Jambo gani la kijinga ulikuwa unatamani litokee ukiwa mtoto?

Jambo gani la kijinga ulikuwa unatamani litokee ukiwa mtoto?

Nilikuwa natamani litokee tatizo kubwa shuleni ili tupate walau siku chache za mapumziko [emoji23] [emoji23].
Pia nilikuwa natamani sana atokee mwizi aibe nguo zangu zote za shule ili wakati wanajipanga kuninunulia zingine nipate muda wa kukaa home
 
Elimu ingekuwa hiyari shule nyingi za msingi zingefungwa hahaha
 
Kuona ukingo wa mwisho wa Dunia.

Nakumbuka nilitembea sana yote kutaka kuona mwisho wa mawingu na mwisho wa mawingu nilifikiri ndiyo ukingo wa Dunia kwa hiyo nikiyaangalia mawingu naona aaah! Kumbe karibu, kumbeeee!
 
nilikuwa nikiona ndege(aeroplanes) zinapita natamani siku moja idondoke jirani na homu ili niione kwa karibu na niokote vitu.

watoto wa kitaa, ujinga unawazwa tangu hatujui mema na mabaya.
kuna siku unakuta michezo imekolea mpaka unatamani usiku usiingieo
 
Nilitamani sana siku moja serikali itangaze shule zote zifutwe na watoto kuanzia siku hiyo wawe mitaani na kucheza tu.
 
Nilipenda vita itokee ,watu wakimbie waache maduka yao nichukue vutu kama pipi,biscut nijaze kwenye mfuko nikimbie huku nakula njian...utoto ufala sana
 
Back
Top Bottom