Jambo gani ambalo uliwahi kulipania kwa hamu kubwa kulipata baadaye likakushinda?

Jambo gani ambalo uliwahi kulipania kwa hamu kubwa kulipata baadaye likakushinda?

proton pump

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
6,814
Reaction score
10,104
Natumaini hamjambo wana jukwaa na mnaendelea vyema

Katika harakati za kimaisha kuna mambo mbalimbali ulipania kuyapata au kuyafanya ila baadae yakakushinda na ukaachana nalo kabisa ama ukapambana tu bila kukata tamaa lakini hola.

Yapo mambo mengi kama vile,
kupata ramani za kwenda abroad, Marekani, uingereza....​
Kukutana na kiongozi mkubwa wa kisiasa au kidini....​
Kumiliki hela nyingi, magari nyumba n.k........hii ndoto ya kila mtu.​
Kuwa na elimu kubwa PhD......​
Kukutana me au ke uliyempania siku nyingi lakini siku hiyo unajaribu lakini huna hisia kabisaa........​
Kupumzika siku za likizo au baada ya kumaliza mtihani lakini siku hiyo usingizi hauji kabisaa ........​
Kulima mashamba makubwa unakuja kushangaa mavuno kidogo.......​
usisite kufollow nofap​
 
Nikipata mwanamke mnenguaji. Akiwa jukwaani anakatika sana. Kweli nilimpania sana na nilipanga kazi Ile namwachisha. Kufika uwanja wa sita kwa sita katulia kama gogo na Wala hainengulii... Alinishinda
 
Back
Top Bottom