Jambo gani la kijamii umekuwa ukilisikia, bila kupata majibu JamiiCheck ilifanyie uhakiki?

Jambo gani la kijamii umekuwa ukilisikia, bila kupata majibu JamiiCheck ilifanyie uhakiki?

JAMII CHECK SWALI 212.jpg

Jukwaa la Jamiicheck lipo mahsusi kwa ajili ya kufanya uhakiki wa taarifa ili kujua kama ni kweli, uzushi au nadharia.

Hukuwezesha raia kufanya uhakiki kwa kuweka maudhui ndani ya jukwaa yanayotakiwa kuhakikiwa na kutoa mchango wa kuhakiki taarifa hizo kwa kile wanachokifahamu.

Je, ungependa Jamiicheck ihakiki jambo gani la kijamii ili upate kujua uhalisia wake?
 
Ifatilie kama walimu wamepewa elimu juu ya matumizi ya mtandao hasa namna ya kujiunga na mifumo inayo tolewa maagizo kila uchwao
 
Ni kweli maji ya mvua yana madhara kwa afya ya binadamu ?

Siku moja dar es salaamu mahali nilipo panga niliwahi kutoa wazo kuwa tutengeneze mfereji wa kukingia maji yanayotok kwenye bati , baada ya kuona maji mengi yanapotea nasis Tunapat tabu kunywa maji ya chumvi, au yale ya DAWASA.

Dada mmoja na wenzake waliniambia maji ya mvua ni mabaya kiafya kutokana ya Anga hewa kukusanya moshi mchafu wa viwanda ,hivyo mvua inaponyesha huja na zile kemikali, Niliingiwa na shaka na sikuendelea na kampeni ya kutaka tuweke mfereji. Kwenu studio naomba ufafanuzi zaidi.
 
Back
Top Bottom