Jambo gani lililowahi kukufanya ujisikie aibu/Ujivunie Utanzania wako?

greater than

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
1,653
Reaction score
3,060
Niliyojivunia:

1. Nilipata safari ya kikazi mkoani Kagera wilaya ya Ngara. Kwenye lile basi raia wengi walikuwa ni wa Rwanda na Burundi. Wakati nipo kwenye basi, nilishuhudia wale jamaa walikuwa wakiongea kwa kuangaliana makabila tu, yaani Mhutu kwa Mhutu au Mtutsi kwa Mtutsi hata kama wamekaa siti moja, Mhutu na Mtutsi hawaongeleshani.

2. Nilienda kikazi nchini Zambia, nyimbo za wasanii wa Bongo zinapigwa sana. Diamond, Harmonize, Rayvan ni majina maarufu.

3. Nilienda Malawi kikazi, nilipata bidhaa nyingi sana zinazotoka makampuni ya Bongo, kama vile vinywaji vya Azam na Mo. Sheli za kampuni ya Meru ni nyingi sana. Barabara za Bongo ni nzuri sana.

4. JWTZ:
- Ilizuia mapinduzi Comoro.
- Imesaidia kupata amani Msumbiji.
- Ilisaidia Malawi katika mafuriko.

Ya haibu:

1. Katika safari ya Zambia, wale wajamaa ni waaminifu sana, hawana longolongo kwenye biashara. Kulikuwa na story nyingi sana za wafanyabiashara wa Zambia waliotapeliwa Bongo.

2. Mbunge fulani kusimama bungeni na kuuliza, "Kwanini Serikali imesitisha uzalishaji/usambazaji wa sarafu kama shilingi 1, shilingi 5 na 10, haioni kama watoto watakuwa hawazijui?" Cha haibu ni kuwa huyu mbunge ameshawahi kukaa ikulu kwa miaka 10, yani alipataje ubunge hutu.

3. Kiongozi mkubwa kutoa tamko la kuzuia asiyeoga kufika katikati ya Jiji la Dar. Halafu ilikuwa kipindi cha joto kali sasa.

Matukio ya haibu ni mengi...
 
Nenda Ulaya na Marekani sasa.

Kule ukisema unatokea Tanzania wanakuuliza Iko wapi hii?

Ukiwapa ufafanuzi kuwa ni Nchi inayomiliki Mlima Kilimanjaro, wanakwambia mbona huu Mlima sisi tunajua uko Kenya?

"Haibu" sana..
 
.........Kwenye lile basi raia wengi walikuwa ni wa Rwanda na Burundi. Wakati nipo kwenye basi, nilishuhudia wale jamaa walikuwa wakiongea kwa kuangaliana makabila tu, yaani Mhutu kwa Mhutu au Mtutsi kwa Mtutsi hata kama wamekaa siti moja, Mhutu na Mtutsi hawaongeleshani.
Wahutu na Watusi lugha yao ni moja Kinyarwanda. Hakuna lugha inayoitwa ya kabila la Kitusi au ya Kuhutu.

Labda useme walikuwa wanaongeleshana kwa kuangalia urefu wa pua, wembamba wa miili na urefu wa kimo
 
😂😂😂😂😂 nlijua tu hii “haibu” italeta shida, mleta mada ni mtanzania wa wapi mbona “haibu” naona mimi
Yaani ,hata sikuliona hilo kosa...
Ila nichambeni, itafanya niongeze umakini kwenye uandishi...
🤣🤣🤣🤣
 
Wahutu na Watusi lugha yao ni moja Kinywarwanda. Hakuna lugha inayoitwa ya kabila la Kitusi au ya Kuhutu.

Labda useme walikuwa wanaongeleshana kwa kuangalia urefu wa pua, wembamba wa miili na urefu wa kimo
Wao wenyewe walikuwa wanatambuana kwa kuangaliana tu...
Kama ilivyo huku tunavyoweza tambuana.
 
aibu yangu nikuona mtanzania kama wewe kuandika "haibu" badala ya aibu!.
Ngoja kwanza nikafanye yangu ninachojivunia mtanzania ni Busara za Uhuru wa watu na Utu wao siku hizi watu wakishika Mwizi msumbufu hawampigi na mawe na kumuua km zamani anashikwa anafikishwa kituoni moja kwa moja Mahakamani anagongewa nyundo akawe meneja mkubwa huko Ukonga Magereza
 
Niliyojivunia:

1. Nilipata safari ya kikazi mkoani Kagera wilaya ya Ngara. Kwenye lile basi raia wengi walikuwa ni wa Rwanda na Burundi. Wakati nipo kwenye basi, nilishuhudia wale jamaa walikuwa wakiongea kwa kuangaliana makabila tu, yaani Mhutu kwa Mhutu au Mtutsi kwa Mtutsi hata kama wamekaa siti moja, Mhutu na Mtutsi hawaongeleshani.

