Jambo gani baya umewahi kumfanyia mpenzi wako na utajutia milele?

Wivu
 
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Nimeipenda hii
 
Kuna demu alinipenda sana kipindi hicho, nimechoka vibaya sina mbele wala nyuma, lakini bado yule mtoto aliendelea kuniganda na kunisikiliza. Mwaka nilipohitimu shahada, yeye pia alihitimu stashahada. Mwenzangu akapata kazi kabla yangu na alipata kazi mkoa tofauti na ule tulioishi, lakini alikuwa anafunga safari kunifata kwa gharama yake. Sitoi hata mia na alikuwa akija, tunaenda zetu lodge, tunalala siku mbili au tatu, tunakula kwa gharama zake. Kipindi hicho bado ninaishi kwa wazazi, na akiondoka bado ananiachia pesa. Tulidumu kwenye mahusiano kwa miaka isiyopungua mitano. Kimsingi kulikuwa na sura nzuri na umbo la kawaida, hakua flat screen, kitu ambacho sikipendi kuhusu yule mwanamke ni miguu. Alikuwa na miguu myembamba sana, jamani, na yeye mwenyewe alijua hilo. Tukikaa, alikuwa anasema kabisa, "Mmm, miguu yangu mibaya."

Kipindi nilipomwacha, sikuweza kumwambia tuachane, ila matukio niliyokuwa nampiga, plus kukaa kimya bila hata kumjulia hali zaidi ya siku mbili, akajiongeza tuuu kwamba ashapigwa chini, na ndio ukawa mwisho wetu. Alikuja kunitext WhatsApp miezi kadhaa baadaye, tukachati kidogo, na akaniambia, "Wewe mwanaume, nilikupenda sana, lakini haikuwa riziki yangu," nikaishia kucheka tuuu.

Nikiri tu kwamba tangu niachane na yule binti, sikuwahi tena kupata mwanamke aliyenipenda kama vile. Sasa ameshavishwa pete ya uchumba, hivi karibuni ataolewa.
 

Aisee pole sana mkuu hii iwe fundisho sasa
 
Kuna dem nilimkopesha ela nyingi tu baada ya kuja analia na shida kibao alaf mda wa kulipa akaanzaga nyodo dadeq nikamuitaga geto kiroho Safi nilichomfanyiaga ni zaidi ya thamani ya pesa niliyompa na roho yangu ikaridhika
 
Hao wapenzi wako ulikuwa mzigo kwao kwakuwa hata kuandika hujui. Ni heri uliachana nao wapate watu sahihi.
Sio kila mtu kafundishwa kusoma na kuandika na mwalimu juma ...wengine kiswahili wamejifunzia ukubwani toka nje ya box
 
Sio kila mtu kafundishwa kusoma na kuandika na mwalimu juma ...wengine kiswahili wamejifunzia ukubwani toka nje ya box

Walimu kila sehemu yeye anajua ni darasani.anaacha kujikita kwenye mada yeye anaanza kutafuta makosa ya kiuandishi wa herufi za R na L[emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…