. Maumivu ya kufumania asikwambie mtu nlihisi mwili umeishiwa nguvu, nikaanza kutetemeka. Halikuwa fumanizi laiv bali kwenye simu maana nlipiga simu haikupokelewa nikarudia mara 3 ndo akapokea. Ss akajichanganya sababu ya hofu na jamaa akastuka. Mbaya zaidi usiku wa juzi kuamkia jana yake nlilala naye usiku kucha. Alivonidanganya nikagundua. Baada ya muda km dakika 10 nikamwamdikia kuwa "upo na mwanaume maana nimemsikia ana guna kwenye simu baada ya kusema uongo" kumbe zile dakika 10 kulikuwa na mtifuano jamaa akawa ameichukua simu.

Jamaa akanijibu ile sms kwa kusema amekudanganya nipo naye mm,
Sms ya pili akauliza unamtafuta huyu kwani mkeo.

Ndo hali mbaya ikanitokea sikuweza hata kuwa na nguvu ya kuandika sms. Nlikaa km nusu saa ndo hali akarudi sawa.
Ikumbukwe mdada huyu anapoushi mm ndo nalipia, fanicha zote nimemnunulia mm, nalipa kila kitu hadi chakula namlisha mm. Simu nilojibiwa pumba nliinunua mm wiki 2 zilizopita ni smart ya laki1 20elf. Vocha naweka mm,
Nikajibu hiyo sms nikimwambia jana nimelala na huyo dada usiku kucha, na nikamweleza gharama ninazomgarimikia. Kumbe jamaa aliizima sim baada ya kumpora.

Baadae jion mwanamke anaanza kunitafta anaapology.nikamwambia its over. Nakuachia kilakitu ila kuanzia sasa jamaa atake charge.

Dem alikuja nimekaa naye kwenye gari lisaa zima amepiga magoti analia. Nikamwacha ila baada ya wiki nikafikiria nikaamua kumsamehe. Nikapanga naye safari tukarnda kenya kupoteza mawazo kidogo bado akanitibua hukohuko tulika 3 days ila akati tunarudi njia nzima hatukuongea na tulitumia gari binafsi.
Hapa napanga nimwekee sub ya nguvu.
Daah mzee kweli wanaumee tumepungua

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Wakuu tulirudiana nikamsamehe tukaendela, tukakorofishana tena baada ya wiki tu tukaachana, tukarudiana tena. Juzi nimekubali yaishe, nimemwacha serious sasa. Ila anaishi kwenye hostel zangu, ni mwanachuo, nimemwambia froma next month ataanza kulipia kila kitu. Ila sasa simu aliyonayo nataka nimnyanganye sababu nasikia uchungu simu yangu ndo anaitumia kuchat na mabwana zake. Vitu vingine nitamwachia vyote
View attachment 1602722
Utoto unamsumbua... sio kwamba hakupendi...
 
Wakuu tulirudiana nikamsamehe tukaendela, tukakorofishana tena baada ya wiki tu tukaachana, tukarudiana tena. Juzi nimekubali yaishe, nimemwacha serious sasa. Ila anaishi kwenye hostel zangu, ni mwanachuo, nimemwambia froma next month ataanza kulipia kila kitu. Ila sasa simu aliyonayo nataka nimnyanganye sababu nasikia uchungu simu yangu ndo anaitumia kuchat na mabwana zake. Vitu vingine nitamwachia vyote
View attachment 1602722
Msamehe tu, hata simu usimpokonye mwache aanze maisha mengine bila wewe.
 
Back
Top Bottom