Kuna demu alinipenda sana kipindi hicho, nimechoka vibaya sina mbele wala nyuma, lakini bado yule mtoto aliendelea kuniganda na kunisikiliza. Mwaka nilipohitimu shahada, yeye pia alihitimu stashahada. Mwenzangu akapata kazi kabla yangu na alipata kazi mkoa tofauti na ule tulioishi, lakini alikuwa anafunga safari kunifata kwa gharama yake. Sitoi hata mia na alikuwa akija, tunaenda zetu lodge, tunalala siku mbili au tatu, tunakula kwa gharama zake. Kipindi hicho bado ninaishi kwa wazazi, na akiondoka bado ananiachia pesa. Tulidumu kwenye mahusiano kwa miaka isiyopungua mitano. Kimsingi kulikuwa na sura nzuri na umbo la kawaida, hakua flat screen, kitu ambacho sikipendi kuhusu yule mwanamke ni miguu. Alikuwa na miguu myembamba sana, jamani, na yeye mwenyewe alijua hilo. Tukikaa, alikuwa anasema kabisa, "Mmm, miguu yangu mibaya."
Kipindi nilipomwacha, sikuweza kumwambia tuachane, ila matukio niliyokuwa nampiga, plus kukaa kimya bila hata kumjulia hali zaidi ya siku mbili, akajiongeza tuuu kwamba ashapigwa chini, na ndio ukawa mwisho wetu. Alikuja kunitext WhatsApp miezi kadhaa baadaye, tukachati kidogo, na akaniambia, "Wewe mwanaume, nilikupenda sana, lakini haikuwa riziki yangu," nikaishia kucheka tuuu.
Nikiri tu kwamba tangu niachane na yule binti, sikuwahi tena kupata mwanamke aliyenipenda kama vile. Sasa ameshavishwa pete ya uchumba, hivi karibuni ataolewa.