2. Nilienda kikazi nchini Zambia, nyimbo za wasanii wa Bongo zinapigwa sana. Diamond, Harmonize, Rayvan ni majina maarufu.

3. Nilienda Malawi kikazi, nilipata bidhaa nyingi sana zinazotoka makampuni ya Bongo, kama vile vinywaji vya Azam na Mo. Sheli za kampuni ya Meru ni nyingi sana. Barabara za Bongo ni nzuri sana.

4. JWTZ:
- Ilizuia mapinduzi Comoro.
- Imesaidia kupata amani Msumbiji.
- Ilisaidia Malawi katika mafuriko.

Ya haibu:

1. Katika safari ya Zambia, wale wajamaa ni waaminifu sana, hawana longolongo kwenye biashara. Kulikuwa na story nyingi sana za wafanyabiashara wa Zambia waliotapeliwa Bongo.

2. Mbunge fulani kusimama bungeni na kuuliza, "Kwanini Serikali imesitisha uzalishaji/usambazaji wa sakafu kama shilingi 1, shilingi 5 na 10, haioni kama watoto watakuwa hawazijui?" Cha haibu ni kuwa huyu mbunge ameshawahi kukaa ikulu kwa miaka 10, yani alipataje ubunge hutu.

3. Kiongozi mkubwa kutoa tamko la kuzuia asiyeoga kufika katikati ya Jiji la Dar. Halafu ilikuwa kipindi cha joto kali sasa.

Matukio ya haibu ni mengi...
Fedheha na aibu nyingine ni Mtanzania mtoa mada asiyejua kuandika AIBU, yeye anaandika HAIBU. Huko Zambia na Malawi nadhani alijinadi anajua Kiswahili vizuri.
 
Niliyojivunia:

1. Nilipata safari ya kikazi mkoani Kagera wilaya ya Ngara. Kwenye lile basi raia wengi walikuwa ni wa Rwanda na Burundi. Wakati nipo kwenye basi, nilishuhudia wale jamaa walikuwa wakiongea kwa kuangaliana makabila tu, yaani Mhutu kwa Mhutu au Mtutsi kwa Mtutsi hata kama wamekaa siti moja, Mhutu na Mtutsi hawaongeleshani.

2. Nilienda kikazi nchini Zambia, nyimbo za wasanii wa Bongo zinapigwa sana. Diamond, Harmonize, Rayvan ni majina maarufu.

3. Nilienda Malawi kikazi, nilipata bidhaa nyingi sana zinazotoka makampuni ya Bongo, kama vile vinywaji vya Azam na Mo. Sheli za kampuni ya Meru ni nyingi sana. Barabara za Bongo ni nzuri sana.

4. JWTZ:
- Ilizuia mapinduzi Comoro.
- Imesaidia kupata amani Msumbiji.
- Ilisaidia Malawi katika mafuriko.

Ya haibu:

1. Katika safari ya Zambia, wale wajamaa ni waaminifu sana, hawana longolongo kwenye biashara. Kulikuwa na story nyingi sana za wafanyabiashara wa Zambia waliotapeliwa Bongo.

2. Mbunge fulani kusimama bungeni na kuuliza, "Kwanini Serikali imesitisha uzalishaji/usambazaji wa sakafu kama shilingi 1, shilingi 5 na 10, haioni kama watoto watakuwa hawazijui?" Cha haibu ni kuwa huyu mbunge ameshawahi kukaa ikulu kwa miaka 10, yani alipataje ubunge hutu.

3. Kiongozi mkubwa kutoa tamko la kuzuia asiyeoga kufika katikati ya Jiji la Dar. Halafu ilikuwa kipindi cha joto kali sasa.

Matukio ya haibu ni mengi...
Mimi nimeona aibu kwa Mtanzania kama wewe kuandika Sakafu badala ya Sarafu.
 
Back
Top Bottom